Wataalamu wa Mobile App development, mkuje mnisaidie mwenzenu

Baba Rhobi

JF-Expert Member
Nov 4, 2020
1,328
2,241
Wakuu mimi ni beginner kwenye hizo mambo za app development, nilipanga kujifunza app development, ila nikapata ushauri nijifunze web development (Front end) kwanza, nina endelea nayo, kwa sasa namalizia CSS, ni ingie Javascript.

Nika amua niweke sawa mazingira kabla ya kuanza ndo nikadownload Visual Studio code (ambayo naitumia pia kwa web development), kwa ajili ya kuja kujifunzia Flutter, sasa nikagundua ili niweze ku debug android app lazima niweze kuinstall Android SDK.

Hapo ndo mtiti ulipo, nimehangaika kuitafuta hiyo SDK kwa muda sasa ila sijaipata, niliyopata ni sdk tools, pamoja na platforms tools na command line tools, ambazo zote nimejaribu kiziweka kwenye android studio zimegoma, nimejaribu kuchange environment variables na zikawa sawa lakini wapi,

sasa naombeni wakuu msaada hapa namna ya

i- Kuinstall Android SDK (Ikiwezekana download link yake kabisa)
ii- Roadmap ya kujifunza app development. (Lengo langu ni kuweza kutengeneza software kwenye windows na Android itakayotumika kwenye presentation za ibadani kanisani.
(N.B) Hii nafanya kama Hobby na si kwa ajili ya kuja kujipatia kipato au vinginevyo.
 
Android sdk una download pale pale kwenye android studio. Pamoja na emulator yake

20230830_142052.jpg

20230830_142134.jpg
 
ii. Road maps za kujifunza Mobile App Development zipo nyingi.

Umesema unataka ujifunze kutengeneza Apps kwa Flutter. Basi anza kujifunza language ya dart then uingie kwenye Flutter.

Ila hapo ulipo upo kwenye njia sahihi sana maana ukianza na web development.. ukapata fundamentals za designing kwa css basi itakuwa rahisi kutengeneza UI's kwa Flutter.

Usisahau kujifunza kudesign apps na web kwa Figma itakujenga kwenye kutengeneza apps zenye mionekano mizuri.

Pia endelea kuchapa javascript mpaka uwe comfortable nayo then ukihamia kwenye dart, itakuwa rahisi sana kujifunza mana programming languages zote zinafanana concept.

Kwa ufupi, Upo kwenye njia sahihi.. Keep going
 
nashauri uwe na bando kubwa la speed nzuri unaposhusha sdk na tools nyinginezo
Mkuu hapo ndipo nataka niwakwepe kama inawezekana,wamenipiga sana, nkataka kama inawezekana nidownload pengine, let's say nichukie from browser then nii configure mwenyewe, sijui inawezekana.
 
Nakazia hapo kwenye bundle kubwa na speed,,la si hivyo atawalaani Google
Mkuu juzi hapa bundle la kama 15 hivi lilikata na sikufanikiwa chochote, ndo maana natafuta kama naweza pata ni downloadie pembeni then nika i configure mwenyewe.
 
ii. Road maps za kujifunza Mobile App Development zipo nyingi.

Umesema unataka ujifunze kutengeneza Apps kwa Flutter. Basi anza kujifunza language ya dart then uingie kwenye Flutter.

Ila hapo ulipo upo kwenye njia sahihi sana maana ukianza na web development.. ukapata fundamentals za designing kwa css basi itakuwa rahisi kutengeneza UI's kwa Flutter.

Usisahau kujifunza kudesign apps na web kwa Figma itakujenga kwenye kutengeneza apps zenye mionekano mizuri.

Pia endelea kuchapa javascript mpaka uwe comfortable nayo then ukihamia kwenye dart, itakuwa rahisi sana kujifunza mana programming languages zote zinafanana concept.

Kwa ufupi, Upo kwenye njia sahihi.. Keep going
Nashukuru sana mkuu.
 
Mkuu hapo ndipo nataka niwakwepe kama inawezekana,wamenipiga sana, nkataka kama inawezekana nidownload pengine, let's say nichukie from browser then nii configure mwenyewe, sijui inawezekana.
zile tools zinatoka kwa repos zao zilizo github, wakati yanashuka wanaonesha kabisa na links zao, kuyashusha manually toka kwa browser naona ni yale yale tu

ukubwa wa bando na speed hasa kwa siku chache za mwanzo, siku za mbele ni MBs kadhaa kwa ajili ya gradle building
 
Android sdk una download pale pale kwenye android studio. Pamoja na emulator yake

View attachment 2733522

View attachment 2733524
Mkuu hii njia labda uwe na unlimited data plan tena yenye kasi ya kimbunga, imenitesa sana na kuishia kuharibu pesa bure, hivi siwezi pata alternative labda nidownload hizo images let's say android 13,12 na 10 only na file zingine pembeni separately.
 
zile tools zinatoka kwa repos zao zilizo github, wakati yanashuka wanaonesha kabisa na links zao, kuyashusha manually toka kwa browser naona ni yale yale tu

ukubwa wa bando na speed hasa kwa siku chache za mwanzo, siku za mbele ni MBs kadhaa kwa ajili ya gradle building
Mkuu kwa mfano nikifanikiwa kuyashusha moja moja kwa browser, yatakubali kuingia hapo kweli.
Na vipi nipitie wapi kufanikisha hilo.
 
Mkuu kwa mfano nikifanikiwa kuyashusha moja moja kwa browser, yatakubali kuingia hapo kweli.
Na vipi nipitie wapi kufanikisha hilo.
yanakubali, issue sikumbuki links zake, nakumbuka tu yana dl.blah blah
ukianza shusha file mojawapo utaona links husika na unaweza cancel, kisha ukazifuata kwa browser

lakini sioni kwanini ufanye ivyo maana ukiyashusha toka kwa sdk manager, setup files ( pamoja na izo emulator images ulizochagua ) zinatupiwa somewhere kwenye C:\Users\user_name\AppData\Local\Android Studio Folder kisha yanakuwa installed automatically

mda mrefu kidogo siwezi kumbuka vizuri
 
Back
Top Bottom