Watanzania na umasikini wetu

FILOMBE

Member
Mar 2, 2012
27
0
Habari wana JF.

Nimetafakari kwa kina sana juu ya huu umasikini wetu unaotukabili Watanzania kama taifa na kama Mtanzania mmoja mmoja. Umasikini huu unaotukabili ni wa aina 2, umasikini wa kwanza ni ule wa kujitakia wenyewe na mwingine ni ule wa kupandikizwa.

Umasikini wa kujitakia ni ule ambao Taifa la Tanzania lina kila kitu kwa maana ya rasilimali kama Ardhi,Watu, Madini, Misitu, Bahari na Maziwa lakini hakuna jitihada zozote za makusudi zinazochukuliwa na sisi wa Tanzania kujinasua kutoka hapa tulipo kwa kuzitumia rasilimali hizi kusonga mbele kama ambavyo wenzetu wengine ulimwenguni wanavofanya kwa kutumia rasilimali zao kusonga mbele katika nyanja ya maendeleo. Kwa Mtanzania mmoja mmoja ni pale ambapo Watanzania tuna uwezo wa kufanya kazi kwa bidii lakini kutokana na tabia yetu ya kupenda kuzungumza tu kwa mipango mingi lakini bila kujituma. Unakutana na mtu ni mjuzi mzuri sana kwa maana ya kuelimika na ana nguvu na afya njema lakini ni mvivu anashindwa kufanya kazi kwa bidii. Hapa umasikini ni mgumu kuweza kuepukana nao.

Umasikini wa pili ni ule wa kupandikizwa, hapa Taifa kama la Tanzania linazidiwa ujanja na Mataifa mengine. Yaana watu wasio Watanzania wanapotumia utajiri wetu kwa maana ya rasilimali zetu kujineemesha wao kama Nchi na Kama wageni mmoja mmoja. Sasa katika aina hii ya umasikini ni suala la mikataba na mbinu wanazotumia wenzetu wageni kuhakikisha kwamba wana tunyonya kwele kweli. Sera za kimataifa ambazo zimekuwa kandamizi kwa Nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania. Ni hapa sera hizi kandamizi zilianza tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia na pale mhimili mmoja wa Kijamaa (Socialist) ulipoanguka, huo ulikuwa ni mwanzo mbaya wa mataifa yetu kupandikiziwa umasikini. Umasikini wa Mtanzania mmoja mmoja ni ule unaopandikizwa na mfumo wa Nchi yetu wenyewe kutoka kwa Watawala wetu, pale wanaposhindwa kusimamia muundo wa kiutawala yaani utawala wa sheria unaowezesha mgawanyo wa rasilimali zetu kwa usawa. Mfumo wa Upendeleo na ufisadi ni mambo kadhaa yanayosabisha na kuchangia umasikini wa mtanzania mmoja mmoja na kuleta utofauti wa vipato.

Naomba tujadili.
 
Back
Top Bottom