Nimewaita bwana mifugo 2 wamekuja kuwaona wakasema kuwa ni kideri,Ila nimeshindwa kuamini kama ni kideri kweli kutokana na namna ambavyo vifo vinavyotokea dalili zenyewe siyo zakideri,Kuku wanapotembea hawaonyeshi dalili zozote za kuumwa,dalili za kuumwa zinapojitokeza tayari ana kuwaameshaisha kabisa,kinachofuata ni kufa moja kwa moja.Watalamu wamenipa OTC 20% ndiyo ninayowawekea kwenye maji ila hii dawa uliyo ni shauri nitaitafuta ni itumie inaweza kunisadia kwani kuna baadhi ya kuku wana mafua yasiyoisha na nilisoma mahali kuwa dawa hii ina uwezo wa kutibu na mafua pia.Kwa vile hawa kuku nimewafuga kwa ufugaji huria sehemu kubwa huwa wanajitafutia chakula na hili ndilo lililosababisha yote haya ila ninapowafungulia huwa ninawapa pumba ambazo zimechanganywa na dagaa au uduvi.Baadhi ya kuku nimesha wafungia tayari,wenye vifaranga nimewafungia chumba chao pamoja na vifaranga vyao.