Watanzania nani katuroga?

Tumerogwa?! Hapana hakuna kitu kama hiko!. Ila UJINGA, UMASKINI, MARADHI NA ULOFA ndio matatizo yetu!
 
Ahaha leo ktk analysis ya match ya simba sc commentator kuzungumzia stahiki watakazo pata baada ya kuvuka semi-final ni sawa na kutumia 50k imekaa tu kwa miaka 54, wadau wamejadili hii kitu kwa hisia mpaka nikacheka.Kwakweli tz bwana ahaha
 
Hakika jambo hili linasikitisha na kufikirisha sana. Jana nilikuwa na mtu akasema, hivi kwanini Lisu anahangaika, si atulie yeye na familia yake? Nilimtazama kwa hasira, kisha nikamwambia, nchi yetu inaangamia kwa sababu ya ukimya wa watu kama yeye. Nikaondoka. Tunahitaji kubadilika kifikra.
 
Mabadiliko yananza na sisi sio Kwa kubandika bila matendo
 
ndo maisha tuliyoyachagua haya.utaumiza akili bure
 
Hawa vijana wenyewe wanakesha kwenye mabanda umiza kubishana simba+yanga? Sijui Barcelona kafanya nin, na wengine siku kucha kufatilia umbea, mabirthday parts, kushinda makanisani kuomba miujiza na mambo ya kipuuzi, sasa huo mda wa kudiscuss mambo ya msingi watanzania watoe wapi?.
Asilimia kubwa ya watanzania ni wavivu na waoga wa kujifunza mambo mapya yanayotumia akili ndiomaana wanaamua kupoteza muda ktk mambo ya kipuuzi,

ili akili za watanzania ziamke ni either ipite mijeredi mikali ya kuamsha akili zao kupitia anguko la uchumi au, kutokea mfumo fulani mgumu ktk maisha au aje kiongozi atakayejenga fikra mpya kwa vijana, tofauti na hapa tutaendelea hivi hivi kuonewa na hawa viongozi wetu majizi na mitaani raia hawahoji zaidi ya kushabikia mambo ya hovyo.

Hili taifa kwa sasa tunaenenda kama mazombi tu kila kiongozi anajifanyia atakalo na hakuna wa kumtisha.
 
Mabadiliko yananza na sisi sio Kwa kubandika bila matendo
Me ninawaza tu mkuu, watu zaidi ya 60 millions, kwenye nchi iliyojaaa kila aina ya utajiri, tunakosa hata kiwanda cha chuma, magari, pikipiki, battery, tires? Mwl. Nyerere aliwezaje? Sisi kama taifa tunashindwaje? basi tufanye sisi hamnazo, hata kuweka mazingira mazuri ya wawekezaji tunashindwa?
 
Yes , remember report ya CAG prof Assad kipindi cha magufuli, 1.5 tillion ilipotea, then watanzania habar hiyo ikapita tu kama inaaga maiti, yaan hatuna habar nazo, ila za mwijaku , simba , yanga ndyo vipaumbele vyetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…