Watanzania nani ameturoga?

senkoP

Senior Member
Aug 28, 2017
160
173
Jamani mimi huwa nashangaa sana mara nyingi nikiingia kwenye mitandao ya kijamii hususani Facebook WhatsApp na Twitter utakuta mtu kaandika mambo ya ajabu ajabu tena matusi yaani utakuta like kibao na comments zaidi ya 5mil.

Lakini tena utakuta mtu kaandika mambo muhimu labda ya kuelimisha jamii jambo flan either inshu za malezi, Kilimo bora, ufugaji au mambo ya ujasiriamali, au mambo ya dini yaani utakuta like moja ama comments 1, hili jambo huwa linanishangaza sana kwa mfano kuna kapage flani kanaitwa HELLO TZ kwakweli mambo yanayo postiwa kule na watu wanavyoshabikia utadhani ni mambo ya maana.

Kwakweli naona tumekosa maadili sisi kama Watanzania baada ya kuchangia mambo ya msingi ambayo yanafundisha jamii lakini tumepotoka......sijui nani katuroga!
 
Mkuu acha kabisa ,nilichogundua ngono inawashabiki wengi kuliko tasnia yeyote hapa duniani
 
Inaonekana unapenda Mathematics , zaidi ya Movie.

Hilo Jambo Ni dunia nzima
 
Jamani mimi huwa nashangaa sana mara nyingi nikiingia kwenye mitandao ya kijamii hususani Facebook WhatsApp na Twitter utakuta mtu kaandika mambo ya ajabu ajabu tena matusi yaani utakuta like kibao na comments zaidi ya 5mil.

Lakini tena utakuta mtu kaandika mambo muhimu labda ya kuelimisha jamii jambo flan either inshu za malezi, Kilimo bora, ufugaji au mambo ya ujasiriamali, au mambo ya dini yaani utakuta like moja ama comments 1, hili jambo huwa linanishangaza sana kwa mfano kuna kapage flani kanaitwa HELLO TZ kwakweli mambo yanayo postiwa kule na watu wanavyoshabikia utadhani ni mambo ya maana.

Kwakweli naona tumekosa maadili sisi kama Watanzania baada ya kuchangia mambo ya msingi ambayo yanafundisha jamii lakini tumepotoka......sijui nani katuroga!
Mkuu hii yote inatokana na malezi ambayo wengi wamekuwa nayo katika familia zao hakuna lingine watu wamrudie Mungu wazàzi tulee watoto wetu katika hofu ya kumju Mungu tàngia wakiwa wadogo tuwaombee na kuwafundisha neno la Mungu inaweza kusaidia kuwaondoa huko walipo.
 
Hii mitandao ni free stress zone na intertainment... Masuala ya maendeleo we nenda field..usitazmie kuona la maana huko zaid ya matusi..nakushauri kama wanakukera fanya kuwa unfollow tu
 
Mkuu ni kweli kabisa unayoyasema mfano kuvunjika kwa ndoa ya pique na shakira wazungu hawana time na habari hzo hata comment na like zinakuwa chache ila wabongo sasa wanatoa mpaka sababu za kuachana haya njoo kwa hawa mastaa wetu wanakesha wanapost upuuzi tu wakati mastaa wa nchi nyingine wanakaa mpaka week hawapost na wakipost ni issue za maana kweli afya ya akili inalisumbua taifa.
 
Maisha ya bongo ni magumu kichizi kiasi kwamba yamejaa stress tupu so, nahisi hilo ni jambo linafanya mtu kuona mitandao ya kijamii ni moja ya sehemu itakayomuondoa stress, Na suala la ngono linapendwa na watu wengi automatically mfano mzuri kumbuka kipindi tunasoma, Topic karibu zote zilikuwa sio favorite kwa wanafunzi ila ilipofika kwenye Topic ya Reproduction hamna aliekuwa hapendi.... So me kwa hilo nadhani Ngono ina mijadala mingi mno so kufanya iwe topic ambayo ina njia nyingi kuiletea mjadala jambo ambalo linafanya mtu asichoke kufuatilia kila aonapo post yenye ngono ndani.... Mmoja atapost "Jana nimekunwa" mwingine atapost " Jana nimekuna" zote ni mada zilezile ila kila mtu atatoa comment yake kwa ufahamu wake.... Kuna atakaetaka umpe story ilikuwaje, Kuna atakaekuchamba uache ushamba, Kuna atakaekupongeza, Kuna atakaecheka tu.... so ipo hivyo.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom