Mrejesho wa kuku

Tuliponga

Senior Member
Feb 11, 2014
190
49
Ninawashukuru wajasiria mali wote kwa ushauri wenu mulionipa,kutokana vifo vya ghafla vilivyo kuwa vinatokea kwa kuku wangu.Baada ya kuomba ushauri kwa wajasiria mali chini ya kichwa cha habari Watalamu naomba msaada kuku wanapukutika, pamoja na kwamba nimepata hasara kubwa lakini michango ya wajasiria mali imenisaidia sana.Kwa kuzingatia michango na maoni ya wajasiria mali nilifanya ya fuatao mbali na kutumia tiba mbalimbali ambazo nilielekezwa kuzitumia,

(1)Niliwakamata baadhi ya kuku nikawafungia ndani nikawa ninawatibu wakiwa ndani na wengine nilikuwa ninawatibu bila ya kuwafungia,kuku niliokuwa ninawatibu wakiwa ndani vifo vilipungua sana kati ya kuku 11 niliokuwa nimewafungia ndani ni kuku 2 tu ndiowaliokufa.

Kuku ambao nilikuwa ninawatibu bila ya kuwafungia ndani waliendelea kufa pamoja na kuwapa dawa kama zilele nilizokuwa ninawapa wale ambao nilikuwa nimewafungia ndani.

(2)Mama kuku wote ambao sikuwafungia walikufa wote kati ya vifaranga 50 walivyokuwa navyo vilibaki vifaranga 25 baada ya kufa vifaranga 25 kutokana na ukweli kwamba vifaranga visingeweza kujichunga kutokana na udogo nilivikamata nikavifungia chumba tofauti na wakubwa pamoja na kuwa fungia ndani niliendelea kuwatibu kati ya vifaranga 25 niliowafungia wamekufa vifaranga 7 wamebaki vifaranga 18 na wanaendelea vizuri.

(3) Wakati kuku wanakufa ghafla kulikuwa na kuku3 ambao walikuwa wameatamia na waliweza kutotoa vifaranga 42,Baada ya kutotoa sikuwaruhusu wakanyage nje niliwatengea chumba ambacho nimewafungia baada ya kuwafungia kitu kilichotokea ambacho sikutegemea nilikuta vifaranga vimepungua ghafula bila kuelewa ni kitu gani kilikuwa kimetokea wakati vifaranga pamoja na mama zao huwa havitoki nje.

Nilianza kufuatilia nikagunduwa kuwa panya wamechimba shimo ndani ya chumba,pembeni mwashimo nilikuta kuna vifaranga 12 ambavyo vilikuwa vimekufa na kuliwa vichwa na utumbo kwa sasa ninawasaka panya kama Marekani alivyokuwa ana msaka Osama,kifaranga kimoja kilikufa kwa kukanyagwa na mama yake,jumla ya vifaranga vilivyokufa ni 13 vimebaki 29 hakuna kilichokufa kwa ugonjwa.

Nilichojifunza ni kwamba kuku wakifungiwa ndani ni rahisi kuwatibu na siyo rahisi kupata magonjwa kama wale wanaoachiwa wakizurula hovyo,pia utafikiri kuwa kuku anaye zurura hata akiwa kwenye matibabu akitoka nje ana kwenda kuambukizwa magonjwa tena zaidi pamoja na kwamba yuko kwenye matibabu.
 
hongera sana jitaidi ufuge kibiashara zaidi sasa vile ilikuwa pata potea au bahati nasibu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom