Pharaoh
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 843
- 157
Zanzibar kuna neema tele za Kitalii wa Beach zao nzuri, ila wazanzibari wanatosheka mapema na hawajishugulishi, kwa wabara ni paradise kufanya biashara Zanzibar, wakifanya inawauma wazanzibari na kuanza kuwaandama kwa kila njia ili kuwaondoa, wakikaza uzi inaingilia kati serikali kuu ya zanzibar, wenzetu serikali yao iko karibu nao sana, usishangae muuza magazeti au madafu anaenda ikulu kulalamika, mtu yoyote anafika kwa rais au waziri kwa muda wa masaa sio siku, kwa hiyo kama mtu wa bara akifanikiwa basi mara moja rais anaambiwa, na atashugulikiwa, hiyo ndio zanzibar, lakini bahari ya Tanganyika hasa Dar na Visiwa mbele yake ni paradise za kupumzika watalii, lakini zote zipo mikononi mwa wahindi wanaouuza kebab tu? Makampuni mengi yameshakuja lakini wahindi wanawapokea na kuwatajia mabei makubwa nao wanakimbia? tuseme bara kuna ushamba fulani bado, zanzibar pamoja na style yake ya kuamua mambo kidikteta ndio mana wanafanikiwa, wakiamua fulani aondoke hapa ije kampuni kubwa ili ajira na uchumi ukuo wanakutua, lakini hao wengi wanaomiliki na kukalia ardhi za bara pia ni wazanzibari pia