Watanzania hodari kwa mitumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania hodari kwa mitumba

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by WATANABE, Feb 13, 2012.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  [h=1]Deacons to close shop in Tanzania over endless losses[/h]

  [​IMG]
  Deacons will close three stores in Tanzania: Truworths, Identity and 4u2. Picture: Phoebe Okall By EMMANUEL WERE (email the author)

  Posted Saturday, February 11 2012 at 15:19

  Deacons, the clothing and lifestyle goods retailer, will close its Tanzanian operations in the next two weeks shielding it from continued losses in that market.  The fact that Deacons has found the going to be tough in Dar es Salaam highlights the challenges of doing business in Tanzania, which is ranked fourth out of the five member states in terms of the ease of doing business in the East African Community, according to the International Finance Corporation’s Ease of Doing Business report 2011.

  The firm’s board decided to exit the country after its subsidiary, Tanzanian Fashion Stores, lost Ksh13 million ($154,394) in the full year ended December 2011, marking a fifth straight year of losses despite efforts to turn it around.

  Deacons will close three stores in Tanzania: Truworths, Identity and 4u2 branded stores, and in the process shed 15 jobs.

  The high cost of doing business in Tanzania, especially the high rental charges where a square foot of office space costs almost double what the prices in Kenya, Uganda and Rwanda, and that their target market, the upper to middle income — is very small compared with operations in other countries, led to the decision, the company said.

  The cost of rental space in Tanzania is $40 dollars compared with $18 dollars per square foot in the rest of the region.


  Tanzania’s middle class make up just 12 per cent of the total population, which is far much smaller compared with Kenya’s 44.9 per cent and Uganda’s 18.7 per cent of the population. Rwanda’s middle class is at 7 per cent its population.“The cost of doing business in Tanzania is 30 to 40 per cent higher compared with other markets. The middle class is also not as big and the uptake of our brands was also not as big,” said Deacons chief executive Muchiri Wahome.

  Dar es Salaam, Tanzania’s Capital, only boasts of two shopping malls. In contrast, Nairobi, Uganda and Rwanda are experiencing a boom in the construction of malls and hence rapid growth of the shopping mall concept.

  Also, long supply chain in Dar es Salaam is a challenge, where it can take up to five times longer by air to clear and deliver goods compared with the rest of the region.

  The firm will be looking to have a fire sale before it shuts shop by the end of February. However, the company will have to write off Ksh20 million ($237,500) in assets and inventories.

  Although Deacons Tanzanian operations have been loss making, it expects to make profits from its operations in Kenya and Uganda boosting its overall profitability. Rwanda, where the retailer opened two stores in December has been a good market

  In the six months to June 2011, Deacons’ sales grew by 38 per cent to $11.7 million compared with the same period last year. Profits after tax grew 51 per cent to $507,700 compared with the previous year.

  The company said operations in Uganda were doing well with a 44 per cent growth in revenues contributing 7 per cent of the total group revenue for the 2011 financial year. Swedfund International is the main shareholder in Deacons, which is publicly traded firm, with a 19.45 per cent stake.

  Pinpoint investment Ltd (12.06 per cent), Charles Mwangi Gathuri (11.04 per cent) and Diana Bird (11.03 per cent) are the other main shareholders of the publicly traded firm, which hopes to list its shares on the Nairobi Securities Exchange later this year.

   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Yaani mitumba ndio symbol ya kuingia kwetu kwenye utandawazi na kumetugharimu sana maana viwanda vyote vya nguo vimekufa bila sababu ya kueleweka. Hivi tunajua kwamba Lethoto inauza nguo nyingi sana nje kuliko Tanzania? Tunalima pamba na tuna viwanda vingi vya nguo. Badala ya kuendesha textile industry kutoka kwenye kulima, mpaka kutengeneza na kuuza nguo, sasa hivi biasharta njema ni kufuata nguo China na far east. Wachina wamegeuza Urafiki sijui godown au sehemu za kulala wakitoka kufanya uchuuzi Kariakoo. Mwatex, na kwingineko kumesambaratika jumla. What a good country!
   
 3. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  Hii ndio sababu wawekezaji wanaokuja hapa wanajisubject kama risk takers kama kwenda Afghanistani, Kongo, Irak na labda Somalia. Matokeo yake wawekezaji wazuri hapa ni dizaini ya DOWANS na MEREMETA. Hatupati wawekezaji walio serious sana on long term basis na sio ajabu hata makampuni ya madini yanatoa kidogo as they are not certain with the future.

  Suala la rent, mwekezaji mmoja alikuwa tayari amesign mkataba na Mlimani city Mall lakini alivyoangalia uhalisia wa vitu alivyotaka kuuza akaamua kuachia mwenyewe maana aliona wazi kwa gharama ile biashara isingewezekana kutengeneza faida katika mazigira ya ukweli.

  Alafu kitu ambacho sikujua ni kuwa kwa Tz middle class income ni 12%, hii ina maana high income (naomba kukosolewa) ni kama >2% ya Watz. Kwa maana hiyo lower income (wanaoishi >$1 per day) ni zaidi ya 85%! ambapo kwa Kenya nadhani inaweza kuwa >30%. Hapo ndio ujue kuwa sisi ni fukara kiasi gani pamoja na rasilimali tulizojaliwa. Ndio sababu concept ta 'supermarkets' inakuwa ngumu kwa mswahili wa kawaida huku tukiendelea kuamini kuwa ni ya 'wazungu'!

  Kwenye supply chain hapo kila kitu ni nani anamjua nani na kwa walivyoandika kuwa kama unaweza kufanya clearance ya mzigo bandarini/airport kwa siku moja Kenya/Uganda, Tz ni siku tano na kana ratio itakuwa siku 3 basi hapa ndio siku 15! Hapa kuna 'wazee' TRA, utadhani hawa 'matajiri' wa nchi hii hawaishi hapa kwa jinsi wanavyorelax wakati mizigo ya wafanya biashara ikiongeza demmurage na storage charges!

  Kwa hakika mfumo wetu ni mbaya sana na wote tunajua lakini wanaofaidika nao ni wale walioko kwenye sysytem. Matokeo ndo kama haya, wawekezaji ambao tunatumia gharama kuwaita wanaondoka!

   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Inaboa kuisomaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Feb 13, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280

  mkuu ni kweli kabisa, hii nchi ni ya kipekee kabisa, mitumba inaathili sana viwanda vya nguo tanzania ingawa watanzania wengi wanaona mitumba ndo ishu but madhara yake kwenye uchumi ni makubwa sana,

  vilivyo kuwa viwanda vya nguo kwa sasa vimegeuzwa magodown na hata mashine zilisha ng'olewa na kuuzwa kama vyuma chakavu na hii ni kutokana na walioziwa kushindwa kushindana na mitumba kutoka ulaya.
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Feb 13, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280

  True kabisa ghalama za kufanya biashara Tanzania ziko juu sana na wawekezaji wengi wamekuwa wakikimbilia kenya na hata Uganda kwa sababu huko ni nafuu kidogo.

  Rent tanzania ni tatizo kubwa sana kila mtu anajiamulia bei ya kukodisha nyumba, na huu utaratibu wa kulipia mwaka mzima uko Tanzania pekee hakuna nchi nyingine yenye huu mfumo wa ajabu na wa kishenzi sana wa kulipia pango kwa mwaka mzima badala ya mwezi mmoja mmoja, cha kusikitisha zaidi Serikali iko kimya na huu mfumo wa ajabu na wakulilizwa wana sema soko huria, nchi kama marekani ndo viongozi wa free market lakini kuna mahali hufika serikali huingilia kati ili kuweka mambo sawa,

  Tukiendelea na huu utaratibu wa ajabu sana wa kulipia kwa mwaka tutajikuta hatuna wawekezaji kabisa, na watu wengi sana wanashindwa kufanya biashara kwa sababu ya rent kuwa juu sana na ya kulipia kwa mwaka mzima
  ,
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 8. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mkuu, pamoja na tatizo la rent, suala la serikali kubuni sera za kupanua hii middle class ni la muhimu sana.

  Serikali ya sasa hivi iko busy kutengeneza 'artificial millionaires' ambao issue kubwa kwao ni money laundering. Haya mambo ku-animate jamii ni jukumu la serikali badala ya kujidanganya kuwa yanaweza kuja automatically! Ukijenga capacity ya wananchi matokeo yake ni mazuri kwa taifa badala ya kudhani kuwa kuziwezesha familia chache ndio ujanja kumbe ni kupalilia matatizo muda mfupi ujao.

   
 9. K

  KVM JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Swala la supermarkets Tanznaia ni geni sana kwa watu wengi labda wale wa zamani walioziona COASATA na STC (Saidia Tujenge Chetu) na ambao wametembea sana nje ya nchi. Baada ya COSATA kutaifishwa na kufanywa STC, STC ilikufa na badala yake yakatokea maduka ya kila nyumba. Ndiyo maana Tanzania kumejaa "mafremu" kila mahali, mpaka Osterbay na Masaki. Watanzania hata wale wenye kipato cha kati (Middle Income) hawana utamaduni wa kununua kwenye "supermarkets". Aliyeandika kuwa sababu ya watu kutonunua "supermarket" ni "low percentage" ya "middle income group" anaweza kuwa hajalifahamu tatizo vizuri. Botswana ina watu millioni mbili lakini karibu kila mtu anaishi kwa kwenda "supermarket" ambako unanunua hadi mchicha. Hata viduka vya mitaani vinapata bidhaa zao supermarket. Ndiyo maana ukiwa Botswana ni nafuu kununua "supermarket" kuliko mtaaani. Kwa Tanzania, kwa ujumla, ni kinyume.

  Kama middle income ya Tanzania ni 12% hiyo ni sawa na kusema watu karibu millioni tano. Kama ni 5% ni sawa na watu millioni 2, yaani idadi ya watu wote wa Botswana. Kama watu wote wangenunua supermarket basi supermarket zingestawi kuliko Botswana ambako kumejaa "Shopping Malls, supermarkets and hypermarkets".

  Kilichoua viwanda vyetu vya nguo ilikuwa ni siasa mbaya - Ujamaa, siyo liberalization. Kwa wenye kumbukumbu nadhani wanakumbuka kuwa alikuwa ni Salim Ahmed Salim wakati alipotembelea Mtwara aliruhusu mitumba iletwe Tanzania baada ya kuona watu wakitembea bila nguo. Tukumbuke tena kuwa kuna wakati watanzania walikuwa na shida sana ya nguo na wengine walitembea uchi! Sipendi kuzikumbuka siku zile kwani huko vijijini watu khanga na kitenge zilikuwa ni "tie-and-die" tu na sisi wa mjini tulikuwa tunavaa tacron za Msumbiji. Chupi zilipotea kabisa. Watu tayari walikuwa wameshaanza kuiba mitambo ya viwanda kama Kilimannjaro Textile na Sunguratex.

  Serikali ya leo ina wajibu wa kutunza viwanda vyetu vya nguo, vya serikali na vya watu bianfsi. Kuna wengi wanataka Mwatex na Urafiki vifanye vizuri. Ukweli ni kuwa viwanda licha ya kutomudu ushindani wa bidhaa kutoka nje vinashindwa kupambana na viwanda vya binafsi vilivyopo Tanzania. Kiwanda cha Urafiki ikiwezekana kiuuzwe tu - lakini mafisadi watapeana wao kwa wao, bureeeeee!

  Mpaka leo sielewi ni kwa nini watanzania wanashindwa kutumia cherehani kushona nguo na kuilazimu nchi kuagiza bidhaa hizo nje hata kama ni sare za shule.
   
 10. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  umeongea vizuri mkuu na hapo kwenye red umemaliza kila kitu hasa underline!

  Ukweli unabaki pale kuwa kama kunakuwa na outlet kama supermarket inasaidia serikali hata kupunguza gharama katika upangaji wa mipango na kukusanya kodi. Lakini hayo yote yanafanikiwa endapo kila anayefanya hivyo ana nia ya kweli kufanya hivyo, tatizo ni hapo kwenye red/underline
   
 11. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #11
  Feb 13, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu hata kiwanda cha urafiki kikiuzwa kwa haki je kitaweza ushindani? Viwanda vingi vya nguo baada ya kufufuliwa/kubansifishwa vilianza angalau kutengeneza mashuka na vitambaa mbalimbali, ila hata mashuka kwa sasa hawatengenezi tena kutokana na kuwepo mashuka mengi sana ya mitumba,

  Kinacho takiwa hapa ni sera na ili kulinda viwanda vya nguo ni lazima serikali ije na mikakati ya uhakika kuhusu mitumba na ikibidi waweka hata import quota ya mitumba kutoka nje, kwa sasa hakuna mwekezaji atakaye kuja tanzania na kuwekeza kwenye viwanda vya nguo, wanafahamu fika kabisa hawataweza ushindani wa second hand kutoka Ulaya,

  Hili swala la supermarket ni kweli kabisa ni vitu vigeni sana Tanzania na kuna factor nyingi sana kwa nini supermarket hazifanyi vizuri Tanzania kama Kenya na nchi zingine.

  Na hata viwanda vya ndani vinavyo fanya vizuri kama A to Z Arusha ni kwa sababu ta tenda ya Net za bushi na ukiangalia mwenzake Sunflag amabae mwanzoni walikuwa sawa kwa sasa yuko huoi sana na amebakia kutengeneza shuka za kimasai tu, ingawa bado nako ni tatizo

  Moja ya sababu ni kwamba,

  1. Yale maduka watanzania wengi wanaya chukulia kama ni sehemu ya anasa

  2. Haya maduka ni kwa ajili ya wazungu na watanzania wachache wenye pesa

  3. Watanzania wengi vijijini na hata mijini wana mudu kulima na kuzazlisha mazao ya chakula kama mahindi, mchele. kufuga kuku wa kula, na kazalika na haya maduka mkubwa ununuzi mkubwa uko kwenye chakula na watanzani wengi wana magunia ya mahindi na mipunga ndani so hawaoni umuhimu wa kwenda kununua unga wa superparket wakati wana mahindi ndani.   
 12. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wafunge tu, makumbusho mitumbani kama kawa.
   
 13. K

  KVM JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Mimi nakubaliana nawe kabisa kuwa serikali inabidi ianze kutazama upya swala la mitumba. Hapo zamani siyo kwamba mitumba haikuwepo. Mitumba ilikuwepo na ilikuwa inaitwa "Kafa Ulaya". Ilikuwa ni nguo inayovaliwa na wazee sana au na watu wenye shida sana kama misaada kupitia makanisani zaidi. Hii ilikuwa hadi vijijini (isipokuwa yale makoti makubwa sana kwenye sehemu za baridi). Ilikuwa ni aibu kuvaa kafa ulaya. Nadhani na serikali nayo ilikuwa inawafanya watu wajisikie hawapo sawa kama wakivaa nguo za watu waliokufa ulaya. Tulijivunia Utanzania. Bahati mbaya leo watu hawajivunii Utanzania tena. Wengine nadhani wanajisikia vibaya hata kuitwa ni Watanzania.

  Kwenye swala la watu kutojivunia Utanzania serikali pia inabidi ilaumiwe. Inaelekea haioni kuwa hilo ni tatizo na wanazidi kuliendeleza kwa njia nyingi. Tanzania siyo nchi mbaya kama watu wanavyotaka tukubali. Lakini serikali inaposhindwa hata kuchapisha au kushona kipande cha bendera ya Taifa na kugawa kwa wananchi wazipepee mtaani ili kuadhimisha miaka 50 ya uhuru ina maana gani? Mimi sikuona bendera zozote za Taifa zikipepea mitaani hapa DSM. Gharama za kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru zilienda wapi?
   
Loading...