Rais Mwinyi aongeza kima cha chini cha mshahara kutoka 300,000 kwenda 500,000

Rais Mwinyi aongeza kima cha chini cha mshahara kutoka 300,000 kwenda 500,000

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,005
Reaction score
3,590
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ametangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kutoka TZS 300,000 hadi TZS 500,000 kwa mwezi.

Dkt. Mwinyi amesema kiwango hicho kipya cha mshahara kitaanza kutumika Januari 2027.


======

RAIS DKT. MWINYI ATANGAZA ONGEZEKO LA MSHAHARA KIMA CHA CHINI HADI SH. 500,000

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kutoka shilingi 300,000 hadi shilingi 500,000 kwa mwezi.

Rais Dkt. Mwinyi ametangaza ongezeko hilo la mshahara leo, tarehe 01 Mei 2026, katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Maonesho ya Kilimo Kizimbani, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Dkt. Mwinyi amesema kiwango hicho kipya cha mshahara kitaanza kutolewa kuanzia mwezi Januari 2027, na kufahamisha kuwa hatua hiyo imezingatia hali ya uchumi wa nchi, gharama za maisha, na kuwapatia motisha wafanyakazi ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi.

Rais Dkt. Mwinyi amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Nane imepata mafanikio makubwa tangu ilipoingia madarakani mwaka 2020, kwa kufanikiwa kuimarisha maslahi ya wafanyakazi kupitia kurekebisha na kuongeza mishahara, kufanya mapitio ya posho na marupurupu ya watumishi, pamoja na kuimarisha mafao ya hifadhi ya jamii na kuanzisha mfuko wa bima ya afya kwa wafanyakazi wote pamoja na familia zao.

Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi ametangaza kuwa Serikali imetenga nafasi za ajira 7,500 katika mwaka wa fedha 2026–2027, pamoja na kuendelea kuimarisha maslahi ya wafanyakazi.

Screenshot 2026-05-01 at 14-47-48 Instagram.png

Pia soma: Rais Samia: TUCTA hawakuja na madai mapya. Kadri uchumi wetu unavyoimarika, tutaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi wetu
 
Kama dola sita hivi Kwa siku, 16000 Kwa siku kama huna makato, wafanyakazi nao ni kundi la kuwahurumia Kwa kweli, mzazi kama Una pesa Bora umpeleke mwanao shule ya kueleweka, mwalimu analipwa laki tano hivi kuna kusoma kweli hapo, si ni mwendo wa viboko Tu.
 
ni kweli ila January mbali
Kwa zanzibar hizo ndo gape zake, mana hata sekta inayoajiri watu wengi kwa mwaka inaachaga gepu ya miaka 3 mpaka 5 ndo inaajiri. Vikosi na askali wa idara maalum za smz pekee ndo inawze kuchukua hata watu 400 kwa mkupuo na mara ya mwisho imechukua mwaka 2024 mwezi februari hadi leo holla
 

. Mwinyi atangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kutoka TZS 300,000 hadi TZS 500,000​

20260501125428_-659316527_8841857277815969496_640_410_85_webp.webp


Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ametangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kutoka TZS 300,000 hadi TZS 500,000 kwa mwezi.

Dkt. Mwinyi ametangaza ongezeko hilo Mei 01, 2026 katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Maonesho ya Kilimo Kizimbani, Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo amesema kiwango hicho kipya cha mshahara kitaanza kutolewa kuanzia Januari 2027.

Aidha, amesema uamuzi huo unaenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kuimarisha mazingira ya kazi na kuhakikisha kuwa watumishi wanapata stahiki zao kwa wakati, huku akitoa wito kwa watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii, juhudi, nidhamu na uzalendo ili kuleta maendeleo endelevu Zanzibar.

Mbali na hayo, Dkt. Mwinyi amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wafanyakazi wa sekta ya umma na sekta binafsi, na kwamba itaendelea kushirikiana na vyama vya wafanyakazi kukabiliana na changamoto zote zinazowakabili wafanyakazi nchini.
 
Wazanzibari hawafikii hata idadi ya wakazi wa Dar es Salaam, they can do anything.

Mambo mengine tuwaache tu.
 
Kwa nini watumishi wa Tanganyika muongezwe mishahara?Kwa lipi hasa?Kwani hamkupokea posho wakati wa "uchaguzi"(?) wa 2025?Hazikuwatosha?Mlipaswa mzitunze na kuzigawa vema ziwasaidie masahibu yenu maishani.😛😛😛😛😛😛🫸🫷
 
Kwa nini watumishi wa Tanganyika muongezwe mishahara?Kwa lipi hasa?Kwani hamkupokea posho wakati wa "uchaguzi"(?) wa 2025?Hazikuwatosha?Mlipaswa mzitunze na kuzigawa vema ziwasaidie masahibu yenu maishani.😛😛😛😛😛😛🫸🫷
Wanalipwa na 7000 ya uchwa inawatosha kabisa
 
Back
Top Bottom