Watanzania 65 wauza 'unga' kunyongwa China

Watanzania 65 wauza 'unga' kunyongwa China

yegella

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Posts
3,113
Reaction score
1,104
William-lukuvi-June25-2014.jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William
Lukuvi, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuhusu
Maadhimisho ya Siku ya Dawa ya Kulevya Duniani yanayotarajiwa kufanyika kitaifa jijini Mbeya


- Ni sehemu ya wengine 338 waoozea jela

Vijana 65 wa Tanzania wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Vijana hao ni kati ya zaidi ya 403 wa Tanzania wanaoshikiliwa katika nchi mbalimbali duniani kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara hizo.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, mjini Dodoma wakati akizungumzia Maadhimisho ya Siku Dawa za Kulevya Duniani yanayofanyika Juni 26 kila mwaka.

Lukuvi alisema kuwa kwa mwaka huu maadhimisho hayo ya kesho, kitaifa yatafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nzovwe jijini Mbeya na Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

"Tangu mwaka 2008 kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wenye asili ya Kitanzania kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi, mpaka hivi sasa idadi yao ni kubwa kiasi cha kufikia zaidi ya 400, na wanashikiliwa katika nchi mbalimbali ambazo pia adhabu zao zinatofautiana kulingana na sheria za nchi hizo," alisema Lukuvi.

NCHI WANAKOSHIKILIWA
Alizitaja baadhi ya nchi ambako vijana hao wanashikiliwa kuwa ni Brazil (108), Hong Kong (118), Kenya (34), Pakistan (16) na China 65.

Nyingine ni Japan (7), Malawi (5), Uganda (3), Uswisi (2), Marekani (2), Uturuki (1), Botswana (5) na Msumbiji (1).
"Orodha ya nchi waliko vijana hao ni defu zaidi," alisema.

Akizungumzia maadhimisho hayo kwa nchini, Lukuvi alisema kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni ‘Uteja wa dawa za kulevya unazuilika na kutibika, chukua hatua'.

AlisemaTanzania imeendelea kuwa miongoni mwa nchi zenye tatizo kubwa la dawa za kulevya kulingana na takwimu za ukamataji wa dawa hizo.

Kwa mujibu wa Lukuvi, kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu kiasi cha kilo 220 za dawa hizo aina ya Heroine na watuhumwa 18 walikamatwa huku pia kilo 15.4 za Cocaine zilikamatwa na watuhumiwa saba.

Lukuvi alisema kwa sasa dawa za kulevya ni tishio kubwa kwa maendeleo ya taifa kwa sababu imethibitika kuwa matumizi yake hupunguza tija na ufanisi wa nguvu kazi ya taifa.

SHERIA MPYA YAJA
Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo, Serikali imekamilisha muswada wa sheria ya dawa za kulevya ambao kama utapitishwa bungeni na kuwa sheri kama ulivyo, unaweza kusaidia kwa Kiwango kikubwa kupunguza tatizo hilo.

Lukuvi alisema tofauti na jinsi ilivyo sheria ya sasa, sheria mpya itaondoa adhabu ya faini na watuhumiwa kunyimwa dhamana wanapokamatwa, hali ambayo itasaidia kukabiliana na wasafirishaji na wauzaji wa dawa hizo.

Kwa mujibu wa Lukuvi, sheria hiyo itakwenda sambamba na uundaji wa chombo imara cha kushughulikia dawa za kulevya ambacho kitakuwa na uwezo wa kupeleleza, kukamata na kushitaki watuhumiwa wa dawa za kulevya kama ilivyo kwa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Alisema kuwa muswada huo tayari umekamilika na kwamba wakati wowote unaweza kuwasilishwa bungeni ili upitishwe hatimaye kuwa sheria.

Alisema maadhimisho hayo pia yatafanyika katika ngazi ya mkoa nchini na kuwaomba wananchi kujitokeza kushiriki ili waweze kupata elimu ya kutosha juu ya madhara na vita dhidi ya dawa hizo.

KANDORO ANENA
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka wananchi mkoani mwake walioathirika na dawa za kulevya kujitokeza kwa wingi kupima afya zao, kupata tiba na ushauri katika maadhimisho hayo.

Kandoro alifafanua kuwa maadhimisho hayo yanafanyika mkoani humo kutokana na takwimu kuonyesha una kiwango kikubwa cha tatizo la dawa za kulevya kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na kutoa mfano wa bangi ambayo inalimwa kwa wingi.

"Kama mnavyojua, mkoa wetu upo mpakani hivyo tuna changamoto kubwa sana ya uingizaji wa dawa hizi, mara nyingi watu hukamatwa katika mipaka ya Tunduma na Kasumulo, hivyo ni budi elimu hii kutolewa kwa wananchi ili tushirikiane wote katika kutokomeza vita hii tuliyonayo," alisema Kandoro.

Alisema kuwa pombe aina ya viroba vya bei nafuu vitokavyo Malawi ni changamoto pia kwani vijana wengi wanavitumia, hivyo kuathirika kwa kiasi kikubwa.


Source: Nipashe
 
Hicho ni kichwa cha habari, habari kamili iko wapi? Waje wawakamate na hao waliowatuma kwa sababu rais wao alikuja na makamu wake kaja juzi tu na sijawasikia wakilalamika kuhusu madawa ya kulevya kutoka Tanzania.
 
Habari,
Katika kipindi cha magazeti asubuhi zaidi ya watanzania 35 wanasubiriwa kunyongwa nchini China kutokana na kujihusisha na madawa ya kulevya.
Nawasilisha

Labda si wewe hujasikia vizuri au uliyemsikia hajaongea sawa.

China wanasheria ya kuuwa kwa watu wanaokamatwa wakiingiza na kusambaza madawa ya kulevya lakini si kwa kunyonga.

Kwa hiyo hao Watanzania itakuwa wamehukumiwa kuuliwa lakini nakuhakikishia hukumu hiyo (kama ni habari za kweli) basi haitakuwa kwa kunyongwa, wanatandikwa risasi za kisogoni.
 
Waanze kunyonga wachina waliopo tanzania wanaofanya ujangili bhana ndo wanyonge na wa tz wa mapouda china
 
Kwakuwa ni PUNDA ndio mnashabakia kwamba wanyongwe tu, Hivi angekuwemo yule aliyesababisha tukakabidhi gesi yetu ya Msimbati kwa Jamhuri ya Watu wa China, kauli zingekuwa hizi tena?!
 
Waanze kunyonga wachina waliopo tanzania wanaofanya ujangili bhana ndo wanyonge na wa tz wa mapouda china

Watazubutu unataka wakose misaada makam wa rais china kasema vijana wake waachiwe haraka sana.
 
Wanyongwe kwakua wamepoteza utashi wao nakuamua kuwa kama punda au ng'ombe.sisi tujiulize hao watu nitajiri au masikini? Kama maskini kafikaje china? Kama amepelekwa kwanini asigome?
 
Na wale tulio wakamata na pembe za ndov nao cjui tunawafanya nin
 
Watoto wa masikini wananyongwa kwasababu ya kukosa ajira lakini maboss waliowatuma wanadunda mtaani bila hata kutajwa,Mwenyezi Mungu azilaze mahali pema roho zao,inauma sn!
 
Kwakuwa ni PUNDA ndio mnashabakia kwamba wanyongwe tu, Hivi angekuwemo yule aliyesababisha tukakabidhi gesi yetu ya Msimbati kwa Jamhuri ya Watu wa China, kauli zingekuwa hizi tena?!

Tanzania haijakabidhi gesi asili kwa China. Gesi hiyo bado inamilikiwa na nchi na uendelezaji wake hufanywa chini ya mikataba wa kugawa na mapato. Kuhusu watanzania wanaosubiri kunyongwa huko China, ieleweke kuwa wao wenyewe ndiyo walichagua kujiingiza kwenye biashara hiyo na kwa maana hiyo inabidi wavune walichopanda.
 
Hakika kwa sasa kuyumia passport ya Tanzania ni noma. Nakumbuka last week nikiwa natoka Washington DC kurudi Doha, nikiwa airport ya Dullus nilikutana na mama mmoja mtu mzima akiwa na umri usipungua miaka 65 kutoka Tanzania akiwa na bint yake wakiwa nao wanasubiri Qatar airways kupitia Doha kwenda Dar.Basi tukawa tunajinafasi kuongea lugha ya kiswahili wakti tunasubiri ndege.

Hakika mimi na mke wangu tulistahajabu sana huyo mama na binti yake walivyopekuliwa kwa takriban dakika 25 kila mmoja na baaade kuruhusiwa na tulipowauliza vipi mama kulikoni mnapekuliwa hivyo kama waNigeria akasema mambo ya Unga hayo ndio yanayotufanya tusiaminike Duniani.

Hakika Unga umeiweka pabaya sana Tanzania na waTanzania wasiaminiwe popote wanapopita Duniani.
 
ataje na wageni waliokamatwa na dawa hizo walioko jela kama keko,ukonga,mbweni,wami
 
Tatizo la Tanzania ni kujifanya watu wa huruma,Ona sasa China inavo2adhibu na bado mpaka 2fikie milion 20 tu.
 
Vijana 65 wa Tanzania wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Vijana hao ni kati ya zaidi ya 403 wa Tanzania wanaoshikiliwa katika nchi mbalimbali duniani kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara hizo. Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, mjini Dodoma wakati akizungumzia Maadhimisho ya Siku Dawa za Kulevya Duniani yanayofanyika Juni 26 kila mwaka.

“Tangu mwaka 2008 kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wenye asili ya Kitanzania kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi, mpaka hivi sasa idadi yao ni kubwa kiasi cha kufikia zaidi ya 400, na wanashikiliwa katika nchi mbalimbali ambazo pia adhabu zao zinatofautiana kulingana na sheria za nchi hizo,” alisema Lukuvi.

Alizitaja baadhi ya nchi ambako vijana hao wanashikiliwa kuwa ni Brazil (108), Hong Kong (118), Kenya (34), Pakistan (16) na China 65. Nyingine ni Japan (7), Malawi (5), Uganda (3), Uswisi (2), Marekani (2), Uturuki (1), Botswana (5) na Msumbiji (1). “Orodha ya nchi waliko vijana hao ni defu zaidi,” alisema.

Akizungumzia maadhimisho hayo kwa nchini, Lukuvi alisema kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni ‘Uteja wa dawa za kulevya unazuilika na kutibika, chukua hatua'. AlisemaTanzania imeendelea kuwa miongoni mwa nchi zenye tatizo kubwa la dawa za kulevya kulingana na takwimu za ukamataji wa dawa hizo. Kwa mujibu wa Lukuvi, kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu kiasi cha kilo 220 za dawa hizo aina ya Heroine na watuhumwa 18 walikamatwa huku pia kilo 15.4 za Cocaine zilikamatwa na watuhumiwa saba.

Chanzo: Nipashe.
 
Back
Top Bottom