Ninafuga kuku wa kienye ambao wamefika 80 na huwa ninawaachia wajitafutie chakula wenyewe,kwa sasa hivi kuku wangu wameanza kufa ghafula bila ya kujua ni kitu gani kinachosababisha vifo hivyo.Nimewapa chanjo ya kideri mara 3 kila baada ya miezi 3.Cha kushangaza ni kwamba kuku wanaingia bandani wakiwa wazima ninapowafungulia asubuhi ninakuta kuku kama 3 wamekufa,nikiwafungulia wakiwa kujitafutia chakula mitaani wengine wanaanguka ghafula hukohuko nakufa.Hawaharishi kinyesi chao ni kigumu isipokuwa nilipofanya uchunguzi kuna kuku mmoja ametoa kinyesi chenye rangi ya kijani japo kuwa ni kigumu kama cha kuku wengine.Kwa maelezo haya ninaomba munisaidie namna ya kufanya au tiba ya kuwapa ili niweze kuokoa kuku wangu.