Watanzania bwana!! Walitaka Rais anayeongea sana, sasa leo hawataki kumsikia akiongea

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,943
18,665
Watanzania hamjielewi mnataka nini. Kwanza hii hoja kuwa Raisi awe muongeaji sana nilikuwa nikipingana nayo sana kipindi cha uchaguzi.

Wengi walimbeza EL kuwa hawezi hata kuongea wengine mara hajui kujenga hoja. Nilikuwa naishia kuwauliza, "hivi nyie mnatafuta kiongozi au mrithi wa mzee yusufu?". Hata niliweza kuwaeleza kuwa hiyu mnayedai anajua kuongea akipelekwa kwenye miji ya mwezetu ni bubu. Ila walinibishia sana.

Hayawi hayawi sasa yakawa. Muongeaji akachukua nchi alianza na kumpa vidonge JK siku anafungua bunge. Nilimuhurumia sana JK siku iyo. Baada ya apo Akaendelea na tabia ya kuongea ovyo bila kuangalia anaongea wapi, na nani na wakati gani. Siku hazikupita nyingi mara Watanzania wakaanza kumuita "mropokaji" wengine "mkurupukaji" wengine "uchwara"

Humu JF kuna uzi ulikuwa ukipendekeza kuwa Raisa azungumze siku ya mwaka mpya. Ukiangalia kwenye huo uzi asilimia kubwa walikuwa hawataki hata kumsikia akiongea. Wengi walidai bora akaekimya asije waanzishia mwaka vibaya.

Mungu si asumani mweshimiwa akaibukia kagera siku baada ya mwaka mpya. Katema cheche hadi leo ni gumzo mitaani.

Nachofurahia hapa ni kuwa hata wale niliokuwa nikiwaeleza kuwa Tanzania inahitaji kiongozi sio muongeaji, leo wameanza kunielewa. Hawa ndyo wanajuta. Hawa ndyo wanandugu na watoto waliokosa mikopo na wengine ajira. Wengine wamebomokewa na nyumba zao kagera, wengine biashara zao zimedoda na wengine nyumba zao zimepitiwa na bomoa bomoa.

Sasa ili liwe fundisho kwenu. Muwe mnakuwa makini na wanasiasa. Sifa ya mwanasiasa ni kuongea. Lakini sifa ya kiongozi si kuongea bali ni kufanya matendo.
TANZANIA INAHITAJI KIONGOZI SIO MWANASIASA
 
061105a29f344ee95b9225173b21ae56.jpg
 
Magufuli alisema alikuta hazina pakavu, yawezekana serikali iliyopita kwa kuhofia kuwa wapinzani wangechukua dola waligawana hazina yote, baada ya kukuru kakara za kuibiwa na kuiba kura wakarudi wao wenyewe ikulu.

Kisha wamemuachia mzigo mwenzao ahangaike nao, akiwa bize kuhangaika na hilo zigo mtu mwenye historia ya kupendekeza kinguvu watu wale majani ili ndege inunuliwe unafikiri atakuwa anaongeaje mbele za watu? Levo yake ya uongo unadhani itakua wapi? Levo Ya kujisifu na kushushua wengine je?

Ila sina uhakika kama anafanya haya yote ili hazina kuwe kama zamani ninawaza tu.
 
Atakuja rais mwingine mtatamani arudi Magufuli, kumbukeni jinsi tulivyomponda Kikwete, kaondoka sasahivi tunamtamani.
Kimsingi hatujui ni nani tunayemtaka awe rais
Acha izo story za ndotoni. Mbona kupindi cha kikwete watu hawakumkumbuka mkapa. Kama ananyota ya kutokupendwa hapendwi tu.
 
Acha izo story za ndotoni. Mbona kupindi cha kikwete watu hawakumkumbuka mkapa. Kama ananyota ya kutokupendwa hapendwi tu.
Unaota wewe
Watu wakati wa Kikwete walisema bora mkapa, mara mkapa alijenga uchumi, mara mkapa alikua na akili, mara mkapa alikua mtekelezaji sera huyu Kikwete kazi kuchekacheka tu, sasa kaja Magufuli asiyechekacheka mmeanza kulialia
 
Unaota wewe
Watu wakati wa Kikwete walisema bora mkapa, mara mkapa alijenga uchumi, mara mkapa alikua na akili, mara mkapa alikua mtekelezaji sera huyu Kikwete kazi kuchekacheka tu, sasa kaja Magufuli asiyechekacheka mmeanza kulialia
Izo ni story hakuna alye mkumbuka mkapa kama anavyokumbukwa kikwete leo
 
Izo ni story hakuna alye mkumbuka mkapa kama anavyokumbukwa kikwete leo
Binadamu tunawahi kusahau sana, watu walimkejeli Kikwete kuhusu ile slogan yake ya Maisha bora kwa kila mtanzania, watu walimponda sana Kikwete, watu walimuandika vibaya Kikwete lakini hakuna aliyepelekwa selo wala kukamatwa, sasa hali imebadilika kaja asiyevumilia utani wala kejeli, Lema yuko selo, vijana mbalimbali wamsfikishwa mahakamani lazima uone mambo ni magumu, lazima uone bora kikwete maana alijua kuvumilia hata ujinga wa watu, hivi unadhani zile bilioni walizogawana akina Tibaijuka kwa upepo wa sasa wangepata hiyo jeuri? Lazima umkumbuke japo ulimponda kua ni dhaifu, sasa kaja asiyekua dhaifu tena wacha uisome namba hakuna ujanja ujanja
59305b90aa1e385f59f58bfa4589ba6d.jpg
 
Izo ni story hakuna alye mkumbuka mkapa kama anavyokumbukwa kikwete leo
Mkuu wewe ni wale wale waafrika wasiokuwa na shukrani.

Ukipewa mwezi utataka upewe sayari nyingine, ukipewa hiyo sayari utataka jua.

Jifunze kuishi na mazingira usiyoyapenda, ili uweze kuepuka maumivu ya moyo.
 
Back
Top Bottom