mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,252
Nimesoma hoja ndani ya Jamii Forum iliyohitimishwa Kwa kusema waogope watanzania.Nimekubaliana Na hoja hiyo kutoka Na ushahidi nilionao Juu ya ya Unafiki wa watanzania tulio wengi.Kwa mfano tulimpenda sana Rais mstaafu wa awamu ya 4 Mh.Kikwete mpaka tukamwita Chaguo la Mungu lakini Leo hii watanzania wale wale wanambeza.Yupo kiongozi wa serikali alikuwa Waziri awamu ya 4 Leo anasimama bila aibu anaibeza ile serikali Na kwanini hakujitoa kwenye ile serikali?Mtanzania utamsikia anajifanya ana uchungu Na wananchi Leo ukimpa cheo anawageuka wananchi.Yupo kiongozi alikuwa anapinga muundo wa serikali mbili mpaka mapovu yanamtoka Leo kapewa ukuu wa wilaya anaushabikia muundo wa serikali mbili.Viongozi wetu Na wananchi Kwa ujumla wao no wanafiki sana wakipata madaraka utauona unafiki wao .Unafiki wa watanzania ni wakuuogopa kama ukoma .Lowassa wakati anatafuta wadhamini ndani ya CCM viongozi walimwunga mkono Na wala hakuitwa Fisadi lakini alipohamia Ukawa viongozi hao wakamwita Fisadi huo ndio UNAFIKI wa viongozi wa Tanzania.Kidumu chama cha Mapinduzi.