Watanzania bara hawana udini

Swali la msingi, majibu yangu yatakuwa based on Plato’ rationale on civil service (he termed it ‘philosophers king’).


For any serious politician, reading Plato’s ‘Repiblic’ is like canon law; the book is the backbone of western government civil service’s succession planning.
 
🙏🙏🙏

Cha msingi ni kukemea pepo la ramli chonganishi ukipata wasaa.

Ngumu kugombana na kila mtu, maana kwa siku kuna wastani wa mada kama 10 za uchonganishi wa udini; uwezi jibizana na wote.

Muhimu ni kuitetea jamii yetu, unapopata nguvu;

Tanzania bara aina udini. Hizi ni narrative tu ambazo watu wachache wanatuuzia kwa promotion ya JF (maana watu wameshalalamika sana kwa uongozi wa JF, juu ya udini) wao wala.
 
Imagine First son anafadhili press conference ambazo dhamira yake ni kulipasua taifa kidini bila kujali athari zake hili yeye na mama yake waendelee kubaki madarakani, halafi mkuu wa usalama wa taifa anaangalia tu,IGP anaangalia tu, CDF naye anaangalia tu kisa tu wamejaziwa mihela kwenye accounts zao

...sasa hao si mazezeta ambao akili zao zimefubazwa na rushwa kiasi cha kuliacha taifa liteketee, hivi mtu kama Davis Mwamunyange angekubali huu ujinga kweli?
 
Udini ni kete zinazotumiwa na ccm kuendelea kubaki madarakani kwa shuruti. Iwapo ccm haitakubali kuwa hiki si kizazi chake, basi itaendelea kutumia kete chafu za divide & rule ili iendelee kusalia madarakani. Ni suala la nyie wanaccm kukubali kuwa wakati ukuta.
 
Udini upo tena sana sana. Ni Waislam ndio tunatulia tu maisha yaendelee, tuko na subra, ila udini upo sana sana sana sana.
 



Tushangae wote ndugu yangu. Hili wanaloita udini ni jambo wanalo mno. Watu wanachuki mno dhidi ya Waislam, halafu wanaona kawaida kabisa. Umetoa mifano ya nyuzi za baadhi ya maustadh wanaotuhumiwa ubakaji au ulawiti zinajaa matusi dhidi ya Waislam na Dini yao, halafu mtu anakuambia ni wachache tu hao! Kwanini nyuzi za mapadri wanaotuhumiwa kwa ulawiti na ubakaji na makosa mengine hazijai sana?

Kuna nyuzi za uchokozi na kashfa zinazoanzishwa mfululizo humu mwezi wa Ramadhaan. Watu wamejaa chuki na husda.

Kutwa kucha kuwatukana Waislam na kuwakejeli, mara hawana akili, mara sijui hawajasoma, unaona kabisa chuki na dharau katika midomo yao.

Kukiwa na viteuzi kukawa na Waislam kidogo tu, kuna vikelele, hii sio bahati mbaya wala utani, ni chuki. Ila Waislam wao maskini wako wachache serikalini na kwenye teuzi, wakilalamika kidogo wanaitwa wadini na wanakejeliwa kuwa tatizo hawajaenda shule, ila wakiteuliwa kidogo tu utasikia kiongozi anaendekeza udini. Fresh!

Nyuzi na hata mitandao mengine kuna malalamiko ya kuwalaumu wafanyabiashara kama Bakhresa kwa udini katika Azam. Ila kina Reginald Mengi na IPP yao Waislam wakiwa wachache ni sawa. Freshi!

Kukiwa na vi tamthilia vya kituruki kidogo tu ni udini, ila kuwekwa movies za Hollywood zinazowa portray Waislam vibaya tena kwa uongo ni sawa! Filamu za bongo movie za kina Kanumba zenye maudhui ya kanisa na ulokole ni sawa sio udini!

Huo unaoitwa udugu na upendo ni wa kinafki, na Waislam uzuri hatuna huo upendo wa maigizo.


Waislam tuko na subra na tunaishi kwa wema na uadilifu na wasio Waislam, tukijua kuwa wana chuki na sisi na husda na roho mbaya wengi wao. Ila tunaishi nao kwa wema.

Ukidhihirisha chuki iliyopo unaitwa mdini na sasa hivi walipoibuka baadhi ya Waislam kulalamika kidogo kuna watu wakijifanya wajanja eti wakataka kuwanyamazisha kwa kuunda dini mpya ya kipagani eti wakijifanya hawana chuki, na wakati huo huo kwa dini yao mpya hiyo ya kipagani wanaukejeli Uislam na kuuvunjia heshima.

Waislam, hatutaki kuvunjiwa heshima Dini yetu Tukufu, kila mtu abaki na Dini yake. Tuishi kwa wema, na kuheshimiana. Kila mtu na Dini yake. Tuishi kwa Amani.
 
Wakristo wa Tanganyika wadini wakubwa, ndiyo ma-architect wa udini wakiongozwa na Julius
 
Ila kwenye siasa utakuta waislamu fulani..ni wachache tu anamtetea rais mhuni kwa bidii kwa kua eti dini yake. Tuacheni wandugu. Tusiruhusu viongozi wabovu kutumia dini kujilinda madarakani.
 
Hao hao ndio wanaongoza hapa Jf kwa nyuzi mbaya na maneno machafu ya kidini pamoja na dhihaka.

Tunachekeana tu moyoni chuki zimetawlaa
Chuki unazo wewe na sijui kama mada umeisoma ukaielewa,ok kwa maneno mengine (labda hivi ndiyo utaelewa) alichomaanisha mleta mada Wabara na dini zetu tunazi-practice tukiwa kwenye nyumba zetu za ibada tu nje ya hapo sisi ni wamoja.

Sijui kwanini watu huwa mnawawazia wenzenu mabaya kisa mmetofautiana imani,bora itikadi za kisiasa lakini kitu imani sidhani na kwa nini (kwa maelezo yako) una chuki inavuja moyoni mwako?
 
Wasomi wa bara ndio wenye udini.
Bara hakuna chuki za udini ! miaka ya 70's Marehemu Babu yangu alikuwa miongoni mwa waislamu wasiozidi 5 katika kijiji chenye wakazi 5000 Wapagani,Wakristo na Waislamu wasiozidi 5 lkn alipewa jukumu la kuchinja vitoweo kila ilipotokea sherehe yoyote pale kijijini na aliheshimiwa sn sababu ya dini yake.. udini nchi hii unaletwa na watu wa pwani hasa Wazanzibari.
 
Watanzania bara ndiyo nani.

Mimi nawafahamu Watanganyika tu, sababu hata hao kuvuka bahari ukilazimisha kuwaita watanzania visiwani nao watakataa na kujiita Wazanzibar.
 
Hicho kitabu kimeelezea vizuri sana jinsi vile good succession planning inavyoandaa mazingira ya uwepo wa accountability kwa kiongozi baada ya kupewa ridhaa, na hapo ndio tunaona umuhimu wa vetting process ya maana.

Pia ime articulate kiongozi lazima awe na elements za kifalsafa zinazompa ujasiri wa kimamlaka kwenye maamuzi ya mambo muhimu..(rulership elements).
 
Nyerere gani unaemzungumzia wewe alipika udini. Nyerere alikuwa mjenga taifa na sio mdini.
Huwa unanishangaza sana.
Ni wapi katika maandishi yangu nimeyaandika, au hata kuelekea kuwa na maana kama hii uliyoweka hapa wewe!.

Kwa mara ya kwanza, naomba kwa UTULIVU MKUBWA, unionyeshe mahali nilipoandika maneno yanayoleta maana kama hayo yako hapo juu.

Tafadhali; naomba kwa heshima kabisa kwako, unionyeshe hayo maneno.
Natumaini kuwa utanisaidia katika hili, ili niwe mwangalifu zaidi kila ninapojibishana na wewe, nisifanye makosa tena.
 
Hawatafanikiwa, usijali, it's too late kwa hayo, ni sawa sawa na kuanza kulewa ukiwa na miaka 75, tumepita hapo kwenye udini mda sana
Napenda sana kukubaliana na wewe; lakini sijui unatumia kipimo gani kujuwa kuwa kuna udini au hakuna udini katika jamii..

Uamini wangu ni kwamba tukiendelea kuwa na uongozi mbovu kama huu tunaoushuhudia sasa, itaniwia vigumu kukubaliana na haya uliyoyaeleza hapa. Nchi hii itagawanyika sana kwa misingi ya kidini. Watu watabaguana waziwazi, na hata hali ya usalama nchini itakuwa ni tete sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…