Watanzania Milioni 7 Hawana Vyoo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania Milioni 7 Hawana Vyoo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by hekimatele, Oct 11, 2012.

 1. hekimatele

  hekimatele JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 9,489
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Watanzania milioni 7 hawana vyoo
  Watanzania milioni 6.5 wanalazimika kujisaidia ovyo porini kutokana na kutokuwa na vyoo.
  Afisa mkuu kitengo cha Afya na Usafi wa Mazingira katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Khalid Massa aliyasema hayo jana wakati wa semina kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhudumia Watoto (Unicef)
  Asilimia 10 ya Watanzania ndiyo wenye vyoo huku asilimia 90 wakiwa hawana vyoo bora hali ambayo huwalazimu kujisaidia porini na kusaabisha kutokea kwa magonjwa ya mlipuko.
  Takwimu nyingine zinaonyesha kuwa choo kimoja hutumiwa na wastani wa wanafunzi 250 hado 600.
  Asilimia 38 ya shule hazina maji ya kunywa na silimia 84 hazina vifaa vya kunawia mikono> Tatizo hili limeitia gharama serikali ya Shilingi bilioni 3 kutibu watu wanaokumbwa na magonjwa ya maambukizi.
  Source: Nipashe la leo Alhamisi Oktoba 11, 2012

  Tafakari:
  Hizo Bilioni 3 ambazo serikali inazitumia kutibu maradhi zingewekwa katika ujenzi wa hii miundo mbinu ya vyoo na maji safi si ingepunguza sana gharama za kutibu maambukizi.
  Ni bora kinga kuliko tiba au bora tiba kuliko kinga?
  Ufisadi unali cost sana hili taifa. Mi na wewe tunaweza kusimamisha ufisadi huu wa nchi.
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hayo ndio maisha bora kwa kila mtanzania! Tunatumia gharama kubwa kutibu magonjwa ya milipuko!
   
Loading...