kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
WATANZANIA wapatao milioni 8.4 wanashinda na njaa au kulala njaa ili kukabiliana na ukali wa maisha, utafiti umeonyesha.
Kwa mujibu wa utafiti wa Synovate uliofanyika kati ya Septemba na Desemba 2009, wananchi wanaahirisha milo kwa sababu hali ya kiuchumi ya Watanzania milioni 20 imezidi kuwa mbaya.
Mbali na wale waliopunguza bajeti zao (asilimia 43), na wale walioamua kuacha kula baadhi ya milo kwa siku (asilimia 21), watu milioni 11.2 (wanaowakilishwa na asilimia 28 ya wahojiwa), walisema hawajachukua hatua zozote dhidi ya kuongezeka huko kwa gharama za chakula wakati watu milioni 1.6 (asilimia 4) walisema wamekopa kutoka kwenye benki za biashara na hawajui jinsi ya kurejesha mikopo hiyo