Wataalamu wa Computer

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
11,644
Reaction score
14,803
Mzigo jamaa anataka million 1.3.

Wataalam nipeni uchambuzi kabla ya kuzama mfukoni.

 
Touch Ina miss maana yake hio ni ya kizamani ingawa specifications zake sio mbaya sema bei amekuwekea juu sana
 
Ingekua mpya sawa ila used hio bei hapana mpeleke mpaka lak 7
 
Unanunua ist kwani? hiyo pesa nyingi Tena Sanaa kununua Hilo plastic.
Mwambie kinaga ubaga kuwa anakupiga
 
Nenda sehemu ya ku search hapo kweye toolbar kisha andika haya maneno ndani ya mabano (DXDIAG) kisha search itakuletea software yenye jina hilo ifungue halafu chagua option imeandikwa ( render ) au video 2 kisha piga picha halafu utume hapa
 
Bei nzuri kama bdo iko na muenekno mnzuri na QUALITY
ila mshuahe kidogo mpk kwenye m1 au 9 ila akikomaa hata 1.2 sio mbaya
 
Umeitest inafaa kwa kazi zako?
Hizo specs zisikudanganye, itest kwanza..kuna i7 nyingine unaweza dhani ni pentium...
 
Nadhani itakuwa latitude 7420 ya mwaka 2021 (sina uhakika) ambayo Amazon kwasasa wanaweza kuwa wanaiuza $500 hadi $600 kwa used na 700 hadi 750 kwa mpya.

-Kama battery bado iko vizuri
-Bado inao Muonekano mzuri
-Umeitest hardware zake zinafanya kazi vizuri

-Inakidhi Mahitaji yako ya sasa na ya badae angalau miaka miwili ijayo

Nashauri uinunue kati ya 850,000 hadi 1,000,000
 
Not worth it kwa gen ya 11. Kuna machine za Ryzen 5500U Hadi 850,000 unapata ambazo ni nzuri kidogo kushinda hio. Kwa hio budget Bora utafute gen ya 12.

Kwa 1.3 gen ya 11 labda iwe na dedicated GPU nzuri.
 
Not worth it kwa gen ya 11. Kuna machine za Ryzen 5500U Hadi 850,000 unapata ambazo ni nzuri kidogo kushinda hio. Kwa hio budget Bora utafute gen ya 12.

Kwa 1.3 gen ya 11 labda iwe na dedicated GPU nzuri.
Nadhani unatofautisha bei za laptop kkoo na za kuagiza
Kwa hiyo Kwa bei za kkoo Bado bei nzuri

Ila kama ataamuua kuagiza mwenyewe atapata nzuri zaidi ya hiyo
Labda tumuulize ananunua KKOO ama amemuagiza mtu nje
Au ananunua Kwa mtu hapahaoa kama SECOND HAND kutoka Kwa ndugu jamaa na marafiki
 
Kuagiza unapata Chini ya hapo mkuu, naongelea Bei za kkoo.

Mfano hii gen ya 12 ni i3 sema ina nguvu kushinda hio i7 Cpu ila GPU imepitwa kidogo, overall performance wise ipo vyema zaidi. Unaweza kuidharau sababu ni i3, hapo unaongeza tu ram na ssd una machine ya maana.



Na hii Ryzen 5800U ina core 8 thread 16 kazi zinazohitaji thread nyingi kama video editing, rendering na mambo yafananiayo Ina nguvu 30-80% compare na i7 gen ya 11


Kifupi mkuu Makampuni makubwa yanatumia Laptop na desktop miaka 3 tu, warranty iliisha wanauza Bei rahisi zinakuja mitumba huku Africa,
 
nimepitia baadhi ya forums nimeona ina heat sana, jaribu kuitumia masaa mawili ucheki kama ina heat usije uziwa mbuzi kwenye gunia.

Ila kibongo bongo napenda kutumia laptops zenye upatikanaji rahisi wa spare nazipenda HP japo lenovo unaweza usimjue fundi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…