Watanzania ni Dhaifu!!

BIG X

JF-Expert Member
Nov 4, 2011
777
212
Najaribu kutofautisha upole na udhaifu. Hivi sisi waTZ ni wapole au wadhaifu!, Mambo mengi yanayofanywa na serikali yetu dhaifu ingekuwa ni nchi nyingine kama kenya tu hapo mfano tungekuwa tunaongea mengine saahizi, sababu wananchi wasingekubali kuonewa kiasi hiki. Sababu tunaimba Amani kila siku, lakini ni amani gani hii ambayo tunayo wakati roho zetu zinateseka kila siku!!. Wakati mwingine tunamkosea Mungu kumuomba atusaidie wakati sisi wenyewe hatujisaidii, huu ni ujinga!. Napata wasiwasi kusema waTZ ni wapole, mi nadhani sisi waTZ ni wadhaifu na ndio mana tunakubali kuongozwa na serikali na viongozi dhaifu!!.
 
Umenikumbusha mbali sana, kuna wakati nilikuwa na jamaa zangu wa nchi nyingine akiwemo mkenya, katika maongezi nikaambiwa tatizo lenu watanzania ni wadhaifu, halafu nyie mnajidanganya ni wapole na wakarimu!. Inawezekana huu upole na amani tunajidanganya wenyewe au kudanganywa na viongozi wetu, tumekubali kudanganyika. Kwahiyo hiyo inawezekana kabisa wakati sisi tunajiona wapole/wakarimu/watu wa amani kumbe nchi zingine wanatuona ni wadhaifu.
 
Yaani kweli tupu mkubwa, Zaidi tunajidanganya na MBIO ZETU TOKEA UHURU NA MAFANIKIO kumbe ni UONGO MTUPU
 
Ni kweli kabisa ni watu wa mboyoyo tuu vitendo hakuna...

Tunapenda majungu tu!!, kufanya kazi wavivu, kusoma wavivu, tunapenda kuombaomba tu na vitu vya bure. Tusipokuwa makini ipo siku vitatutokea puani!.
 
Tunapenda majungu tu!!, kufanya kazi wavivu, kusoma wavivu, tunapenda kuombaomba tu na vitu vya bure. Tusipokuwa makini ipo siku vitatutokea puani!.
Ha ha ha, kama wewe mkuu, full uvivu kazini muda wote JF!
 
Watu kama wewe wavivu wa kufikiri ndio mnaotuwekea viogozi dhaifu madarakani.

Wewe jasiri so far umefanya nini? kama siyo kupiga maneno humu JF? Lisongeshe kama kamanda Dr. Ulimboka tukuone!
 
Wewe jasiri so far umefanya nini? kama siyo kupiga maneno humu JF? Lisongeshe kama kamanda Dr. Ulimboka tukuone!

Kama we uko safi fanya hiyo hesabu hapo chini, nakupa dakika 5.

3[SUP]x[/SUP]=9x, what is x, onyesha njia. ukishindwa jitukane mwenyewe kwamba we ni dhaifu.
 
Kama we uko safi fanya hiyo hesabu hapo chini, nakupa dakika 5.

3[SUP]x[/SUP]=9x, what is x, onyesha njia. ukishindwa jitukane mwenyewe kwamba we ni dhaifu.

Ha ha haaa, kaka kweli sasa unataka kuniambia Maths ndo kipimo ja ujasiri? Sikupi njia, kula jibu ni 3!
 
Uliyeanzisha hii thread ni dhaifu zaidi, vinginevyo ungeisha chukua hatua zaidi ya kulalamika tu kama PM Pinda.
 
Uliyeanzisha hii thread ni dhaifu zaidi, vinginevyo ungeisha chukua hatua zaidi ya kulalamika tu kama PM Pinda.

1 gawanya kwa 0 ngapi, haya tuone na wewe udhaifu wako, nakupa 0 seconds.
 
Back
Top Bottom