Wataalam wa kuandika wasifu tafadhali

Wataalam wa kuandika wasifu tafadhali

Mhakiki

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,389
Reaction score
2,118
Habari za mchana wanajamvi.

Kichwa cha habari hapo juu chajieleza.

Mwezi wa 10 mwaka huu mwizi wa siku nyingi ajulikanaye kwa jina CCM atazikwa rasmi.

Kutokana na msiba huo naomba mwenye utaalam wa kuandika wasifu wa MAREHEMU atusaidie kuuandika akizingatia vitu vifuatavyo:-

1.Tarehe aliyozaliwa marehemu.

2.Mahali alipozaliwa marehemu.

3.Nafasi alizowahi kutumikia marehemu.

4.Pengo aliloacha marehemu.

5.Marehemu ameacha wajane/ wagane wangapi?

Nawasilisha.
 
Kubwa ulilosahau ni deni la marehemu,aliowaachia Watanzania
 
Marehemu CCM alizaliwa 05/02/1977 Karikoo mtaa wa Lumumba akiwa mtoto wa pekee wa Mzee TANU na mama ASP.
Marehemu alipata elimu ya awali kupitia azimio la Arusha kabla ya kuja kufelishwa na azimio la Zanzibar.

Enzi za uhai wake chini Marehemu CCM alijihusisha na kuasisi mashirika ya uma na kupanda mazao ya biashara kwa ajili ya viwanda vya ndani ila baadaye baada ya kulikashifu azimio la Arusha akashindwa kuendeleza mazao.

Aidha marehemu aliua mazao ya biashara mfano pamba,korosho huku akidhoofisha viwanda vya ndani kama Tanganyika Packers.

Marehemu ameacha watoto kadhaa ambao hakuwapata kwenye ndoa halali,aidha marehemu kawaacha Wachina kariakoo,waarabu Loliondo,Makaburu Mererani,wamarekani Mtwara na wazungu wengine kila kona ya nchi wakijichimbia tu madini aina tofauti tofauti!

Marehemu ameacha Mume mmoja UKAWA na watoto wakuasili ACT na ADC. Israel aiweke roho ya Marehemu panapostahili!
 
Hahahaaaaa, umetisha hasa hapo kwenye mume.
 
Hahahahaaa... funny thread with funny replies...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom