Wassira si msafi; achunguzwe!

Wassira si msafi; achunguzwe!

Kumbe ana uzoefu,sasa rasimali za nchi ukimwachia mwizi asimamie unategemea nini
 
Duuuu, jamani mwishowe mtakuja na kashfa ya KUKOMBA MBOGA akiwa darasa la nne mwaka 1965. Kazi kwelikweli. Ukiwa kwenye nyumba yenye vioo usimrushie mwenzie jiwe.
 
CDM wana mafaili ya kila mtu!! Mtu akijipendekeza kifisadi anapewa file lake. M4C
 
"Msimuandame handsome wetu!!" Mpeni heshima yake au hamjui kwamba analiingizia Taifa pesa nyingi za kigeni kutoka kwa watalii wanaongia nchini!!? Kwa taarifa yenu yeye ndie kivutio cha watalii hapa Bongo ha Ikulu!! MUHESHIMUNI!!
 
Mwangalieni vizuri huyu jamaa anavyotetea Magamba wenzie, waswahili wamesema " aisifiae mvua imemnyea". Jamaa anaonyesha yuko pale Magogoni kimalengo na biashara zake haramu!
 
SIYO VIVYO TU MKUU. WASSIRA MWAKA 1995 akiwa NCCR-MAGEUZI alimtukana JAJI WARIOBA aliyekuwa mgombea wa CCM UBUNGE JIMBO LA BUNDA kwamba wanannchi wasimchague WARIOBA kwani anaumwa (1) UKIMWI, (na (2) TB hivyo atakufa baada ya uchaguzi. WASSIRA akachaguliwa MBUNGE kupitia NCCR. WARIOBA akapinga matokeo. Mahakama Kuu IKAFUTA MATOKEO KWANI WASSIRA (1) alitumia lugha ya ubaguzi, na (2) alitoa HONGO na kumzuia WASSIRA asijihusishe na siasa kwa miaka 5. TATIZO LA TANZANIA USAHAULIFU, WASSIRA HAFAI, BUSARA HANA (REJEA HUKUMU HIYO)

Waziri Ofisi ya Rais - Mahusiano na Uratibu (President's Office-Social Relations and Co-ordination) Bwana Stephen Masato Wassira, ameripotiwa kuwa na historia ya kuoa na kuacha wake zaidi ya wanne katika historia yake.

Na cha kusikitisha zaidi wanaharakati wa haki za binadamu na jinsia,wamehabarishwa kupitia vyanzo vya kuaminika kuwa, amemtelekeza mkewe, Mama Rose Wasira, ambae amezaa nae watoto sita,ikiwa ni pamoja na kijana alieoa hivi karibuni, aitwae Kambarage Wasira. Wengi wamepinga kupewa nafasi hii ya mahusiano ya jamii kwani yeye binafsi hana sifa hiyo. Ameripotiwa kunyanyasa kwa kijinsia na kuwapiga wake zake.Habari za kuaminika zimeripoti kuwepo kwa nyaraka za hospitali za mkewe mkubwa ambaye amepata ulemavu wa mgongo na shingo wa kudumu,kutokana na vipigo vya waziri huyu, ajulikanae pia kwa jina la TYSON.

Wadau wapenda maendeleo,wa forum hii waliwahi kuhoji nini Majuklumu ya Wizara ya "TYSON"?? Wakati mjadala huo ukiendelea, kumeibuka habari hizi ambazo zinaendelea kuongeza hamaki baina ya wadau mbalimbali.

Habari za kuaminika zinadai kuwa,Mzee Wasira,alipopata Uwaziri,alimtelekeza mkewe huyu,ambae alihangaika nae maisha yake yote, na kumtwaa kimwana machachari,ambaye ni Diwani Viti Maalum,Kata ya Mwananyamala(CCM), Florence Gathi Wasirra. Mwanamama huyu inasemekana ni mroho wa mali na mpenda utajiri alikuwa mke wa Marehemu Casmir, Bigacho Ndege, aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwananyamala. Mzee Wasira anaishi na Mama huyu katika nyumba ya Uwaziri Masaki.

Habari zilizotufikia hivi punde, zimebainisha waziri huyu kuwa mshirika wa kibiashara wa huyu Diwani ambapo wanamiliki kwa Pamoja, makampuni kama Gati Insurance Brokers, yenye makao makuu jijini Dar,na STEGA COMPANY LIMITED.(Stephen & Gati).

Makampuni haya yanatumika kufanya ufisadi katika Wizara anazoenda Wasira.Habari toka ndani ya Wizaera ya Kilimo zimebainisha kuwepo na vitendo vya ufujaji, ikiwa ni pamoja na kuomba kununuliwa Samani za ndani mara kwa mara (Furnitures), ambapo samani hizo zimetumika kufungua Guest (nyumba ya Kulala Wageni), iitwayo PINA, Bahari Beach ambayo ilikua nyumba ya Marehemu Ndege.

Watu hawa hawastahili kuwa viongozi wetu.na jamii iwakemee.Wadau wamemuomba Rais JK amuondoe huyu Waziri kwenye nafasi za umma.

Aidha Wanaharakati wa Legal and Human Rights Centre, wamepata habari hizi kwa mshituko na kuahidi kuzishughulikia,hasa kuhakikisha Mama huyu anapata haki zake.

Habari zaidi kutoka Kitengo cha Vizazi na Vifo(RITA),zimethibitisha kuonekana kwa Mama wasira akifuatilia cheti cha ndoa, ambacho inasemekana Waziri wasira alitumia madaraka yake Kula njama na kufuta katika kumbukumbu.

Akizungumza na Wanaharakati waliofuatilia zaidi, Kiongozi wa RITA ambae hakutaka jina lake litajwe,alisema;'Hata sisi tunashangazwa na jinsi kumbukumbu ya cheti hiki ilivyotoweka, lazima kuna jambo'.

Wanaharakati wameomba vyombo vya maadili,ikiwa pamoja na PCCB.kumchunguza kwa kina na kuchukua hatua za kinidhamu kukomesha maovu baina ya viongozi wa Umma.Maswali muhimu ya kujiuliza ni kwamba,Je Vyombo husika havifahamu mambo haya?na hatua gani zinachukuliwa?

Vyanzo vya kuaminika kutoka Tume ya maadili vimebaini kuwa,Bwana Wasira hakutaja Hisa zake katika makampuni yanayoshutumiwa hapo juu,wakati wa zoezi muhimu la viongozi kuweka bayana mali zao,na hii inahusisha hisa za kampuni na Biashara mbalimbali.Aidha,Rais JK,aliwahi kuwataka viongozi wachague kati ya SIasa na Biashara,na kuwataka Wanasiasa waachane na Biashara ili kuepuka migongano ya Kimaslahi katika utendaji wao na kuunga mkono juhudi za Rais katika kupiga vita ufisadi na ubadhilifu ndani ya serikali.
 
Wa kulaumiwa hapa ni RA aliyemrudisha Wassira wakati wanaunda mtandao wao haramu wa kukamata IKULU. Mzee huyu kabla Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 alikuwa hoi bin taabani akivaa soksi vidole vinachungulia nje kama kichwa cha kobe na gamba lake. RA akamfuata akampiga jeki la nguvu akamwezesha kwa sana tu kugombea Ubunge Bunda. Kwa kuwa Mzee wetu huyu ni mshawishi, mfitini na mjenga hoja mzuri akafiti sana ndani ya Mtandao. Alipopita Ubunge Cabinet ya kwanza ya JK akaukwaa Uwaziri. Akaingia kwa nguvu sana kuzitafuna taasisi zilizokuwa chini ya wizara alizopitia. Ametoka. Ana miradi mingi tu sasa. Ana kahoteli kake kule Mbugani Serengeti pia. Hakufanya makosa safari hii.
 
SIYO VIVYO TU MKUU. WASSIRA MWAKA 1995 akiwa NCCR-MAGEUZI alimtukana JAJI WARIOBA aliyekuwa mgombea wa CCM UBUNGE JIMBO LA BUNDA kwamba wanannchi wasimchague WARIOBA kwani anaumwa (1) UKIMWI, (na (2) TB hivyo atakufa baada ya uchaguzi. WASSIRA akachaguliwa MBUNGE kupitia NCCR. WARIOBA akapinga matokeo. Mahakama Kuu IKAFUTA MATOKEO KWANI WASSIRA (1) alitumia lugha ya ubaguzi, na (2) alitoa HONGO na kumzuia WASSIRA asijihusishe na siasa kwa miaka 5. TATIZO LA TANZANIA USAHAULIFU, WASSIRA HAFAI, BUSARA HANA (REJEA HUKUMU HIYO)

Binafsi naikumbuka sana hukumu hii, kwa kuwa miaka hiyo nilikuwa nishaanza kujiingiza katika kushabikia siasa. Kimsingi jamaa hafai kuwa kiongozi mwadilifu
 
Aseee!!!!sasa hilo tairi alilifungua kwenye gari au aliliiba stoo?nafikiri alitoka nalo nduki ya kufa mtu,CCM haya mambo ya wizi wameanza nayo mbali sana.
 
ni mimi ndio nilianzisha uzi wa kutaka kufahamishiwa majukumu ya kisheria wa Waziri Wassira maana najua yuko 100% kinyume historically anayotakiwa kuyasimamia/kuyaongoza. Wakati wa utawala wa Clinton, alimteua mama fulani kuwa Waziri wa Sheria, ikaonekana katika historia ya yule mama alipata kuajiri housemaid ambaye ni illegal immigrant so akajiuzulu.
 
Back
Top Bottom