watabiri wa haliyahewa hawa!

mzee wa upako alisema hakuna mafuriko wala mvua, daily naona mawingu yanajikusanya manyunyu kidogo halafu upepo kwa sana, mawingu yote yanatawanyika jua hiloo hakuna cha mvua wala radi siku zaenda tu
 
wamesema mawingu ya mvua yame kata kona kuelekea kwingine eti upepo umepiga ukayahamisha, si tupige makofi kwa hilo jamani!
 
juzi mtabiri wa hali ya hewa channel ten anasema mvua imenyesha baharini baada ya mgandamizo wa hali ya hewa kuwa wa joto baharini na kusababisha mvua kunyeshwa kwa bahari, tehe tehe nikaona utabiri umekataa lkn si jambo la ajabu coz mara nyingi huwa naona cnn vile vimbunga vinabadili direction huku ikiacha wakazi wa eneo walilojiandaa kwa dhahma wakishangilia, tusiwabeze sana yanatokea sana kwa wenzetu
 
kwetu Bongo hii mambo naona bado hatuwezi,wenzetu hutabiri hadi saa na dakika....
 
juzi mtabiri wa hali ya hewa channel ten anasema mvua imenyesha baharini baada ya mgandamizo wa hali ya hewa kuwa wa joto baharini na kusababisha mvua kunyeshwa kwa bahari, tehe tehe nikaona utabiri umekataa lkn si jambo la ajabu coz mara nyingi huwa naona cnn vile vimbunga vinabadili direction huku ikiacha wakazi wa eneo walilojiandaa kwa dhahma wakishangilia, tusiwabeze sana yanatokea sana kwa wenzetu

Ni kweli tusiwabeze na tumshukuru Mungu. maana mvua ikinyesha Dasilama huwa ni disaster na mtafutano.
 
baada ya ile ya December 20/21 2011 walionya kuwa iliyokuwa inafuatia ilikuwa funga kazi mpaka leo sijaiona mbali na mabwawa kukauka.
Sasa hii ya juzi nilikiwa pia nasikilizia kwa hamu sana lakini sijasikia wakisema zaidi ya manyunyu.
Sawa ni utabiri lakini wenzetu utabiri wao unakuwa precise kwa karibia 80% sio huu wa kwetu ambao ni precise kwa 15% tu
 
Hiyo ndio Bongo TZ,kila kitu ni kuchakachua mada hii inanikumbusha siku niliyonunua mbegu za vitunguu nitengeneze bustani nyumbani kwangu lakini yakaota majani..
 
Hivi tunaelewa maana ya utabiri?
Utabiri sio unabii jamani, unaweza kukamilia au usikamilike. Tunaposema tabiri matokeo ya mechi ushinde SAMSUNG Galaxy haimaanishi kuwa unachokitabiri ndio kitajiri.
Tuwape break TMA wakuu, pia tufahamu kuwa hawako kufanya battle na whoever, bali kusema wanachokiona kwa vyombo vyao na kuwapa tahadhari inapobidi.
 
zitakuja tu just wait na vile sie twaishi kwa hope ....so lets hope
 
Back
Top Bottom