Watanzania, hatumjui Paul Makonda?!

Watanzania, hatumjui Paul Makonda?!

Kweli kabisa..Hata wauza chips huku newala wanamzungumzia Rc dar sijui anawasaidiaje..Tufanye yetu tumechoka na hizi story
 
c3ac8c93e455358cf96dc574a61d5cb6.jpg
 
Kuna watu hawamjui mwenyekiti wa mtaa, mtendaji wa kijiji & kata, mwenyekiti wa kijiji, Mkuu wa Wilaya, Mbunge na Mkuu wa Mkoa kwenye eneo analotoka lakini wanamfuatilia Bashite Daudi na Dsm yake. Huku ni kuwa kiherehere.

Kila siku Makonda, kila siku vyeti...tunaacha kazi zinazotuhusu,tunaamka, tinashinda na kulala na mijadala ya Makonda. Akionesha cheti wewe utapata nini? Utaingiza pesa?Utapata ajira?

Ni nn kiuchumi utakipata kwa kumjadili Makonda?

Mtu yupo Urambo, Ngudu, Naliendeli, Chato, Songea,kumasi, Mbwewe, Mkinga, Mboro nk anakomaa na Makonda.Tuiache Dsm na wenyewe.

Ukaguzi wa vyeti ni swala la Kitaifa.. wamefukuzwa watu kazi nchi nzima... kwa hiyo issue ya Bashite ni ya kitaifa...najua inawauma...
 
ukweli toka hii issue ianze kutokea na mazingira ya Kada Makonda kutoka huko,CCM kindaki NDAKI Mara mkuu wa Wilaya Mara mkuu wa mkoa na Tamko LA Mkuu pale ubungo Naanza kuogopa Makonda hana IQ ndogo kama tunavyomfikiria nadhani Makonda ni zaidi ya tunayemjua Kwenye Swala LA Elimu yake ndo kuna wasi wasi sana coz kila nikijiuliza sababu za msingi zilizokuwa zinamfanya Asome chuo na kufika mahali anaacha na kurudi tena anasoma kwa muda tena anapotea na kurudi tena chuo, Huenda siyo kufeli ni mpango maalumu napenda sana kujipa muda na kuwa na subra muda utaamua
Una maana Mr zero ni shushushu? wakati hata kujua kama jengo lina camera ameshindwa kama usalama ndo wako hv mmmh twafwa
 
Kweli asee waachieni wa Dsm sisi tu deal na Hawa wauza ngada mpaka wakimbie jiji.. Nusu Tupo upande wa makonda nusu wapo upande wa Gwajima na clouds.. Sasa nyie wengine wa mikoani kuweni neutral tu. Ila ungeni vita ya madawa ambayo tayari serikali itashinda
 
Do you remember the statement which state that, the problem can not be solved by the people who are the same level of thinking? This was what we happened in our country, my question is, whom one will be responsible to rescue the situation which we have in our Nation (Tanzania)?
It begins wit u
 
Well said but still dosn't change MIND of the great thinkers

NB: It possible to happen the same scenario in American Movies but not in TZ
 
WEWE ULIYELETA MADA NI MPUMBAVU WA KUTUPWA. Bashite angekua mtu wa medani angemkamata Ngwajima au Mbowe live wakiwa na madawa ya kulevya.
USITULETEE HADHITHI ZA KINA WILLY GAMBA
Tunga kitabu cha hadithi uuze, tena utapata hela nyingi sana.
 
Mkuu maelezo yote haya unayatengeneza ili umtetee daudi bashiite,sikubali niitwe ndumilakuwiri kamweeeee tunataka vyeti mezani
 
umetumia ID hii kujipongeza? na zile nyingine 8? yaani we jamaa unafurahisha. unatoa mawazo halafu una log off na ku log in kwa account nyingine kujipongeza kuwa una akili sana. nazijua account zako nyingine ngoja ntakutajia tu kila utakapotumia.

Yaani narudia kukupongeza, nimepitia tena mada na hoja mbalimbali za watu wengi, hakika wewe umeongea kitu sahihi na cha weledi wa juu sana. Kila mada na hoja nazopitia ni nyepesi na za kijinga . Yaani zinaanzishwa na watu wasio na weledi wowote na zinachangiwa kizumbukuku. Wewe ni The Genuine Great Thinker.
 
Naona wewe una mwili mkubwa halafu kichwa kidogo...yaani usanii unataka kuufanya sayansi...yaani umeongea km vile huyo makonda ametoka iceland ambako wanadar wachache wamefika... kumbe kazaliwa hapahapa bongo na kusoma juzijuzi tu wakati ambapo hata simu za mikononi watu hawazishangai tena.
 
Wewe huwezi kumuelewa kabisa kwanza hata vitabu alivyovitaja mwenzio kwako ni "usumbufu". Unayoyasoma wewe ni " karatasi za kuchambia"
Asha jazz serveur tayari ya jf

Ova
 
Mwanduhitinje! Usidanganye watu , huko meatu simiyu hicho kijiji hakipo! Naitambua "Mwanduitinje" , kwa ulivyondanganya nafisi ni kuwa wewe mchambuzi. Wew ni mpiga debe tu , akisoma post yako mh Mbunge Luhaga Mpina "naibu waziri wa muungano&mazingira" stakushangaa. Huna logic
 
Kuanzia Sakata la kutaja Watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya mpaka kinachodaiwa "Uvamizi wa kituo cha Clouds Media Gruoup"! RC Paul Makonda amekuwa gumzo kuu hapa Nchini kwa sasa ,kuanzia kwenye vyombo vya habari,mitaani na kwingineko!

Nikiwa hapa Kijijini kwangu Mwanduhitinje nimekuwa nikilifuatilia suala hili kwa taratibu sana bila mihemuko ili nijifunze kitu kipya na kwa kweli nimejifunza sana!

Kabla sijasema mafunzo niliyopata kutokana na "Sakata" hili niwaeleze kuwa nimesikiliza Clips zote za "Askofu" Gwajima kuhusu RC Paul Makonda,Nimesoma magezeti yote yaliyo na yanayoandika habari kuhusu RC Paul Makonda,Nimefuatilia post zote za Mange Kimambi kuhusu RC Paul Makonda,nimefuatilia comments za Watu mbalimbali kuanzia RC Paul Makonda akichipukia UVCCM akitokea TAHLISO kama Rais wake na hata alipom-blast Lowassa kuwa hana sifa za kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM, na sasa naeleza mafunzo niliyopata na hasa baada ya kusoma Gazeti la JAMUHURI kwa kile walichokiita Uchunguzi uliofanywa na WAANDISHI WETU!

FUNZO LA KWANZA: Tanzania ni miongoni mwa Nchi Duniani zenye uhaba wa Waandishi wa habari na Wasomi (Ninaposema wasomi simaanishi wale wenye "A" zote na Makofia mengi lakini wameishia kufuga kuku na Nguruwe kule CHANGANYIKENI).

FUNZO LA PILI: Watanzania wengi ni watu wasio na agenda yoyote ya maana ya ku-accomplish katika maisha yao bali ni watu waliokata tamaa na wanaotumia MATUKIO kama "pain killers" ya kuwapunguzia maumivu kutokana na KUSHINDWA kwao.Ndio maana Watanzania wengi hushabikia sana habari zinazomdhalilisha mtu au kumshusha chini mtu aliyeko juu kama RC Paul Makonda.

FUNZO LA TATU: Watanzania hatuna wanasiasa wenye maono,wanasiasa wetu wengi ni waganga njaa tu ambao wamefanya siasa kama kichaka tu kujifichia na kutafuta riziki kwa ajili ya maisha yao na siyo maendeleo ya wapiga kura na Taifa kwa ujumla!

FUNZO LA NNE: Tanzania hakuna UPINZANI,na itachukua miongo mingi sana Nchi hii kuweza kuongozwa na Chama cha Upinzani.Hawana Ajenda na ni watu wa MIHEMUKO! Ajenda zao ni kama hizi WEMA SEPETU KUPOKELEWA CHADEMA,TUNDU LISSU KUWA RAIS WA TLS, RC PAUL MAKONDA KAVAMIA KITUO CHA CLOUDS MEDIA GROUP.

FUNZO LA TANO: Wapinzani wa Tanzania HAWAJITAMBUI na WALA HAWAJUI WANAMTUMIKIA NANI! Hawana Rafiki wa kudumu wala Adui wa Kudumu! LOWASSA FISADI,LEO LOWASSA JEMBE! NAPE VUVUZELA leo NAPE JEMBE kwa kuwa "amekurupuka" kutoa tamko la kulaani Kabla ya Taarifa ya uchunguzi wa kamati yake aliyounda kumfikia mezani!

Baada ya kusoma hayo MAFUNZO niliyopata kuhusu "SAKATA" la RC PAUL MAKONDA embu njoo sasa nikupitishe kwenye hizi "hypothesis" zangu kabla hamja-conclude jambo lolote.

Observation moja muhimu kwanza ni hii hapa: Watanzania wengi, Wanasiasa,Wasomi na Wananchi wa kawaida wanafananishwa na mnyama mmoja mwenye umbo kubwa sana sawa na Uwanja wa mpira wa miguu lakini ni mnyama mwenye kichwa kidogo mithili ya bakuli ndogo ya kulia supu! Uwezo wa mnyama huyu kufikiri ni mdogo sana na kuhisi chochote ni mpaka umguse kichwani.( Their brains are very small to entertain two big events at once ! they must drop one event to entertain the other !) ! Ndio maana Nchi hii ni ya MATUKIO hili likija litafunika hili na hakuna impact yoyote na hata hili la RC Paul Makonda litapita muda si mrefu kama unabisha subiri Bunge lianze April! RC Paul Makonda wewe vumilia tu bado KITAMBO KIDOGO WATASAHAU TU!

HYPOTHESIS YA KWANZA:
Nimesoma kwa utulivu sana Uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI kuhusu Paul Makonda,Mtu aliyesemwa na akina "Askofu" Gwajima kuwa Paul Christian Makonda anatumia vyeti vyake Ndugu Paul Pierre Christian amekanusha vizuri sana na pia hana dada aitwaye Christina aliyetajwa na akina "Askofu" Gwajima. Hakuna dhambi yoyote jina lako kufanana na la mwingine, Juma Ali wako wangapi Zanzibar? Mohamedi Ali wako wangapi Duniani?!
Sheria inaruhusu kubadili jina na RC Paul Christian Makonda na kama ni kweli alikula kiapo mahakamani kubadili jina basi alijua jina alilokuwa akitaka kutumia la PAUL CHRISTIAN MAKONDA si lake la awali! Kwa nini basi aliende mahakamani?

HYPOTHESIS YA PILI;
Je PAUL CHRISTIAN MAKONDA hawezi kuwa ni mtu makini mwenye "SPECIAL MISSION" kutoka "KITENGO" fulani anayo-accomplish ?!
"Qualities "anazoonyesha RC PAUL MAKONDA zinazoweza ku-support hii hypothesis ni hii ya kupoteza "initial identity yake",pili angalia comments za Mzee Khamesse na familia yake ni watu ambao wamekuwa "disappointed" na tabia za RC PAUL MAKONDA, Nawanukuu kwa mujibu wa JAMHURI, " alikuja hapa kama mara mbili saa saba usiku na saa tano usiku,hakuingia ndani! Hapokei simu na namba anazowapa ni feki muda wote hazipatikani!
Kwa utamuduni wa kiafrika kwa watu waliokulea na tena kwa MUSUKUMA kama PAUL MAKONDA na pia kwa umaarufu na hesima aliyonayo Mzee Suleiman Khamesse lazima kuna KITU HAPA si Bure!!!!!

HYPOTHESIS YA TATU;
Katika vita hii ya Madawa ya kulevya tunajua RC PAUL MAKONDA amefanya jambo ambalo hata Marehemu Amina Chifupa alitaka kujaribu lakini hakulifikia.Kilichompata Amina Chifupa sote tunajua.Hivyo hawa WAUZA UNGA NA WATEGEMEZI WAO HAWAWEZI KUMFURAHIA RC PAUL MAKONDA LAZIMA WAJARIBU KUMWANGAMIZA TU! Na hapa Mheshimiwa Rais DR. JMP kama unaujua ukweli kuhusu kijana huyu basi please MLINDE KWA GHARAMA YOYOTE!
Ndio maana unapoona NAPE NNAUYE anatukuzwa kuwa ni jembe japo ukweli ni kuwa "AMEKURUPUKA" sana na kutozingatia ile dhana ya "collective responsibilty". WENGI WANAPIGANA VITA YA WAUZA UNGA DHIDI YA RC PAUL MAKONDA BILA WAO KUJUA au KWA KUJUA na Nape Nnauye AKIWEMO!

HYPOTHESIS YA NNE;
Kuhusu RC PAUL MAKONDA kuvamia kituo cha CLOUDS pamoja na kupewa Magari na Watuhumiwa wa biashara ya Madawa ya kulevya yaani kampuni za TANGA PETROLEUM LIMITED NA NAS HAULAGE LIMITED. Hapa nikiri wazi kuwa najenga hoja yangu kufuatia maarifa niliyopata kutokana na kusoma vitabu vifuatavyo: Kitabu cha The Book of Five Rings cha Mjapani Miyamoto Musashi, Kitabu cha 48 Rules of Power ,Kitabu cha Lucifer Principles cha Howard Bloom na Kitabu cha Mwanamapinduzi wa Kichina Sun Tzu cha "The Art of War".

Ukiangalia kwa hao marafiki zake kwa pamoja RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA amejaribu sana kujenga nao urafiki wa karibu mno! Je hii HAIWEZI kuwa ni strategy ya "kum-nail" adui ?! Je CLOUDS media Group hawatajwitajwi katika hii biashara HARAMU ya Madawa ya Kulevya?! Chunguza na fuatilia kifo cha Msanii Albert Mangwea kama MKONO wa CLOUDS MEDIA GROUP hautajwitajwi.

RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA anaweza kuwa ni mtu "HATARI" kuliko anavyochukuliwa ,kubezwa na kudhalilishwa na WATU WENYE UPEO MDOGO kama yule Mnyama niliyemwelezea hapo juu!

Yawezekana RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA akawa sawa na mtu anayetupia kuku wake mahindi pale tu anapotaka kumkamata ili amchinje! ZITTO KABWE anasema ameambiwa kuwa kile kikosi alichotumia RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA "kuvamia" CLOUDS kilikuwa maalum ambacho idhini yake hutolewa na Rais au Boss TISS. Je,tunajuaje kama RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA alitumia style ile ya YUDA ISKARIOTE aliyotumia kumtambulisha YESU Christo kwa wale maadui waliofika bustanini kumkamata? Labda RC PAUL MAKONDA "alinusa" kuwa CLOUDS MEDIA GROUP depot yao ya "UNGA" wameihamishia Studio na hivyo akaona aende na kikosi maalum incase ameukuta huo "UNGA" upo awakombe na incase ameukosa awapotezee tu kuwa yeye ni mtu wao na anafuatilia "Kipindi chake".

Kwanini isiwezekane hivyo kama ni huyu PAUL CHRISTIAN MAKONDA ambaye alituhumiwa kumfunga Ridhiwani Kikwete kamba za viatu na bado akaja kumuorodhesha katika orodha ya watu 97 anaowatuhumu kufanya Biashara ya dawa za kulevya!

Amemtaja Ridhiwani Kikwete na Yusufu Manji kuhusika na biashara ya Madawa ya kulevya kitu ambacho MWIGULU NCHEMBA hawezi kufanya hata kama angekuwa na ushahidi mkononi!

Tungekuwa na Waandishi makini wangechunguza RC Paul Makonda anapokuwa nje ya Nchi anaongea na akina nani MISSIONS zake ni zipi lakini kwa hawa wetu ambao wakiamka wanakimbia kuangalia leo Mange Kimambi ame -post nini au Jumapili hii "Askofu" Gwajima atamchanaje Paul Makonda!

Hivi ukiwa hujapewa Vyeti uangalie na ukaambiwa uwasikilize wakijenga hoja SAED KUBENEA, BONIPHACE JACOB (MAYOR WA UBUNGO) na RC PAUL MAKONDA nani utasema ana ZIRO! obviousily ni KUBENEA na BONIPHACE JACOB! Je,ZIRO ya Paul Makonda haiwezi kuwa ni ya kutengeneza kwa "SPECIAL MISSION".?!

Albert Einstein alipata kusema kuwa akili iliyotumika kutengeneza tatizo haiwezi kutumika kutatua tatizo hilo.NDUGU WATANZANIA TUTAMBUE KUWA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA NI NGUMU KULIKO TUNAVYOFIKIRIA na kama unabisha kamuulize JAKAYA MRISHO KIKWETE au WILLIAM LUKUVI.

Unayepiga kelele bila kuruhusu kichwa chako kufanya kazi piga tu kelele LAKINI TAMBUA KUWA yawezekana unapiga kelele bila kujua kuwa wewe ni sawa tu na MBUZI aliyeko kwenye banda la mpika supu!
Your intellectual ability is impecable. there is no doubt about that. But hizo sifa na kujaribu kumhusisha huyu mkuu na TISS ni stori za kusadikika even yourself don't know what you are talking about. Ina maana hata wachambuzi mahiri wa tasnia ya ujasusi wameshindwa kuingamua hii angle yako mfano Everist Chahali halafu wewe ndo unayejua zaidi. The evidence you have presented so far is inconclusive ni wa kuunga unga (anecdote)..So geraa raa here...
 
braza ningekuwa na dada mzuri ningekupa buuure kwa haya uliyoyaandika.
 
Mtoa mada kajitahidi kushawishi hadi kwa nguvu za giza. Anataka kuuhadaa umma watanzania kuwa Bashite hana hatia.

Mtoa mada kashindwa kabisa kutoa sababu zinazowafanya Watanzania kugusagusa habari bila kufikia hatima. Nakusaidia kuwa sababu ni kwamba serikali ya CCM inapenda sana kufanyia kazi majungu na inawakuza sana waleta majungu.

Bashite nilimfuta pale alipowataja akina Lowasa kuwa wanaharibu chama japo hakusema sababu. Yaliyofuata yoooote ni mwendelezo wa laani zinazomkumba huyu bwana. Muda ndio utaongea. Wa kudanganywa na vijimaneno hivi viwili ndio huyo mnyama mkuuubwa lakini bichwa dogo. Naamini sio wengi wa hivyo hapa nchini. Hata CCM wenyewe wana akili kabisa ila ni wavivu wa kufikiri. Sio kweli kwamba hawana akili kama mtoa mada unavyodhani. Saikojia yako imekupotosha sana
 
Back
Top Bottom