Unakosea, haimaanishi kama mimi ninamiliki mabasi yangu sasa nimekuwa mbunge niyaache ama niachane na biashara hiyo, si kweli hata kidogo, ni kwamba kwa vile wewe unaingia siasani, zile biashara zako unakabidhi waendeshaji wengine (Delegates) kwa mfano kama wewe ni Managing Director na unatakiwa ofisini kila siku, unamwajiri mwingine, unabaki kupata ripoti ya kampuni yako na unaendelea kutinga mjengoni, jamani unataka kusema Obama, Bushi, Clintoni wanakaa tu kusubiri mshahara wa White house? Wewe si hivyo. Hata wewe kama una ndoto za siasa endelea tu na hizo biashara zako ipo siku ukiingia utakabidhi watu nawe unakuwa msimamizi wa mbali huku unatumikia Taifa.
Marufuku kusukumia dili katika kampuni yako, ila unaruhusiwa kuomba tenda kama wenzako kwa ushindani wa kawaida na ukubali kupata ama kukosa tenda!!
Nikosolewe kama siko sahihi.