Wastaafu na matumaini hasi

Deghe Mangae

Senior Member
Mar 3, 2020
171
149
Binafsi naona kizungumkuti kwa wastaafu wa utumishi wa Serikali bado hawajui hatima yao ya mafao manake hawapati kwa wakati.

Hii haileti picha nzuri mtumishi ameshajichokea bado anacheleweshewa mafao yake. Hii kitu
mbaya sana na huu sio ustaarabu kabisakwa kweli hii tabia siipendi kabisa mimi binafsi.

Mtumishi amesota miaka kibao
bado tu hatendewi haki kwanini?

Hebu Serikali iliangalie hili kwa jicho la tatu mnasubiri mpaka Afariki?
 
Watu walikuwa wanawacheka wale wastaafu wa Jumuiya ya Afrika mashariki waliokuwa kila mara wanaandamana mitaa ya Posta kudai mafao yao ya toka miaka ya 1977. Sasa ngoma tunaicheza wote.

CCM ni zaidi ya laana.
 
Ndio serikali ya wanyonge hio,huku ikisema ina mapesa mengi saana(donor country).
 
Katika uamuzi mzuri niliowahi kufanya ni kuchota hela za nssf za mwajiri wangu wa kwanza.. angalau nimezionja.. japo za mwajiri wa pili nimezikosa
 
Katika uamuzi mzuri niliowahi kufanya ni kuchota hela za nssf za mwajiri wangu wa kwanza.. angalau nimezionja.. japo za mwajiri wa pili nimezikosa
Usijali serikali hii sikivu ya wanyonge kabisaa itakupa na hizo za mwajiri wa pili.
 
Back
Top Bottom