Watalii Wafurika SERENGETI kushuhudia NYUMBU wakirejea NYUMBANI toka Mapumzikoni KENYA

Hivi Nyumbu wakienda Maasai Mara huwa wanaenda mapumzikoni au wanaenda kutafuta malisho mapya kutokana na ukame upande wa Serengeti?
 
heri yetu sisi tunapata Kimolo.....tunawasubirije hapa Robanda wapite........naanza kuchukua order.......kwa anaehitaji.....
. Preta nichukulie kilo 3 nipo hapa Fort Ikoma getini
 
Last edited by a moderator:
Wa Kenya wanatuchezea ndevu zetu sana!!JK juzi amewaambia tujipange sote kutangaza utalii,yaani kama anawaomba vile,wenzetu wamejipanga muda mrefu sana,na wanajua wanawalenga wapi hao watalii.....sisi tunasubiria huruma ya watalii wenyewe waulize ndio waambiwe nenda Tanzania utaona hiki,na hiki na kupanda mlima Kilimanjaro
Zamani Tanzania tulikuwa hatutangazi siku hizi na sisi tunatangaza hadi CNN na channel zingine pia!!!!

 
Gys we must wake up na kuachana na na biashara ya kupakwa sifa ambazo hazina tija. Tunapoongelea Serengeti ecosystem tunamaanisha nini! Mfano nani anamiliki Ngorongoro mahesabu yake yanakwenda wapi? In short ncaa ni mali ya ccm no quiz! Grumet Sasakwa ni mali ya nani! Huyu Jones kaingiaje hapo, then wakawafukuza wenyeji waliokuwa wanajipatia protini tangu Adam na Hawa kwa kuwaita porchers, ok waliondolewa je wamepelekwa wapi? Maisha wanayoishi ni chaguo lao au ni 'toka ondoka nenda uendako' Grumet sasa ni nchi nyingine kina Mawala associate ndo wanatumaliza Watz wenzao. Yapo mengi ya kuhoji tuamke na siyo kushabikia gnu wamerudi je unawakatiaga majani au unawachanjaga dawa?

ok, asante kwa contribution to Tanznanians in a Kenyan accent. ........ Katiaga majani!, unawachajanga ndawa!
 
Hivi Nyumbu wakienda Maasai Mara huwa wanaenda mapumzikoni au wanaenda kutafuta malisho mapya kutokana na ukame upande wa Serengeti?

Nadhani ni sahihi kuyaita mapumziko. Wazungu wengi pia wanakuja Afrika kuogopa kibaridi kwao. Sasa nao kutokana na ukame wanaamua kwenda kenya kuganga njaa. Karibuni nyumbu, kila wakati mkienda huko msisahau kurudi nyumbani japo twajua wengi wenu mnaishia pale Carnivore kama mchomo wa kutelemshia tusker!
 
Pengine itasaidia kuwapunguzia jamaa zangu safari za ulaya na marekani....wataanza kwenda serengeti kula bata.
 
Safi sana...picha nzuri! mapumziko nitarejea Arusha...ngorongoro na serengeti.
 
ah kweli tuna hazina za ajabu sana.sasa me nilikuwa na wazo naona kama wanapata shida kuvuka huo mto kwanini tusiwajengee daraja kubwa kabisa ukubwa wake uwe kama daraja la kigamboni hivi??


Na hao viboko na mamba wale wapi? Hayo ndo maisha ya wanyama.
 
Natural wonders of the world mkumbuke kupigamkura jamani!
Ivi msimu wa kupiga kura umeksha au bado waendelea?
 
Da niko Bongo lakini hadi nitakufa sitakuja kuona live haya maajabu mshahara wangu wa ualimu ndo hivyo tena da najuta kuwa mtz
 
Hawa nyumbu wamestukia uchaguzi mkuu kenya umekaribia, wasije kuwa wahanga wa vurugu
 
ah kweli tuna hazina za ajabu sana.sasa me nilikuwa na wazo naona kama wanapata shida kuvuka huo mto kwanini tusiwajengee daraja kubwa kabisa ukubwa wake uwe kama daraja la kigamboni hivi??

Hahahaha swt girl umenifurahisha sana, sasa wewe unataka hao mamba waishi wapi? Nature should not be distubed, let it take its course.
 
Back
Top Bottom