Wasukuma Msilazimishe Wageni kwenye Nzengo/ vikundi vyenu

Wasukuma Msilazimishe Wageni kwenye Nzengo/ vikundi vyenu

Pantomath

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
842
Reaction score
3,487
Hii jamii sijui inaishi dunia ipi, mimi nijuavyo ni kweli mtu ukienda kwenye Jamii mpya Jichanganye kwenye shughuli za Kijamii(kwangu mimi zaidi majanga), hilo halina ubishi, tunaishi kwa kushirikiana.

Sasa hawa jamaa wana mambo meusi kweli, kwanza kuingia kwenye hio sijui wanaita Nzengo yao Eti unachamgia elf 15 wengine mpk 30, wengine chini ya hapo. Sasa mimi kushiriki Shughuli za kijamii nalipia ili?

Lakini zaidi Wao unaambiwa bora usishiriki msiba kuliko sherehe, yaani hio ni kesi. Hapa tulipofikia na mshkaji wangu, jana kukawa na harusi(hili nalo sielewi, kila siku wanaharusi na ni za katikati ya week, nikauliza wakasema sijui ni kipindi cha harusi) sasa mshkaji akasema ngoja niende na mwenyeji wetu.

Daadeki kajikoroga, kufika kusalimia wa mama Kiswahili maana salamu zao bado hatuja zi masta ili usije ukachafua lugha ya watu unasalimia lugha ya taifa,

Khaaa wamama wakaanza kumteta, kwa Mtu mzima unajua tuu hapa nasemwa ukiangalia sura, mapokezano n.k, wakati kurudi jamaa ndio akawa anamuambia walivyokua wanamsema, mara oooh anajifanya mswahili, Hajui kuishi na watu n.k n.k..

Hajakaa vizuri akaambiwa jitambulishe, Likaletwa daftari aandike jina, anamaliza anaambiwa toa 15k, mwingine 10k, mwingne 20k, kwa ufupi haina mtiririko? Ukiuliza ya nini huambiwi.

Kapiga kazi, baada ya mda akaomba kuondoka.

Wakaanza Wewe tunakuruhusu tuu leo hio tabia hatuitaki, kwanza wanaume mnakuja asubuhi saa 12 nyie mmechelewa, na maneno mengi balaa, mwenyeji anatuambia huku siku ya nzengo yao hata kama ni muajiriwa inabidi uombe ruhusa kazini, na hio inajulikana.

Jamaa karudi kainamisha kichwaa, wema wake ukamponza,

Mimi kuniambia hivyo nikasema nilikua na hilo lengo ila huo upuuzi sifanyi, Potelea kote, nitashiriki kwenye Mambo ya jamii ya lazima kama nijuavyo ila sitaki waniweke kwenye hio mizengo yao, Hii jamii nilikua naona ni kama utani kwenye mitandao, Wonderful enough ni mjini, jee huko ndani ndani? Hawa watu bado wapo nyuma sana, nimalize Majukumu yangu nirudi Zangu.

Haya masuala ya kutishana eti siku likikupata la kukupata, ni maneno tuu ya kumjengea mtu hofu ya mbele, Wangapi wanaonesha wema hawarudishiwi?

Nyie wasukuma mliopo JF elimisheni wasukuma/wanyantuzu wenzenu waache mambo ya kikale pia wache ukabila na Umuhimu wa vyoo.
 
Huko Bariadi utakoma.

Nimeishi Mwanza 2 years nimehudhuria misiba na sherehe ya watu niliowafahamu tu tena wengi wao ni katika connections za kikazi.

Huko mtaani kwangu sidhani kama kuna aliyekuwa ananifahamu.

Labda pale sehemu ya ibada.
 
Hii jamii sijui inaishi dunia ipi, mimi nijuavyo ni kweli mtu ukienda kwenye Jamii mpya Jichanganye kwenye shughuli za Kijamii(kwangu mimi zaidi majanga)...
Jifunze kwa mtume Paulo "Ukiwa kwa wahebrania ishi kama mhebrania ili uende sawa na wahebrania, pia ukienda kwa wayunani ishi kama wanavyoishi wayunani......"

Ukishindwa kuishi kama wao hamia kwenu ulikozoelea kuishi, mambo ya wengine waachie wenyewe ikiwa huwezi kuishi kama wao.

Utaratibu huu upo kila pahali duniani.
 
Jifunze kwa mtume Paulo "Ukiwa kwa wahebrania ishi kama mhebrania ili uende sawa na wahebrania, pia ukienda kwa wayunani ishi kama wanavyoishi wayunani......"

Ukishindwa kuishi kama wao hamia kwenu ulikozoelea kuishi, mambo ya wengine waachie wenyewe ikiwa huwezi kuishi kama wao.

Utaratibu huu upo kila pahali duniani.
Utaratibu wa kuchangia pesa ili uingie kwenye kikundi cha kushiriki shuguli za jamii? Imekua vikoba?
Utaratibu wa kusemwa usipo ongea kilugha?
Acheni ukale
 
Ningekuwa mwenyekiti wa wana nzengo huko ulikozamia ningekushikisha ugoni ili upigwe viboko hadharani maana naona umelelewa kihuni huni sana.
Umeona sasa , huelewi unachoandika,
Ulanzi utakuponza Dogo, hautakufikisha popote.
 
Back
Top Bottom