My Favorite Stacks for Web, Mobile, Desktop &DAPP App development

kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
1,996
5,054
Hello world...

Kwenye dunia ya technology hasa hasa computer programming chaguo sahihi la technologies za kutumia ili kutatua tatizo au kutengeneza kitu fln ni muhimu sana.

Kufanya chaguo hilo kunategemea na skillset ya engineer anaehusika na pia environment ambapo product hio ita-run

Leo napenda kushare stack nnazozitumia kwenye kazi zangu mbalimbali za programming kwa sababu naamini kuna beginners watanufaika na au hata professionals wanaweza kudiscuss na aidha kuadapt hz stack au kufanya mm niadapt suggestion zao. Twende moja kwa moja kwenye mada....

NOTE: Simple things should be done in simple ways

1)WEB & WEB BASED SYSTEMS DEVELOPMENT
Hapa kama ni simple to medium Web system projects huwa natumia ReactJS kwenye front end na php kwenye backend. Ukitokea ulazima sana* ntatumia framework hasahasa laravel. Lkn mara nyingi napendelea kuandika APIs zangu from scratch coz inanipa overall control japo najua inakuja na gharama yake ila inakua ndani ya uwezo wangu.

Kama ni plain content based system eg Blog au News based site huwa natumia WordPress kisha naandika themes na plugins ili kukidhi matakwa yangu na ya mteja endapo kuna ulazima huo. Pia kama mtu anataka simple ecommerce web na bajeti yake sio kubwa sana huwa natumia WooCommerce then naiextend kwa plugins zangu kama hapo kwenye WordPress

2)MOBILE APP (ANDROID)
Kabla ya kuendelea nikubali kwanza napenda android dev ya java coz inakupa real flavor ya AndroidOS na mechanics za lifecycle nzima ya app ambayo ndio kiini cha matumizi ya hio OS. Kama unataka kuielewa kweli AndroidOS basi code Apps in Java. Hivyo stack yangu kwenye hii part inaweza kuwa biased na hio issue.

Kwa simple Apps zisizohitaji Native support kwa wingi natumia React Native. Kwa apps zinazohitaji native support kwa wingi huwa natumia Java na XML kwenye styling.

Ofcourse kotlin na flutter zinakuja kwa kasi lakini bado napendelea Java kwenye android development.

3)DESKTOP APP DEVELOPMENT.
Hapa inategemea kutokana na categories zifuatazo

a)Kama app ni client tu kwa ajili ya webbased system huwa natumia ElectronJS framework. Hapo ntatumia CSS, React na NodeJS

b)Kama app inahitaji local database mfano labda ni business management software huwa natumia stack hiohio kama hapo kwenye (a) lakini database natumia IndexedDb ambayo ipo available kwenye kila browser. Nmeongelea browser coz ElectronJS kiukweli ni browser environment kwa ajili ya desktop app yako, so features zote ambazo ungezipata kwenye browser unazipata pia kwenye ElectronJS. Tofauti ya electron na browser ni kwamba inakupa native access kwenye Operating system kupitia NodeJS integration. So unaweza tengeneza hata adobe photoshop yako kwa kutumia browser based technologies. Na ndio maana ni chaguo kwa desktop apps nyingi kwa sasa ikiwemo Atom IDE.

IndexedDb yenyewe kama yenyewe ni ngumu sana kuitumia so mara nyingi natumia Lovefield.js kama wrapper, lovefield pia inatumiwa na Gmail web version kutunza local data kama opened emails etc.... Tutorials zake ni chache sana lkn inakupa MySql-like database kwenye browser so kuitumia inabidi uwe na tabia ya kusoma directly documentaion husika kwanza. Japo it worth it coz performance yake ni nzr na ina queries zinazoendana na SQL

4)DAPPS (BLOCKCHAIN BASED APPS)
Hapa kuna truffleJS, solidity (kuandika contracts) na front end huwa natumia ReactJs pamoja na bootstrap. Kwa kuwa dapps zote nlizoandika bado hazijawa deployed kwa ajili ya production na kuwa na real user base basi siwezi toa comment khs perfomance na efficiency ya hii stack kwa app inayopaswa kuwepo kwenye market. Japo kwa nisikiavyo hio ndio popular stack kwa sasa kwenye ulimwengu wa Dapps

Conclusion:
Japo market ya tech kwa Tanzania bado ina changamoto ila kama mtu anatafuta beginner guide ya ajifunze stack zipi basi anaweza tumia hio hapo juu kwa kuanzia na kuwa anamodify kadiri anavyopata uzoefu. Mfano ukitumia sana ReactJS utakuja kuona uhitaji wa NextJS kutokana na requirements na mazingira.

Peace
~Kali Linux
 
Nimeipenda sana hii, hongera
 
Whole department in one person. 💪🏾
 
Kuna watu wanatafuta mtu wa kuwafanyia mobile na desktop app ya taasisi yao ya mambo ya Kiislam, waliniuliza mimi niwatafutie source.

Kama unaweza kuongea nao wapigie au whatsapp nifate pm.
 
Kwa sasa mimi kwenye web app nimejikita kwenye matumizi ya Joomla ambayo nimeitumia kwa kama miaka kumi hivi, japo kwa uzoefu nimetumia frameworks nyingi kulingana na pale mteja akisisitiza framework ipi nitumie, au lugha anayotaka yeye.

Kwenye desktop app huwa natumia Electron ya Javascript, naipenda kwa sababu inarahisisha pale nikihitaji hiyo code niihamishe kwenye web au mobile. Kwa kweli dunia imebadilika sana maana mimi ni mojawapo wa old school tuliokua tunatumia VB5/6 enzi zile.

Mobile app huwa natumia Ionic Javascript nikichanganya na Angular.

Kwa kifupi mimi huwa napenda kuwashauri madogo usihangaike sana na haya mambo ya frameworks, huwa zinakuja na kuondoka na kupoteza umaarufu, nimezitumia nyingi sana na baadhi nilikua nimewekeza nguvu nyingi sana ila zikaja kufa, nakumbuka nilivyokua nimejikita kwenye library ya Mootools halafu haipo tena yaani.
Hata library ya JQuery inaelekea kujifia maana Javascript yenyewe imeboreshwa sana kiasi cha kuwa na functionalities zilizokua zinatulazimu tutumie JQuery.

Muhimu sana kutia jitihada za kuelewa kwa undani teknolojia behind the framework, halafu pia tengeneza mfumo wako uwe framework agnostic, kwamba unaweza ukauhamisha kutoka framework moja kwenda nyingine bila usumbufu, kwa mfano jifunze Domain Driven Development, itakusaidia sana kufanya separation ya code yako na framework.
 
Mkuu framework Kama bootstrap mpaka leo hii hakuna framowork iliyotrend kwa upande wa kuresponsivika mfano foundation by zurb haitumiki sana unasemaje hapa
 
Kuna watu wanatafuta mtu wa kuwafanyia mobile na desktop app ya taasisi yao ya mambo ya Kiislam, waliniuliza mimi niwatafutie source.

Kama unaweza kuongea nao wapigie au whatsapp +255625249605
Hawa wanahitaji mwalimu kama sijakosea
 
Kwa kifupi mimi huwa napenda kuwashauri madogo usihangaike sana na haya mambo ya frameworks, huwa zinakuja na kuondoka na kupoteza umaarufu, nimezitumia nyingi sana na baadhi nilikua nimewekeza nguvu nyingi sana ila zikaja kufa, nakumbuka nilivyokua nimejikita kwenye library ya Mootools halafu haipo tena yaani.
Hata library ya JQuery inaelekea kujifia maana Javascript yenyewe imeboreshwa sana kiasi cha kuwa na functionalities zilizokua zinatulazimu tutumie JQuery.

Muhimu sana kutia jitihada za kuelewa kwa undani teknolojia behind the framework, halafu pia tengeneza mfumo wako uwe framework agnostic, kwamba unaweza ukauhamisha kutoka framework moja kwenda nyingine bila usumbufu, kwa mfano jifunze Domain Driven Development, itakusaidia sana kufanya separation ya code
Hii barua , with all due respect natamani imfikie kama ilivyo Mr Stephano Mtangoo

Umesema bonge moja la point. Mie kama hakuna ulazima wa framework huwa najitahidi sana kutumia core hasahasa upande wa php na java. Nani angepredict downfall ya jquery kpnd kile. Mie jquery nlidhan itaisha na mwisho wa dunia. Huo ni mfano tu.

Af hata hivyo nmekuja kuona bila kuwa na uelewa na core hautopata respect kwenye dev communities. Kuna project bila core hugusi utaishia kusema kila kitu ni ninja code kumbe huna concept
 
Mkuu framework Kama bootstrap mpaka leo hii hakuna framowork iliyotrend kwa upande wa kuresponsivika mfano foundation by zurb haitumiki sana unasemaje hapa

Sitosahau kilichonikuta baada ya kutengeneza systems nikitumia Boostrap 2 wakati ikiwa mpya, halafu baadaye wakaja kuachia verson 3 mara verson 4, ambazo hazikua backward compartible, nilihangaika kubadilisha code zangu parefu sana ili kufanikisha upgrade.
Naipenda Boostrap na pia sijakandia framework yoyote, kawaida frameworks huwa nzuri sana kwenye kurahisisha shughuli, maana mteja anahitaji mradi wake ndani ya muda mfupi na hayupo tayari kulipia gharama za kuupiga from scratch.
Lakini huwa nashauri sana wadau wajifunze technologies behind these frameworks, hata hii Boostrap leo hii inafukuziwa sana, kwanza native CSS yenyewe imeboreshwa mpaka kuna baadhi ya functionalities unatia tu line moja, wala hauhitaji framework yoyote.
Kama likija suala la responsiveness, hebu piga darasa la CSS grid, yaani native code na unapata responsivess.
 
Ushafuatilia kabla ya bootstrap alikuwepo nani? Anyway, ili kudumu kwenye game inahitaji uwe unajiupdate sana coz kila siku kuna vitu vipya. Ndo maana mwisho wa siku wale tu wanaoweza kumove na speed ndio wanakua successful
 
Sitosahau kilichonikuta baada ya kutengeneza systems nikitumia Boostrap 2 wakati ikiwa mpya, halafu baadaye wakaja kuachia verson 3 mara verson 4, ambazo hazikua backward compartible, nilihangaika kubadilisha code zangu parefu sana ili kufanikisha upgrade.
Naipenda Boostrap na pia sijakandia framework yoyote, kawaida frameworks huwa nzuri sana kwenye kurahisisha shughuli, maana mteja anahitaji mradi wake ndani ya muda mfupi na hayupo tayari kulipia gharama za kuupiga from scratch.
Lakini huwa nashauri sana wadau wajifunze technologies behind these frameworks, hata hii Boostrap leo hii inafukuziwa sana, kwanza native CSS yenyewe imeboreshwa mpaka kuna baadhi ya functionalities unatia tu line moja, wala hauhitaji framework yoyote.
Kama likija suala la responsiveness, hebu piga darasa la CSS grid, yaani native code na unapata responsivess.
Haya mambo kuna mashabiki wa frameworks humu wakisikia wanakuja kwa fujo balaa.
 
Nafikiri soko la ajira ndio sababu, watu wengi wanasema framework zina security, code base nzuri, pia ni simple kufanya maintenance.

Kuchwizzy na Stefano Mtangoo washa zungumza mambo kama hayo.

Ni ngumu kwa kampuni kubwa kutotumia framework japo inapendeza kujitengenezea framowork wenyewe.

Mfano kampuni x badala ya kutumia laravel basi waunde yao ila hapa kuna kazi nzito vipi wakiajiri new dev itabidi aisome na wakati kuna hizi public
 
Kama ukiweza, na jinsi nilishauri kwenye andiko langu hapo mwanzo, tengeeza system ambayo ni framework agnostic, maana kwamba business logics hazitegemei framework, tumia concept ya Domain Driven Dvelopment (DDD), na pia SOLID itakuchukua muda kuielewa ila ikikukaa, utashukuru sana.

DDD inakuewezesha uhamishe shughuli yako kutoka kwa Laravel kuja kwa Yii au framework yoyote bila mahangaiko, inakuwezesha kufanya upgrade ya framework yako bila kuvuruga business logics zako maana umezintenganisha na kuzilinda.
Pia inakuewezesha kubadilisha DBMS kama vile MYSQL kwenda hata MS SQL au Postgres bila shida, system yako inabaki wima licha ya misukosuko ya frameworks na vita vyao.

Kuna kipindi nilipoteza mradi wa hela ndefu kwenye taasisi moja ya kiserikali, yaani nimepiga mzigo ulioshikamana na kutegemea framework fulani, kisha taasisi ikaajiri vijana kutokea chuo ambao walikua wameiva Laravel, wakapiga siasa humo ndani kwamba system yangu iko based on old technology ambayo kwa maoni yao na ushauri kwa mabosi wa taasisi ni kuwa kwa vile sio Laravel, basi ni old technology.

Siasa kama hizi hauwezi kuziweza maana madogo kama hao huwa wamewekwa humo kwa connections za wakubwa, chochote wanachokisema kinachukuliwa kuwa kweli na ndio basi, ukizingatia wakurugenzi kwenye hizi taasisi hawajui mambo ya teknolojia.
Nililazimika kupoteza mradi, ila kama enzi hizo ningekua nimejilinda na concept ya DDD, mbona ningehamisha kwenda kwa Laravel na kuendelea kutafuna hela
 
Back
Top Bottom