Watabiri huwa wanatumia nini kutabiri...?

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,115
2,815
Kuna hawa watu ambao wanatoa tabiri mbalimbali juu ya mambo mengi ya mbele, muda mwingine huwa wanapatia kabisa japo huwa kuna malalamiko kuwa muda mwingine huwa ni uwongo. Sasa nataka kujua hawa watabiri huwa wanatumia uwezo gani kujua mambo yatakayotokea mbeleni??
 
Hao wanaojiita au kuitwa watabiri au wengine huwaita makuhani,shughuli zao hizi za 'utabiri' zina mchango mkubwa wa MASHETANI YA KIJINI.Majini wana uwezo wa kuruka na kwenda umbali mreefu na kurudi kwa muda mfupi mno.Kwa uwezo huu huwa wanakwenda karibu na mbingu ya kwanza kusikiliza mazungumzo ya malaika juu ya kitakachojiri siku za usoni kadri wanavyojulishwa na Mwenyezi Mungu.Wakishazinasa habari huwaletea 'watumwa' wao zikiwa zimeshatiwa na uongo kibao na mara chache sana yanayotabiriwa huwa kweli.
Pili,hakuna kiumbe yeyote mbinguni na ardhini ajuae yaliyojificha ISIPOKUA MWENYEZI MUNGU.Usidanganyike na hawa watabiri ;wote hao ni watumishi wa SHETANI na WANAKUFURU kwa kujivika joho M/MUNGU.
 
Utabiri unafanyika kwa crstal ball,astrology,palmistry,tarot cards, halafu ksma unafanya astral travelling,ukienda kwenye Hall of Memories utaeezakuiona akashic record na record of probabilities.Katika Akashic unaona mambo yaliyopita since the beginning of time. Katika record of probabilitied you see the future,from now until 3000 years into the future. Hii dunia ni physical plane,baada ya hapo ipo astral plane,baada ya hapo ipo brahma plane. Csll it whatever name you like,the plane above the astral plane,wanapokwenda watu wanapokufa,hapo ndipo ilpo hall of memories. Kwa maana hiyo,ukikutana na roho ya mtu aliyekufa,anaweza kukuambia something that will happen in the future.Unaweza kutabiri kwa kuingia katika kufikiria record of possibilities kuona kama vita inaweza kutokea.
 
Hv haya wanasomea wap haya? Dunia ina mengi hii. Yani humu jamii forums hata ukiuliza utakufa Lin watakuja watu kukujib.
 
Utabiri unafanyika kwa crstal ball,astrology,palmistry,tarot cards, halafu ksma unafanya astral travelling,ukienda kwenye Hall of Memories utaeezakuiona akashic record na record of probabilities.Katika Akashic unaona mambo yaliyopita since the beginning of time. Katika record of probabilitied you see the future,from now until 3000 years into the future. Hii dunia ni physical plane,baada ya hapo ipo astral plane,baada ya hapo ipo brahma plane. Csll it whatever name you like,the plane above the astral plane,wanapokwenda watu wanapokufa,hapo ndipo ilpo hall of memories. Kwa maana hiyo,ukikutana na roho ya mtu aliyekufa,anaweza kukuambia something that will happen in the future.Unaweza kutabiri kwa kuingia katika kufikiria record of possibilities kuona kama vita inaweza kutokea.
 
biblia mguu mmoja quran mwingine, maziwa kwenye bakuli kubwa, chooni kwa mkao wa kukata gogo. manuio kadhaa kisha matokeo yanaonekana kwenye maziwa.

shirk!, usipendelee hata kusikiliza upuuzi wao.
 
",the plane above the astral plane,wanapokwenda watu wanapokufa,hapo ndipo ilpo hall of memories.".
hapa pamenifanya nifikirie saaana bila majibu...sasa uko kwenye plane above astral plane unafikajefikaje jamani,na iyo roho ya mfu unaionaje mpk ukapata na muda kabisa wa kuongea nayo,na ilhali tunaambiwa ukishakufa roho zinazibitiwa na Mungu mwenyw na kama ni mtu mbaya/mtenda dhambi ni mwendo wa kichapo tu chini ya ulinzi mkali wa malaika.
mh,ila na sie binadamu kwa kufukunyuafukunyua,mwisho ukutane na yasiyokuridhi...mengine ni ghaibu jamani.
 
Kuna hawa watu ambao wanatoa tabiri mbalimbali juu ya mambo mengi ya mbele, muda mwingine huwa wanapatia kabisa japo huwa kuna malalamiko kuwa muda mwingine huwa ni uwongo. Sasa nataka kujua hawa watabiri huwa wanatumia uwezo gani kujua mambo yatakayotokea mbeleni??
Nionavyo mimi, watabiri huwa Wanatumia mapepo ya utambuzi Ambayo ni mashetani katika ulimwengu wa Roho.

Ambayo huwaeleza kile yanaenda kufanya. Kwa mwaka mzima ama miaka.

Tangu ancient civilizations walikua wakifanya hivyo.

Ila ikitokea watabiri wamekosea kutabiri ama matokeo yamekwenda ndivyo sivyo ni kutokana na nguvu ya MUNgU, ime interrupt mipango yao.
Nguvu hii ipo katika ulimwengu wa Roho, nguvu hii mapepo hawawezi kuitabiria( anticipate) . inatokana na wanaomwomba MUNgU wa KWELI. kuna watu huombea wengine, huombea dunia, taifa, wagonjwa. Wafanyakazi, ndugu, jamaa, marafiki, viongozi, nk.

Maombi ndio njia pekee ya kuvuta nguvu ya mungu. Na nguvu ya mungu ni contrary na nguvu zA mapepo. Nguvu ya mungu inakawaida ya kuvuruga mipango ya kishetani iwe ya wiki, miezi, mwaka , miaka hata siku. Hapo Ndipo utabiri wa kipepo unapokwama.
 
Ninapenda nichangie kwa namna ninavyofahamu. Watabiri wamegawanyika katika makundi mawili, ambayo ni; wale wanaotumiwa na Mungu, na wale wanaotumiwa na roho chafu za giza (mapepo au majini).

Kwa mujibu wa Biblia tunaona ya kwamba watabiri (wanaotumiwa na Mungu) walijulikana na wanajulikana kama "manabii." Hawa walitumiwa na Mungu ili kuwapasha watu habari za mambo yaliyopo (forthtelling) na yale yajayo (foretelling). Hii ni kwa sababu maisha ya mwanadamu tangu kuumbwa kwa ulimwengu yapo wazi mbele za Mungu, yaani Mungu anajua yote juu ya ulimwengu huu na hata yale yajayo. Ushahidi huu upo kwenye maandiko kama vile:

"Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake" (Amosi 3:7).

"BWANA, mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni" (Isaya 45:11).

Hivyo manabii walitabiri kwa msaada wa Mungu wa mbinguni. Wakati huu tulionao wale wanaotabiri wanasaidiwa na kuongozwa na Roho Mtakatifu aliyemo ndani yao. Na hapa ni kwa wale wanaomuamini Yesu Kristo pekee maana Neno la Mungu linasema:

"Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mabo yajayo atawapasha habari yake" (Yohana 16:13).

Kwa upande wa wale wanaotumiwa na roho chafu za giza (majini au mapepo), hawa wanaongozwa na roho hizo ili kuweza kutabiri mambo mbalimbali katika maisha ya mwanadamu. Hizi hujulikana kama roho za utambuzi (mapepo ya utambuzi) ambayo huweza kusoma nyota ya mtu na mwelekeo wa hatma ya mtu na hivyo kuwapasha habari mawakala wao yaani wapiga ramli na watabiri hao.

"Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua (Matendo ya Mitume 16:16)".

Hivyo ndivyo watabiri wanavyoweza kutabiri kwa habari za mambo yaliyopo na hata yale yajayo pia. Yote katika yote ni bora kumwamini na kumtegemea Mungu na si waganga wa kienyeji, wasoma nyota, wapiga falaki, na wengineo wafanyao mambo yafananayo na hayo.
Nawasilisha.
 
Kama kuna mtaalam wa kutabiri hapa Jf ajitokeze aniangalizie nyota yangu na ni biashara gani inaendana nayo maana naona nazeeka maskini.
NDugu yangu Muumba hajaumba kiumbe chake kije kuishi kwa masosoneko na unyonge,hiyo ni hali ambyo unaikubali mwenyewe ya kukata tamaa,jaribu kuweka Imani kwake na pia bidii ongeza,Ktk shughuli zako,chukua mfano mama tibanjuka,alitegemea kama angeenda sokoni kununua mboga na bilioni kwenye kapu?.
 
Back
Top Bottom