Watamfungulia mashitaka au watamwacha?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,026
Reaction score
142,925
Sijui kama Nchimbi alikuwa amejiandaa kukabiliana na dhahma ambazo zinaweza kumkuta baada ya kufukuzwa kutoka CCM na kuachia madaraka haramu aliyokuwa nayo.

Hapa nawaza tu kama labda watamfungulia mashitaka ya kula njama za kufanya uhaini au mapinduzi au whatever.

Nchimbi, kwa nafasi yake haramu aliyokuwa nayo, atakuwa anajua mengi ya kutosha, hususan yale ya Oktoba 29.

Wakimfungulia mashitaka, watakuwa wamefungua boksi la pandora, jambo ambalo sidhani kama wako tayari kukabiliana nalo.

Nyie mnaonaje? Watamfungulia mashitaka au watamwacha aende zake ila labda watamnyanyasa kwa njia zingine kama kumsumbua kupata mafao [kama anayo], labda kumnyang’anya au kumpunguzia walinzi, na kadhalika.

Ila pia kwenye mambo kama haya mara nyingi mtu huwa hayupo peke yake tu.

Huko CCM sijui ni akina nani wengine ambao wako na Nchimbi kwenye yale aliyoyaongea.
 
Nasikia Nchimbi tangu yale mauaji ya October yaliyotokea alipoteza hamu, lakini alishindwa tu kujing'oa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…