Wataalamu wa saikolojia tunaomba mtusaidie

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,407
Kuna hiki kitu kinaonekana cha kawaida na kimezoeleka na mtu sio rahisi kutokukifanya au kuki avoid. Lakini ukijaribu kukifikiria sana (deep thought) unagundua kuwa ni kitu cha ajabu sana na ukienda mbali sana kufikiria unaweza ona huwa unafanya 'utoto' lakini ndio hivyo kinatokea beyond our control. Nina uhakika asilimia 99.999% ya watu wote wanakifanya. Ningependa kujifunza kutoka kwa wanasaikolojia, hiki au hali hii inasababishwa na nini?

1. Unakuwa umekaa unachat na mtu kwa msg. Mara yule mtu ataandika kitu cha kukufurahisha na kukuchekesha sana. Huku nje katika uhalisia wako kama binadamu utakuwa unacheka kwa sauti hadi jirani zako watakushangaa. Lakini cha ajabu ushacheka sana halfu unachukua simu yako unaendelea kuchati unaandika 'hahahahahahahaha'.

Hoja yangu ni kwamba, ile natural force ya kuandika 'hahahaha' wakati tayari huku nje kwenye uhalisia wako umeshacheka inatoka wapi? kwanini ni vigumu kwa 99.99% ya watu kuendelea kuchat bila kuandika hivyo 'hahahaha'. Automatically tu mtu unajikuta umetype.

Binafsi naamini kuna kitu kwenye saikolojia na nipo tayari kujifunza.

karibuni.​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom