Wasukuma Msilazimishe Wageni kwenye Nzengo/ vikundi vyenu

Wasukuma Msilazimishe Wageni kwenye Nzengo/ vikundi vyenu

We shiriki tu misiba na sherehe ukipata nafasi, usishiriki kwasababu ya kuogopa eti ukipata msiba watakutenga we shiriki kwasababu ni wajib kwa binadam kuzikana na kushirikiana
 
Jifunze kwa mtume Paulo "Ukiwa kwa wahebrania ishi kama mhebrania ili uende sawa na wahebrania, pia ukienda kwa wayunani ishi kama wanavyoishi wayunani......"

Ukishindwa kuishi kama wao hamia kwenu ulikozoelea kuishi, mambo ya wengine waachie wenyewe ikiwa huwezi kuishi kama wao.

Utaratibu huu upo kila pahali duniani.
Nakazia.
 
Leo ngoja niseme jambo. Nina miezi takribani saba tangu nianze kuishi hapa Chato mkoani Geita. Niko taasisi ya kiserikali, lakini sasa wakazi wa hapa hususani wasukuma wamekuwa na mambo ya kidwanzi sijapata kuona. Kwakuwa tunahudumia wananchi unakuta mteja mmoja anajuana na mtumishi mwenzangu, basi kama ana harusi aidha ya kwake, ndgu yake wa familia, mtoto wa mjomba,shangazi sijui bamdgo unakuta analeta kadi kwa huyo anayemfahamu, then anakusanya majina ya kila mtumishi anatoa kadi ambazo hazijajazwa anajaza taarifa alizokusanya, kisha anamwachia huyo mtumishi anayemfahamu ili aje azigawe kwa wahusika. Ni mara tatu napigiwa simu na watu tofautu naulizwa mbona sijafika kwenye kikao cha wanakamati. Yani watu huwajui ila kisa tu upo ofisini unawekwa kwenye masuala bila ridhaa yako tena kwa mtu ambaye hata humjui wala hujawahi kumwona. Kwakweli hili nilipinga ila wenzangu wanaogopa kwa kupitia ile dhana ya "vp siku ukipata shida" ukiuliza shida gani hawana la kusema, wengine wana ile "je, siku ukitaka kuoa hawatakuchangia" hapa huwa nacheka sana kwa sababu sijawahi kuwaza kuchangisha watu hususani huku nilipo maana mkoa wangu common ni mwingine na nimeji establish huko. Hapo sijaongelea mentality na perceptions za watu wa huku maana hiko nacho ni kipengele. Mpaka huwa nasema kwamba kuna maeneo TZ bado sana
 
Back
Top Bottom