Watanzania milioni 8 washinda njaa kila siku

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
WATANZANIA wapatao milioni 8.4 wanashinda na njaa au kulala njaa ili kukabiliana na ukali wa maisha, utafiti umeonyesha.
Kwa mujibu wa utafiti wa Synovate uliofanyika kati ya Septemba na Desemba 2009, wananchi wanaahirisha milo kwa sababu hali ya kiuchumi ya Watanzania milioni 20 imezidi kuwa mbaya.
Mbali na wale waliopunguza bajeti zao (asilimia 43), na wale walioamua kuacha kula baadhi ya milo kwa siku (asilimia 21), watu milioni 11.2 (wanaowakilishwa na asilimia 28 ya wahojiwa), walisema hawajachukua hatua zozote dhidi ya kuongezeka huko kwa gharama za chakula wakati watu milioni 1.6 (asilimia 4) walisema wamekopa kutoka kwenye benki za biashara na hawajui jinsi ya kurejesha mikopo hiyo
 
Ni kweli hata wale wanaochukua chips vibandani kwa ajiri ya watoto wao na wao wanajiita wamekula?
 
Tulivyokua UD tulikua tunaiita 'technical dash'..

Lakini swali la kujiuliza ni ..

Kipi kipya hapa??
 
Au uswazi kuna ile inaitwa "Pasi ndefu",unapiga ugali wako na samaki wa kukaanga asubuhi,then unasikilizia night.Bongo bana
 
hahaha kuna jamaa yangu namsikia anasema kazini kwao kuna chama kinaitwa CHAWASHINTA eti Chama cha Washinda Njaa Tanzania. eti wao kazini hawapigi msosi kabisaaaaaaaa
 
Miaka Minne ilopita waliahidiwa kushibishwa kwa kuletewa maisha bora. waliowaahidi hawakurudi kuwajulia hali. Waliowaahidi wameshiba na hawakumbuki kuna watu hawana chakula. Waloshiba wanajiandaa kuchukua usukani, tena si lazima warudi kuwapigia magoti wenye njaa bali wanaweza tu kufanya ujanja ujanya wa kuunda makundi ya kuwapitisha, ili waendelee kula wao. Iko siku watavuna wanachokipanda!
 
hahaha kuna jamaa yangu namsikia anasema kazini kwao kuna chama kinaitwa CHAWASHINTA eti Chama cha Washinda Njaa Tanzania. eti wao kazini hawapigi msosi kabisaaaaaaaa

Ofisi nyingine ni balaa bwana. Ukitoka tu na bosi anakuita kukupa kazi utadhani anaka-CCTV flna ofisini kwako, ukirudi tu unakuta secretary anakuita bosi alikuwa anakutafuta, sasa inabidi mjanja kwelikweli. Wengine ilibidi tuwe tunaisogeza ile chai ya kizushi ya ofisini mpaka kwene mida ya saa 5 au 6 hivi ili kupalilia mazingira ya kutokula mchana na kusev vijisenti kwa ajili ya ada ya watoto. Bongo bana..ni u-sterling tu kila mahali, bila hivo imekula kwako.
 
[h=2]Pres. Kikwete's "Maisha bora kwa kila Mtanzania"[/h]



Reflecting on President Kikwete's promise – maisha bora kwa kila Mtanzania or a better life for every Tanzanian, see the photos and your comments are welcomed!
01.jpg

Five years already and it doesn't appear to have brought any difference to the lives of these two boys, whom I spotted following proceedings to mark the Day of the African Child at Chanzulu village

02.jpg

03.jpg

The two photos above show an old woman called Loi, in front of and in her house in Ibwaga Village. She has lost her sight with age, and lives with her daughter who is deaf. They normally depend on farming for their livelihood but last year their farm was among many others that were destroyed by the December floods in Kongwa District. At the time photograph was taken they had stock of only ten kilos of "uwere" left.

04.jpg

05.jpg

Above, Ekilia Ngonyani, 46 is a single mother raising five children alone. She is also suffering from an unestablished condition that has caused her stomach to swell up and has been for the past 16 years. She cannot afford to go to a 'big hospital' as advised by the doctor in her village. For a living she walks 14 kilometres thrice a week to buy vegetables in a village called Tubugwe and only gets Sh2000 in profit for her trouble.

06.jpg

Theresa with her four grandchildren, having lunch of boiled 'uwere,' the family can only afford to eat two meals a day.

07.jpg

A young boy Village walks more than 20 kilometres in one week to collect firewood.



MAISHA BORA KWA KILA MDA-NGANYIKA.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom