Wataalamu wa gari ambazo ni automatic

Foundation

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
1,420
Reaction score
613
Wasaalam wakuu,

Kuna kiduara kwenye dash board kimeandikwa herufi ABS kinawaka wakati gari inatembea, nahisi kutakuwa na tatizo. Je tatizo hilo ni lipi?

Kwa kawaida kiduara hiki huwaka gari inapowashwa, na huzima baada ya gari kuwashwa.

Naombeni msaada wenu
 
Umenikumbusha tatizo hili kipindi nipo na Premio.Taa ya ABS iliwaka sana na hakuna gereji yoyote maeneo ninayishi iliweza kunisaidia.Mafundi waliinamisha na kutikisa vichwa vyao kwamba hawajui lolote.

Kipindi hicho sikuwa na kompyutailiyounganishwa kwenye mtandao wa internet.Ningegoogle na kupata suluhisho/ufahamu wa hilo tatizo.Leo nilipoona thread yako, just out of curiosity nikasema hebu nigoogle. Nimepata kitu hiki,pengine kitakufungua macho:
It means that the Anti lock Braking System has detected a fault and is now turned OFF.
Your brakes will still work normally but you won't have ABS in an emergency stop situation.
The most likely fault will be a wheel sensor or a wheel sensor connection.
 

1.brake pads/sensor zimeisha.
2.anti locking brake system ina matatizo.

HAINA UHUSIANO WOWOTE NA MANUAL OR AUTOMATIC

cc: OLESAIDIMU MANI CYBERTEQ
 
Last edited by a moderator:

Mkuu uko sahihi kabisa, sometimes hata brake pads zikiwa zimeisha hiyo taa huwa haizimi ajaribu kubadili Brake pads kwanza kama itaendelea basi hayo ya sensor na mfumo mzima wa ABS inabidi uchekiwe.
 

Mkuu kuna fundi aliniambia gari lina matatizo ya brake, nikamuuliza kivipi, hakunijibu. Nataka nifanye kasurvey kabla sijapeleka kwa mafundi, maana na wenyewe hawatabiriki
 
Sawa kabisa mkuu yangu inawaka taa ya kuonyesha kuna bulb imekufa lakini nimekagua zote nzima na zinawaka.cc OLESAIDIMU
Ningeanzia kujua kuwa kila bulb ina sensor inayotuma mawasiliano kwa central light controlling system labda sensor za balbu moja ina.shida hivyo haionekani kule???!!

Volkswagen kaka??!!!
 
Last edited by a moderator:
1.brake pads/sensor zimeisha.
2.anti locking brake system ina matatizo.

HAINA UHUSIANO WOWOTE NA MANUAL OR AUTOMATIC

cc: OLESAIDIMU MANI CYBERTEQ

Asante mkuu, kuna kamlio huwa nasikia tairi la kulia hasa nikikanyaga brake, vina uhusiano? Siku si nyingi nilimepelekea fundi, yeye akafungua tairi zote za mbele na kuanza kukagua bush na vitu vingine hakukuta tatizo
 
Last edited by a moderator:
Mkuu uko sahihi kabisa, sometimes hata brake pads zikiwa zimeisha hiyo taa huwa haizimi ajaribu kubadili Brake pads kwanza kama itaendelea basi hayo ya sensor na mfumo mzima wa ABS inabidi uchekiwe.

Brake pads zikiisha huwa kunatokea mlio ukikanyaga brake? Wanaziuzaje hizi brake pad kwa gari ndogo? Au inategemea na gari husiaka
 
Ningeanzia kujua kuwa kila bulb ina sensor inayotuma mawasiliano kwa central light controlling system labda sensor za balbu moja ina.shida hivyo haionekani kule???!!

Volkswagen kaka??!!!

Toyota crown.
 
Asante mkuu, kuna kamlio huwa nasikia tairi la kulia hasa nikikanyaga brake, vina uhusiano? Siku si nyingi nilimepelekea fundi, yeye akafungua tairi zote za mbele na kuanza kukagua bush na vitu vingine hakukuta tatizo

Pads zinashikwa na"vibati" sasa zikiisha au saa nyingine hiko kibati kikikaa upande kinaweza
kuwa kinagusa pasi (hub??!!) na kutoa scratching sound hiyo unayosikia!!!!

Ina suggest zaid kuwa tatizo ni pads!!!
 
Toyota crown.

Ok, nimewahi kukuta fundi anapasuka kichwa kwa hii issue ila ilikuwa volkswagen!!!!
Bado mi naona ni issue ya "particular bulb sensor" either distal or proximal end
 
kuna mambo mengi yanayopelekea ABS ijizime (hicho kitaa kikiwaka inamaana ABS iko off na unatumia brake kawaida), huenda kuna tatizo kwenye sensor, ukienda garage wakafanya diagnostic watakwambia for sure tatizo ni nini, meanwhile unachapia mwendo kama kawaida, sema kwenye mwendo mkali ni hatari, abs inasaidia tairi liendelee na mzunguko na kupungua kwa utaratibu maalum unapokanyaga brake ili gari isipoteze traction na kula msele (skid).
 
Ok, nimewahi kukuta fundi anapasuka kichwa kwa hii issue ila ilikuwa volkswagen!!!!
Bado mi naona ni issue ya "particular bulb sensor" either distal or proximal end

Kuna fundi mmoja amesema niweke za used maana nilibadili baada ya moja kuungua ilikuwa ni za breki.
 
Asante mkuu, kuna kamlio huwa nasikia tairi la kulia hasa nikikanyaga brake, vina uhusiano? Siku si nyingi nilimepelekea fundi, yeye akafungua tairi zote za mbele na kuanza kukagua bush na vitu vingine hakukuta tatizo

nenda kwa fundi mu-instruct akague brake pads zote.
 
Pads zinashikwa na"vibati" sasa zikiisha au saa nyingine hiko kibati kikikaa upande kinaweza
kuwa kinagusa pasi (hub??!!) na kutoa scratching sound hiyo unayosikia!!!!

Ina suggest zaid kuwa tatizo ni pads!!!

Mkuu nashukuru
 
Brake pads zikiisha huwa kunatokea mlio ukikanyaga brake? Wanaziuzaje hizi brake pad kwa gari ndogo? Au inategemea na gari husiaka

zikiisha sana hata ukikanyaga brake unahisi mkwaruzo.....ila zikianza kuisha hio taa huwa inawaka as a warning...nashauri kazikague....bei inategemea na gari hizi za toyotas very cheap
 

Mkuu nashukuru kwa ushauri wako, hili tatizo limetokea jumapili iliyopita natoka boko nakuja maeneo ya ubungo, tena ilikuwa saa 4 usiku, na barabara inavyoita usiku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…