Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,480
- 37,756
Habari inayobamba kwa sasa kuhusu Elimu yetu baada ya kutangazwa kwa matokeo ya darasa la 4, darasa la 7 na kidato cha 4 ni kuhusu mkoa wa Mtwara kuingiza shule 9 kati ya 10 kwenye orodha ya shule zilizofanya vibaya. Tayari Mkuu wa mkoa Mtwara na NECTA wametoa tamko kukanusha kwamba hayo siyo matokeo ya mwaka Jana bali ni ya miaka mitatu iliyopita. Yote kwa yote bado inabaki kuwa ni matokeo ya mkoa wa Mtwara ulioko mwambao wa Bahari ya Hindi.
Ukiondoa mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera na Mara inayopakana na mwambao wa Ziwa Victoria na Mbeya (Kyela) wanaopakana na ziwa Nyasa waliobaki hususani wanaopakana na Bahari ya Hindi yaani mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es salaam, Lindi na Mtwara, ile inayopakana na Ziwa Tanganyika yaani Kigoma na Rukwa mwamko wao wa kielimu uko chini sana na matokeo yao ya mitihani kila mwaka yako chini (Tazama matokeo ya Kigoma mwaka Jana) na wenyeji wanaona kama haliwahusu.
Sasa wito wangu ni kwa wataalamu na humu JF naamini mmo wataalamu wa kada mbali mbali ikiwemo utafiti wa kielimu, naomba tuje na andiko la kwa nini maeneo niliyoyataja bado wanaona Elimu si kipaumbele? Zamani kidogo jamii za wafugaji nazo zilikuwa katika mwelekeo huu, lakini Leo Wamasai na Wasukuma ni miongoni mwa makabila yenye mwamko wa kielimu na watoto wao wanafanya vizuri.
Karibuni Kwa maoni na maboresho.