Elections 2010 "Watanzania ni watu wanaopenda umoja na amani" !!!!!!! Sijaelewa nisadieni

Vumbi

Senior Member
Nov 7, 2010
191
27
"Watanzania ni watu wanaopenda umoja na amani" ukimsika mtanzania anayetamaka haya maneno ni wakuogopa sana. Hivi kuna amani na umoja gani wakati wengine hawana chakula cha kula hata kwa siku moja, hawana huduma afya hata kwa kiwango cha zahanati, hawawezi hata kulipa ada ya shule ya kata 20,000/= kwa mwaka, anaishi nyumaba ya tembe au majani? nk

Hivi kuna amani na umoja gani wakati hapa Dar penyewe mtu huwezi kupokea simu ya mkononi kwa amani kwa kuogopwa kuporwa? Vijani wamejazan kila kijiwe wakirandaranda bila kazi ya kufanya?

Hivi kuna amani na umoja gani wakati kunawatanzania mamilionea tena watumishi wa-Uma ambao hawawezi hata kueleza utajiri huo wameupata kivipi?

Hivi amani na umoja kwa watanzani ni nini?

Hivi kwanini watu waonao hubiri amani na umoja ni wale wenye-maisha mazuri? hawa wanaogopa nini? au hawa wenzetu amani na umoja kwao nin nini?

Nimejaribu kutafakari hii amani na umoja nimeshindwa kupata jibu. Naomba wenzangu mnisaidie mnamaanisha nini amani na umoja wa Tanzania?
 
Back
Top Bottom