Hii imekuja baada ya yule jamaa kusema anasafisha kucha kwa laki 5 kwa kila kichwa kimoja na ana Baada ya huyo jamaa kutamka vile ilibidi niingie mitaani kuulizia wapaka kucha huwa watoza kiasi gani kwa kichwa kimo, nikauliza pia wapakwa kucha hutoa kiasi gani. Huyo mjuba ni kama alitaka sifa kwa kazi yake ya kupaka kucha, anasema inalipa kuliko muziki anaoimba. Anadai amepaka kucha mastaa wengi wakiwemo wanamuziki na maproducer wa kiume. anadai kuna producer mmoja alimpa laki moja na baadaye akaongeza ikawa milioni moja. Sijui kama ni kweli alipewa dau hilo au anataka sifa tu ili naye ajulikane ni mwanamuzi mpaka kucha. Kuna wapaka kucha mitaani wamechoka vibaya hadi buku wanachukua lakini huyo mjuba anasema anapaka kucha hadi milioni moja kwa kichwa kimoja!