Wataalam wa hesabu, nisaidieni

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,267
29,906
Msaada kwa wanaojua Mathematics

N:B mi nimeumiza kichwa nimeshindwa

34d6e0ec2b1027f93c4d6f0b11e6de55.jpg
 
Utapusuka kichwa bure ndugu yangu hizo ni namba witiri, kamwe huwezi jumlisha namba witiri katika idadi ya witiri na kupata jibu namba shufwa.
Namba witiri ni namba ambayo ukiigawanya kwa mbili hugawanyika na kubaki moja.

Shufwa ni namba ambayo ukiigawanya kwa mbili inaisha bila baki.

Tuchukue namba witiri kwa idadi ya namba witiri, tuchukue namba witiri tatu, 5,7,9. Hizi number kwa idadi ni tatu. Idadi ya tatu ni namba witiri.
5+7+9=21

Au tuchukue namba tano(idadi hii ni namba witiri)
1,3,5,7,9
1+3+5+7+9=25

Nimesema huwezi chukua namba witiri zenye idadi witiri ukazijumlish na jibu lake kuwa shufwa.
21 na 25 ni namba witiri.

Lakini chukua namba zenye idadi ya namba shufwa kwa mfano 1 na 3.hizi ni namba witiri mbili, mbili ni shufwa.
1+3=4
Namba witiri mbili, zenye idadi ya nmba shufwa zimetoa jibu witiri.

Kwa maelezo haya hilo swali halina jibu lenye namba nzima.
 
Swali walishaleta, kwa namna ya kawaida haiwezekani! Isipokuwa kwa kutumia factorial! Kama ulifanya PCM najua unanipata
 
Utapusuka kichwa bure ndugu yangu hizo ni namba witiri, kamwe huwezi jumlisha namba witiri katika idadi ya witiri na kupata jibu namba shufwa.
Namba witiri ni namba ambayo ukiigawanya kwa mbili hugawanyika na kubaki moja.

Shufwa ni namba ambayo ukiigawanya kwa mbili inaisha bila baki.

Tuchukue namba witiri kwa idadi ya namba witiri, tuchukue namba witiri tatu, 5,7,9. Hizi number kwa idadi ni tatu. Idadi ya tatu ni namba witiri.
5+7+9=21

Au tuchukue namba tano(idadi hii ni namba witiri)
1,3,5,7,9
1+3+5+7+9=25

Nimesema huwezi chukua namba witiri zenye idadi witiri ukazijumlish na jibu lake kuwa shufwa.
21 na 25 ni namba witiri.

Lakini chukua namba zenye idadi ya namba shufwa kwa mfano 1 na 3.hizi ni namba witiri mbili, mbili ni shufwa.
1+3=4
Namba witiri mbili, zenye idadi ya nmba shufwa zimetoa jibu witiri.

Kwa maelezo haya hilo swali halina jibu lenye namba nzima.
Chukua 9+8+13 =30, kweli vyeti fake ni jipu
 
Chukua 9+8+13 =30, kweli vyeti fake ni jipu
Hoja yako inesimamia wapi ndugu?

Kama ni jumla ya witiri ambazo idadi yake ni witiri haiwezi toa witiri kamwe.
Hizo nmba zako ni idadi witiri kweli, lakini namba zenyewe moja si witiri kati ya hizo, 8 ni shufwa na si witiri
 
(1+9) + 7 + 13 = 30
Umenikumbasha enzi zile nilikuwa najua jawabu la swali lakini njia kulifikia hilo jawabu siijui, so nilichukua namba zozote zile ambazo ukizidisha/gawanya/jumlisha/kutoa zitafikia jawabu langu..kama ulivyolazimisha hapo mkuu. Hahahh
 
Ulifanya hivi utakuwa umekiuka masharti ya hesabu au ni sawa
(15+3) +(15-3) +(3-3)=30
Maana 3 nimeijulisha na kuitoa ili kupata namba shufwa lkn pia kutoa logic kwa nini nimeitoa na juijumlisha ndio nikaongeza chumba cha (3-3).
 
Back
Top Bottom