Hii joke ni ya ovyo sana ya Kisukuma.
Naona hufai kabisa kutoa JOKE maana kuanzia mwanzo tu unafahamu itaishia wapi.
Maadamu umesema Wasukuma ni Wachungaji ng'ombe basi soma hii ya huyu Mchungaji:
Mchungaji mmoja wa ng'ombe na huku akiwa ndiye mwenye hao ng'ombe, alienda kwenye mnada maarufu wa ng'ombe pale Pugu na kuwauza ng'ombe wake wote aliotaka kama behewa moja. Aliamua kwenda Dar na pesa kuziweka Bank. Alibakiza kwa matumizi yake ya kawaida wakati akiwa pale Dar. Jioni alienda kupata moja baridi na nyama choma na akiwa hapo akaja dada mmoja akakaa na mazungumzo yakaanza:
Dada: Habari yako kaka? Naona sura ngeni hapa, wewe ni mwenyeji wa hapa?
Mchungaji(Mdemi) aka Ngosha: Nzuri sana. Mie ni mchungaji na mfugaji wa ng'ombe kutoka Ushirombo. Nipo hapa kibiashara.
Dada: Sasa umejuaje kuwa wewe ni Mchungaji au kama ulivyosema wewe kwa Kisukuma , wewe ni Mdemi?
Mchungaji: Nikiamka nyumbani, huwa naenda kwenye zizi kuangalia kama ng'ombe wazima. Baadaye nawapeleka kuchunga, narudi kukamua maziwa, nawapeleka kunywa maji, nawafanyia matibabu ya kila aina, kuzalisha .......... Hii ndiyo ilinifanya niamini kuwa mie ni MCHUNGAJI. Na wewe mwenzangu?
Dada: Mie ni Lesbian. Nikiamka nawaza Mwanamke, nikienda kazini nawaza mwanamke, ninapopika, mwanamke ....... mwanamke.
Yule dada na Mchungaji wakanywa bia moja moja na dada akaaga.
Baada ya dakika tano, akaja jamaa na kukaa na Ngosha Mchungaji:
Jamaa: Habari yako. Mie naitwa James, mwalimu wa Secondary Forodhani. Mwenzangu ni nani?
Mchungaji: Naitwa Ng'inki. Hadi dakika tano zilizopita, nilikuwa nafahamu kuwa mie ni Mchungaji, ila sasa nimejua kuwa mie ni Lesbian.