Wataalamu wa sheria, nisaidieni

Wataalamu wa sheria, nisaidieni

Mawakili wa serikali na wenyewe watatoa mapendekezo yao ya kisheria ya kutaka mahakama imtie hatiani Lissu! Wakimaliza mahakama kwa kupokea maelekezo kutoka juu, watatoa hukumu ya kifungo kwa Lissu. Ni mahakama ya rufaa pekee ndiyo itakayomfutia hayo mashtaka baada ya kukata rufaa.

NB: Ikitokea ukahitaji wakili msomi wa kukusaidia kuitafsiri PGO au Committal Proceeding, nipo hapa.
 
Ndugu zangu wataalamu wa sheria au hata yeyote mwenye ufahamu, naomba kujua, baada ya Lissu kuhitimisha Final Submission, utaratibu gani unafuata?

..mawakili wa serikali au upande wa mashtaka nao watafanya final submission wakikazia hoja kwamba Lissu ana hatia na anastahili hukumu ya kifo.

..baada ya hapo Majaji watapanga siku watakayotoa hukumu yao.

..kulingana na hukumu kila upande utakuwa na haki ya kukata Rufaa.
 
Kinachofuata ni upande wa mashitaka na wao kufanya submission ya hoja zao, kwanini Lissu anahatia. Kwa kuwa uhaini kwenye penal code hauna adhabu mbadala. Hoja zao zitajielekeza kueleza mahakama kuwa Lissu anahatia, hivyo ahukumiwe kunyongwa mpaka kufa.

Ingekuwa kosa la uhaini lina adhabu mbadala au adhabu mbili, au adhabu kulingana na mahakama inavyoona inafaa. Basi kesho ungesikia upande wa mashitaka ukipendekeza adhabu. Lakini kesho hakutakuwa na pendekezo la adhabu sababu ya kosa hilo kuwa na adhabu moja tuu. KUNYONGWA MPAKA KUFA.

TURUDI KWENYE SWALI: Baada ya upande wa mashitaka kuwasilisha submission yao; kinachofuata hapo kwa kesi kama hii, sio hukumu bali; ni majaji kutangaza kumluta na hatia mshitakiwa, kulingana na ushahidi uliowasilishwa.

Kama mahakama itamkuta Lissu anahatia, wanaweza kupanga tarehe ya hukumu hasa kwa kesi kubwa hizi za mahakama kuu.
Hii inaitwa "Mitigation". Kesi kubwa kama hizi; zinafiata utaratibu huo.

MAONI YANGU: Kwa ushahidi uliowasilishwa mpaka sasa, kama majaji hao hawana maelekezo. Lissu hawezi hukumiwa kifo, ataachiwa bila masharti.
Kuna udhaifu (matundu/matobo) mengi sana katika kesi hii. Haya ni maoni yangu, yasichukuliwe kama ni maoni ya kila mtu.
 
Mawakili wa serikali na wenyewe watatoa mapendekezo yao ya kisheria ya kutaka mahakama imtie hatiani Lissu! Wakimaliza mahakama kwa kupokea maelekezo kutoka juu, watatoa hukumu ya kifungo kwa Lissu. Ni mahakama ya rufaa pekee ndiyo itakayomfutia hayo mashtaka baada ya kukata rufaa.

NB: Ikitokea ukahitaji wakili msomi wa kukusaidia kuitafsiri PGO au Committal Proceeding, nipo hapa.
mbona kama umesha-conclude atafungwa! mnakuja na matokeo yenu mfukoni?
 
Ndugu zangu wataalamu wa sheria au hata yeyote mwenye ufahamu, naomba kujua, baada ya Lissu kuhitimisha Final Submission, utaratibu gani unafuata?
Baada ya Final Submission Majaji huzisoma na Wataandika hukumu ikishakalimilika Final submission kuna uhakika wa kurudi na tarehe ya Hukumu.
 
Back
Top Bottom