Watanzania mna matatizo gani?

Watanzania mna matatizo gani?

hii tabia ni mbaya sana ya kurudishanA nyumA nakumbuka mzee wangu alinunua shamba njia ya kisini na kumyafuta kijana pale kijiji ambaye atakuwa anaangalia shamba na kusimamia na alimjengea kibanda pale shamba ili awe karibu .dah!mwisho wa cku jamaa katafuta mteja kauza na katokomea zake
 
We we acha izo......kama unaona wanakuibia....Fanya kazi mwenyewe au Fanya nao kazi.....alafu beba bastola.....nobody messes with a guy with the gun
 
Tena wanapoiba hawafikirii kuwa kale ka biashara mtaji uliupata bank na ile wanayoiba ndiyo faida, matoke yake biashara ikianguka yeye anakosa ajira na wewe unabaki na deni la bank.
 
We we acha izo......kama unaona wanakuibia....Fanya kazi mwenyewe au Fanya nao kazi.....alafu beba bastola.....nobody messes with a guy with the gun
Some people have itchy fingers mkuu kama ditopile, unaweza shoot mtu kisa amekanyaga ya la kuku wako kwa bahati mbaya [emoji23] [emoji23].
 
1. Unaanzisha mradi wako wa kuku au nguruwe shamba, kuna watu watakuja watavunja wataiba kuku au nguruwe wako.
2. Unamuajiri mfanyakazi akutunzie shamba huku unamlipa. Hafanyi kazi anazotakiwa kufanya na bado anataka kulipwa.
3. Unamuajiri mtu akusimamie kwenye biashara, anakosa uaminifu anakuibia.

N.k
Tatizo la watanzania ni wezi na wanakosa uaminifu. Wanataka wasimamiwe back to back. Wanataka walindwe usiku na mchana.
Huwa najiuliza hii ni tabia au ni dhiki? Inakuaje uajiriwe na unalipwa mshahara na bado unamibia muajiri wako? Kama mshahara ni mdogo si uache kazi ukatafute wanapolipa zaidi?
Mbona mnawakwaza wajasiriamali na wafanyabiashara? Kama huwezi kuwa muaminifu si uende kwa amani kuliko kuwa mwizi au kuchoresha ramani za wizi?
Mkuu inaonekana haya mambo yamekukuta nini ndio maana umeamua kutoa la moyoni.[emoji85] [emoji85]
 
Tatizo kubwa ni ukosefu wa ustaarabu kuna jamii zimestaarabika pamoja na kuwa maskini hakuna wizi wa kijinga kijinga nenda Zanzibar au tanga au kahama wizi wa kwa kijinga upo Kaskazini moshi Arusha wanajifanya wajanja kumbe hawana ustaarabu
Mkuu una point nzuri sana hapo uliposema; Tatizo ni ukosefu wa ustaarabu.
 
1. Unaanzisha mradi wako wa kuku au nguruwe shamba, kuna watu watakuja watavunja wataiba kuku au nguruwe wako.
2. Unamuajiri mfanyakazi akutunzie shamba huku unamlipa. Hafanyi kazi anazotakiwa kufanya na bado anataka kulipwa.
3. Unamuajiri mtu akusimamie kwenye biashara, anakosa uaminifu anakuibia.

N.k
Tatizo la watanzania ni wezi na wanakosa uaminifu. Wanataka wasimamiwe back to back. Wanataka walindwe usiku na mchana.
Huwa najiuliza hii ni tabia au ni dhiki? Inakuaje uajiriwe na unalipwa mshahara na bado unamibia muajiri wako? Kama mshahara ni mdogo si uache kazi ukatafute wanapolipa zaidi?
Mbona mnawakwaza wajasiriamali na wafanyabiashara? Kama huwezi kuwa muaminifu si uende kwa amani kuliko kuwa mwizi au kuchoresha ramani za wizi?

upo sahihi kabisa. Watu imefikia hatua kuanzisha mradi kinachoumiza kichwa ni msimamizi mzuri atampata wapi? hii imekuwa changamoto kubwa sana hapa kwetu. Faida mnagawana na msimamizi unaishia kufunga biashara, na huyo alie kuibia anaenda kuanzisha biashara yake akisahau kuwa alichokutendea, atatendewa nae pia vivyo hivyo huishia kufisirika.
Usimamizi wa miradi ni umiza kichwa, ukimwachia fundi ujenzi anaiba au anakuletea low quality materials, mafundi magari unaweza hata ukaleta oil usiposimamia anauza oil yote au anaongeza lita moja na kukubadilishia filter tu, wakati mwingine anakubambikizia vipuri vya gari vilivyo haribika ambavyo si vyako na anauza alivyotoa kwako ili ukanunue vingine..kero nyiingi kila kitu kinahitaji uangalizi wako wa karibu..aaaagh ni sheeeda!

Jamaa yangu alikuwa na taxi aliajiri driver na ile taxi alikuwa inalala kwa driver, makubaliano gari inafanya kazi usubuhi mpaka saa 2 usiku. W'end moja jamaa yangu akaniambia dereva wake kapata ajali usiku anajua yeye alikotoka sasa aliambiwa apeleke card halisia ya gari, ikabidi aende mwenyewe akasikilize maamuzi ya maafisa usalama, muda wote huo mimi nilikuwepo nikimzisindikiza jamaa yangu, nae yule driver alikuwa na jamaa yake nikajua kwakuwa mambo ya kipolisi anahitaji mtu kumsindikiza. Wakati sasa ndio tunataka kuingia kwa afisa usalama jamaa akaona anataka kuumbuka ikabidi aseme ukweli dereva hakuwa yeye ni huyo jamaa alikuwa nae tena ajali imetokea usiku wa manane. Hivyo mapato ya mchana anagawana na tajiri, na yeye kaajiri mtu usiku mapato yote yake..kaaazi kweli kweli. Niliinunua kesi hiyo..aligharamia kila kitu hadi kutengeneza gari na kibarua kikaishia hapo.
 
Rafiki yangu aliamua kuinvest kwenye kuku wa mayai, alikuwa na kiwanja ambacho alikizungushia fensi, akajenga mabanda matatu mle ndani na hutchery. Aliajiri mtu wa kusimamia na wengine wawili wa kuokota mayai na kuweka chakula na maji kwa kuku. Msimamizi alibomoja fensi akawa akitoka kwenye gate, anakwenda kuchukua mayai kwa nje na kwenda kuyauza. Wale waokota mayai ndiyo wanamstua kuwa kuna tundu kwenye fensi. Fikiria pesa aliyopoteza kuweka ulinzi wote huo.
 
Uvivu, wizi ni sifa za watanzania walio wengi. Management skills ni sifuri kabisa kuanzia serikalini hadi kwa watu binafsi. Muda hauna thamani kabisa kwetu.

Sisi kama wanugu ukitupa Kazi in a month tunakuja kazini labda siku14 siku zingine tunaumwa, tumeenda msibani, tumekosa usafiri na sababu zingine kede kede

Huwa nasema Kazi anayofanya mkenya mmoja inahitaji watanzania watatu au wazimbabwe saba (hawa ni wavivu mwisho). Ndiyo ukweli wenyewe samahani lakini
 
Ila ajabu zaidi ni pale mtu anakuja kukuvunjia kwenye biashara yako halafu anaiba.
Yani nashindwa kuelewa kabisa.
Inakufanya hadi unakuwa mtumwa wa mradi wako.
Huna amani kabisa.
Haya maswali hata mi najiuliza sana majibu, watanzania wengi hawaaminiki kabisa. Niliwah kufungua stationary pale Mabibo hostel, yule mfanyakazi aliniibia pesa nyingi sana akatoroka. Maan nilikuwa namwamini na mm nabanwa na shughuli nyingi namwachia mauzo hata ya mwezi mzima, siendi kuchukua, siku alivyonitendea siamini mpaka leo.
 
Uvivu, wizi ni sifa za watanzania walio wengi. Management skills ni sifuri kabisa kuanzia serikalini hadi kwa watu binafsi. Muda hauna thamani kabisa kwetu.

Sisi kama wanugu ukitupa Kazi in a month tunakuja kazini labda siku14 siku zingine tunaumwa, tumeenda msibani, tumekosa usafiri na sababu zingine kede kede

Huwa nasema Kazi anayofanya mkenya mmoja inahitaji watanzania watatu au wazimbabwe saba (hawa ni wavivu mwisho). Ndiyo ukweli wenyewe samahani lakini
Unaanza kazi wiki ya pili umefiwa na baba mkubwa, baada ya sikutatu jirani, baada ya mwezi binamu. Haya makampuni ya kigeni hayanunui hiyo biashara.
 
Tena wanapoiba hawafikirii kuwa kale ka biashara mtaji uliupata bank na ile wanayoiba ndiyo faida, matoke yake biashara ikianguka yeye anakosa ajira na wewe unabaki na deni la bank.

Haya mambo yanaudhi sana.
 
Mkuu inaonekana haya mambo yamekukuta nini ndio maana umeamua kutoa la moyoni.[emoji85] [emoji85]

Sio mara moja wala mbili.
Hebu fikiria una miradi mingi, unamuweka mtu 'in charge' wa kila mradi.
Halafu wanakuibia.
 
Haya maswali hata mi najiuliza sana majibu, watanzania wengi hawaaminiki kabisa. Niliwah kufungua stationary pale Mabibo hostel, yule mfanyakazi aliniibia pesa nyingi sana akatoroka. Maan nilikuwa namwamini na mm nabanwa na shughuli nyingi namwachia mauzo hata ya mwezi mzima, siendi kuchukua, siku alivyonitendea siamini mpaka leo.

Pole sana mama.
Halafu watu kama hao wakikosa ajira wanalialia kwa serikali.
 
Unaanza kazi wiki ya pili umefiwa na baba mkubwa, baada ya sikutatu jirani, baada ya mwezi binamu. Haya makampuni ya kigeni hayanunui hiyo biashara.

Dawa ni kulipana kwa siku.
Hapo atawaza akuibie ili afidie siku zilizobaki.
 
Back
Top Bottom