Watangazaji wa bongo

Watangazaji wa bongo

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2008
Posts
255
Reaction score
78
Nikiwa mfuatiliaji mkubwa wa habari za Runinga, redio na magazeti nasikitishwa sana na kiwango kidogo cha uelewa kinachoonyoeshwa na watangazaji wetu. Kwa ujumla wa wana udhaifu mkubwa sana katika maeneo yafuatayo:

1. Kutamka kwa usahihi majina ya watu na sehemu- sikilizeni radio za nje ambazo watangazaji wanatamka kwa usahihi majina hayo
2. Kuchanganya maneno ya kiingereza wanapoongea kiswahili. Mfano watangazaji wa Radio magic utasikia unajua ''Arsenal wapo weak sana katika kudefence'' mifani ni mingi sana- Ushauri kma lugha haipandi tumia kishwahili wakati wote au sio mbya kujiunga na mafunzo ya kiingereza
3. Kuchanganya mambo- utasikia Rooney alifunga goli akiwa kwenye impossible angle-ukweli huwezi kufunga goli ukiwa impossible angle.
4. Kutokamilisha habari- wakiripoti tukio leo basi ndo mwisho hakuna habari za kufuatilia baada ya hapo. Mfano tukio la vijana wanaodaiwa kufufuka mwanza na Njombe, habari hiyo ndio hivyo ilishaisha

......................na mengine mengi tunaweza kuongezea
 
na pia wawe wanajifunza jiografia kidogo..wakitangaza habari za kimataifa hiyo miji wanavyoitamka huwa nahisi kudondoka...khaaa
 
hivi vituo vipo kibongo flavor zaidi kuliko kujuza watu habari. ni mziki masaa yote
 
Juzi kati radio one kwenye kipindi chao cha michezo wakawa kwa mbaali wameweka uefa champions league anthem.

Ilikua imetulia. Safi sana sababu walikua wanatangaza mechi za uefa.

Mara habar hiyo ikaisha, wakaendelea na habari za english Premier league na lìgi nyingine. Kale ka anthem bado kakawa kanaendelea tu. Nkaanza kua bored sasa.

Hii naita lack of situational awareness kwa yule mtangazaji.

Ndo watangazaji wetu hawa!
 
Tuvumiliane wajamani huu uhuru na utitiri wa vyombo vya habari bado mchanga kwetu.........Tukikuwa tutaacha ujinga huo!!
 
Kwa kifupi hakuna udhibiti wa hivi vituo vya runinga na redio kabisa. Kila siku zinakuja kwa wingi kitu ambacho ni kizuri lakini tatizo ni kuwa ubora havina kabisa hata waendeshaji wake hamna kitu kabisa yaani ni thufuri
 
labda hao watangazaji ni wakenya manake huku wenzetu wanavyoongea kiswahili na kuchanganya na kiingereza hata raha hamna. Halafu hao watangazaji wetu wanaopenda kuongea Kiswanglish ukiwaambia tuongee pyua english hawafiki mbali!
 
Watanzania tunapendelea burudani zaidi kuliko habari ndoo maana vipindi vingi kwenye TV na radio ni vya burudani. Magazeti yanayouza ni ya michezo na udaku. Mambo ya msingi hatuna muda wa kuyasoma wala kuyasikiliza.
 
Nilibahatika kutembea MBEYA wiki iliyopita. Yaani Radio zinatia kinyaa kusikiliza. hakuna tofauti ya R wala L. Halafu wanakuwa kama wanawaiga watangazaji wa baadhi ya Radio za DAR
 
Back
Top Bottom