Watanzania hii ni kweli?

Ngo

JF-Expert Member
May 25, 2010
284
51
:welcome:
Katika pita pita zangu kwenye post za website mbali mbali, nikakutana na watu wengi wameunga mkono post ya jamaa mmoja inayosema ''Unauliza tena watanzania kwa ngono na pombe naona kama ndio nusu ya maisha yao ,ukipasua kichwa cha mtanzania utaona ngono,pombe,wizi,zulma na kukabana'' Kuna ukweli wowote kuhusu hii post ya mchangia mada kuhusu maisha ya watanzania waliyo wengi?. Nikaanza kutafakari kwa mda, nikaona kw kiasi fulani huyu jamaa ana ukweli ndani yake maana kwa maisha ya leo watu wengi wawe wameowa au kuolewa, Kwenda nje ya ndowa ni jambo la kawaida, Vimada/nyumba ndogo usiseme.Kunywa pombe zilizopitiliza hiyo usisema hata kama vipato haviruhusu mtu anaweza kukalisha creti kadhaa na kutoa round nyingi kwa marafiki wakati familia nyumbani ina mambo mengi haijatimiziwa.Tofauti na Wenzetu wa nchi zilizoendelea budgeting ni muhimu zaidi, wanatafuta vipato kwa ajiri ya savingi/Investment kwa maisha ya kesho.Tunalia vipato vidogo na maisha ni magumu lakini Ikifika kwa hizo starehe pesa zinapatikana.
 
Back
Top Bottom