"Watanzania milioni 39 wanakunywa mataputapu"

Waache use nge huo utafiti wameufanyia wapi na imechukua muda gani kutafiti au ndio mwendo wa kukurupuka kutafuta kick
 
Sio mataputapu ni pombe za asili, waache dharau.

Na asilimia kubwa ya wanywaji wa bia ndio hao hao wanywaji wa pombe za asili.
 
Watu wazima ni kama milioni 20 tu na watoto idadi nyingine inayobaki ni watoto ukisema 87% ya watanzania wanakunywa mataputapu maanake mpaka watoto wadogo wanakunywa hayo mataputapu.
Kumbe hata huko juu kuna villaza hivyo.
 
Sio mataputapu ni pombe za asili, waache dharau.

Na asilimia kubwa ya wanywaji wa bia ndio hao hao wanywaji wa pombe za asili.
Tazama hivi. kuwe na viwango, zisindikwe vizuri kiasili, tuache kuziitaajina mabaya lkama mataputapu, tuziite majina yake matamu kama komoni, kangala mbege lubisi nk nadhani zisingeitaji afisa masoko hizi wala promo wanataka kusifia zao hao hawana lolote kweni hata hizo zao zinaadhara ndio maana zina maonyo ya umri wa mtiaji +18, kunywa kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.
 
Nadhani alimaanisha kuwa 87% ya wanaokunywa pombe wanakunywa mataputapu,ina maana asilimia 13 tu ndio wanakunywa pombe za viwandani.
Hii ndio labda naweza kuiamini lakini kwamba eti hiyo asilimia kwa watanzania wote basi na watoto ndani ( japo kwa wataniwangu wa a=kabila Fulani wanawapa watoto wanachapa usingizi wao wanaendelea na kazi. Pamoja na hayo angalau takwimu uliyoileta angalau inaweza kuamninika.
 
Ni dharau na ukosefu mkubwa wa adabu na heshima kuziita pombe za kienyeji matapu tapu. Kila pombe inathamani yake kwa mnywaji na kila mtu anafurahia kinywaji chake kulingana na mazingira, asili, uwezo na upatikanaji wake kirahisi. Hizi ni pombe zinazotengenezwa nje ya viwanda vya kisasa na hazina makemikozi kama hizi za viwandani. Hata nyakati za mitume (sio hawa wa sasa) walikuwa na pombe zao za asili. Acheni kudharau vinywaji vya asili jamani kwa kuviita majina mabaya.
 
Ni moja ya tafiti za aina ya "Twaweza zaa". Na mwisho wa siku hata vile vyakula vyetu vya asili kama ugali na makande vitaitwa mataputapu au "matopetupu"
 
Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni, Milioni 39.06 kati ya Milioni 44.9 ya watanzania wanakunywa pombe!??. Mbona idadi inatisha mno?
Ni utafiti wa hovyo kuwahi kutokea duniani...yaani watanzania mil 5.3 ndo ndani yake wapo wanywa pombe safi, wasiokunywa kbs na watoto wadogo!nina mashaka na watafiti na uwezo wao wa kutumia asilimia....!
 
ImageUploadedByJamiiForums1467033305.491041.jpg

Utafiti uliofanywa na shirika la Afya Dunia ‘WHO’ umeonesha kuwa 87% ya watanzania wanakunywa pombe za kienyeji, huku mikoa ya Dar es salaam na Kilimanjaro ikiiongoza kwa kuwa na wanywaji wengi wa pombe hiyo.

Mkoani Kilimanjaro eneo linaloongoza kwa wanywaji wa pombe hiyo ni Moshi, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Tanzania ilikuwa na watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 44.9, hivyo 87% ya idadi hiyo kulingana na utafiti huo ni watu milioni 39.06.

Kulingana na gazeti la Jambo Leo limeeleza kuwa utafiti huo umebaini kuwa kwa sasa vijana wengi wanatumia pombe kupita kiasi kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu hali inayosababisha wakumbwe na magonjwa ya akili na kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu.

Matokeo ya utafiti huo yalitangazwa jana katibu mkuu wa chama cha wataalam wa afya ya akili Tanzania (MEHATA), Dk. Kissah Mwambene. Alikuwa akitoa mada kwa wabunge juu ya athari za matumizi za matumizi ya pombe iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawwake ‘TAMWA’.
 
Back
Top Bottom