Wassira, ninamleta kwako Abasalom Kibanda

Wassira, ninamleta kwako Abasalom Kibanda

Mkuu Tunduruboy, political life story ya smw ni story ambayo hata kijana kizazi kipya aliyekata tamaa anaweza kupata inspiration tumaini jipya kuwa usikate tamaa in life..Wassira huyu ni jembe aliwahi kupanda sana na kweli akashuka sana hata pengine kunyeshewa mvua akielekea kwa Mkuu Kibanda, sio hilo tu, na pia alishafanya hata biashara ya fish-Namanga.Ila kwa kutokukata tamaa, akarudi, in english wanasema, alifanya comeback katika siasa ya Tanzania, na haya sishangai ni because hivi sasa yuko juu in CCM. Kwa vijana wasiokuwa na ajira au tumaini, au vijana waliomaliza form four usahishaji umewaleta division zero--nasema: "dont give up" Amini si mwisho. Muige kwa babu yenu mzee Wassira "kwa kichwa", "sio kwa ufisadi' hajanunua mtu na akarudisha ramani yake binafsi iliyopotea katika kilele cha siasa Tanzania..

Matatizo yapo mengi Tanzania, Swala la Kibanda linatumika kuchanganya watu kwa maksudi sababu alichosema juu ya Kibanda alikuwa haongei kama yeye Wasira, aliongea kama msemaji wa Serikali ikizushiwa mambo mengi naye kama Waziri wa Mahusiano, refuting kwa kutumia commonsense, akihoji mantiki for the State of TZ to wage a war on Mr. Kibanda. Why? Yeye kumjua au kutomjua binafsi Abasalom Kibanda sio Mastakabali wa Nchi kihivyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wa sasa, Bwana John Kerry, aliwahi kugombea Urais wa Marekani mwaka 2004 dhidi ya George W. Bush, Rais wa 43 wa USA. Kwa ustadi mkubwa, wakati wa kampeni, aliandamwa na mbinu chafu za kubadilisha maneno, upotoshwaji wa matamshi au hoja mpwitompwito za aina ya "Kibanda ni nani?" dhidi ya Kerry hadi kupoteza uchaguzi ule na huku pengine angewafaa Wamarekani kuliko George W. Bush na Vita zake Iraq zilizoharibu Uchumi, Rais Obama asingempa John Kerry kazi kubwa aliyonayo kama kweli ni mtu asiyefaa kiuongozi

Nasi tunaelekea Uchaguzi 2015, watanzania kama wachina tutacopy and paste mbinu nyingi tupate ili Nani awe nanhii wetu. Bado guys.CHUKUENI POPCORN HII KIBANDA MOVIE NI TRELA TU, SINEMA YENYWE HAIJAANZA


Eehe KIPANDE KINGINE CHA MOVIE KITACHUKULIWA WAPI MKUU?
NA WEWE BILASHAKA KUNAKIPANDE UMESHIRIKI NI KIPI KATI HIVI V3
1.KUTOBOA JICHO
3.KUNGOA KUCHA
3.KINANA YEYE YUPO KWENYE MENO YA TEMBO WEWE YA WATU NINI KWA KUTUMIA COMBINATION PLIES?
 
Tunamsubiri kwa hamu kubwa kibanda arudi salama atupe new episode baada ya yeye kuwa "marehemu"anaetembea ,kama yaliyomtokea Mwakyembe!baada kunusurika,akasema sasa haogopi mtu na atafyatuka tu!tunaamini Kibanda nae hatakaa kimya!tutasikia mengi sana na nyeti kutoka kwake ,siamini kama atakaa kimya kama Dr Uli!
 
Kwani wewe huoni hata chemistry ya uumbaji wake haiko sawa?ukimuangalia kafanana na kiumbe gani?hata akili zake ziko kama hicho kiumbe!

Usikosoe uumbaji wa Mungu hata kama mhusika amekosea. Hayo siyo maneno mazuri kumwambia binadamu mwenzako.
 
Wasira kweli kiboko, anawanyima usingizi kila kukicha.
Nimeamini huyu ndiye Mwarobaini wa Chadema, Suala la Kibanda Wasira alishafafanua na Ikaeleweka.
Mie nadhani mnaweweseka kama huyu Taison akikabidhiwa rungu 2015.
 
Hakumbuki tena alivyokuwa akiomba lifti kwenye daladala. Wanadamu bwana.
 
Ma CCM bwana kila kukicha yanachapwa .Haya Wassira na genge lako njooni mjiteteee hapa .Kama Nchimbi jana ana hoji juunya Chadema kupewa Nchi .Eti tukiwapa Nchi hakika I was amazed uwezo wa huyu jamaa

Safi sana Nchimbi tena! amekwisha 2015 mwisho waki Songea
 
WASIFU wa watu wakubwa hutolewa na watu wadogo. Kiongozianapochaguliwa wasifu wake huandikwa au kusomwa na watu walio chini yake, iliwaliomchangua kuwaongoza ambao ni watu wadogo kwake, wamfahamu vema.

Huu ni utaratibuwa kawaida kabisa na unatumika karibu duniani kote. Ndivyo ilivyokuwa kwarafiki yangu, Rais Jakaya Kikwete na wale waliomtangulia Ikulu. Na imekuwahivyo kwa watu wengine wakubwa.

Kwa kufuatautaratibu huo huo, ninaandika kwa mbwembwe zote za kichokonozi wasifu waAbsalom Kibanda, mtu mkubwa sanahapa nchini ambaye watu wadogo wa aina ya Steven Masatu Wassira, hawamfahamu!Ninaandika wasifu huu kwa lugha adhimu ya kichokonozi, ili Wassira amueleweKibanda vizuri.

Nieleweke hapakuwa ukubwa ninaouzungumzia siyo wa nyama za mwilini, huo hauna maana sana kwa sababu hatasambusa zilizonona zimetengenezwa kwa nyama. Ninachomaanisha ni ukubwa wawadhifa.

NinakuandikiaWassira wasifu wa Absalom Kibanda, ili siku nyingine usihoji ni nani. Ninatakaufahamu kuwa Kibanda ni mtu mkubwa, maarufu na anayeheshimika sana hapa kwetu na hata kwa wenzetu.

Wassira,ninakuandikia wasifu wa mwandishi anayeheshimiwa na wakubwa kiasi cha heshimahiyo kupitiliza na kuwa woga. Wapo wakubwa wenzie wanaomuogopa. Wassira,Kibanda anaogopwa na wakubwa na wanamtambua.

NinakuandikiaWassira wasifu wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania,ambao nao ni watu wakubwa pia, hivyo ili kuwa mkubwa wao ni lazima uwe mkubwakweli kweli kama alivyo Kibanda.

Wassira, ninakuandikiawasifu wa Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd.Ninakuandikia wasifu wa mwalimu na bosi wa wachokonozi, watu adimu sana kupatikana hapaduniani, hivyo kuwa mwalimu au bosi wao shurti nawe uwe wa aina hiyo.

Ninafanya hivi kwasababu yako Wassira, mtu mdogo kiwadhifa usiyemfahamu mtu mkubwa anayeheshimiwana wakubwa. Ninakuandika kukusaidia wewe Wassira umfahamu kiongozianayeheshimiwa na wengi wenye akili, ambao kamwe hawawezi kuhoji Kibanda ninani kama ulivyofanya wewe!

Ninaanza; Wassira,sina sababu ya kukujuza Kibanda alizaliwa wapi, baba na mama yake ni akinanani, ni mtoto wa ngapi kuzaliwa na anao ndugu wangapi aliozaliwa nao tumbomoja, kwa sababu sikuamini sana.Siku nikikuamini nitafanya hivyo.

Muhimu kwako kujuani kwamba, Kibanda sasa ana umri wa Miaka 47. Ni mhariri mwenye nguvu kati yawachache waliopata kutokea hapa nchini. Ni mchambuzi mahiri wa masuala ya siasana amekuwa mshauri na mkufunzi kwa muda wa miaka ipatayo 19 sasa. Kwa sababuhiyo anaheshimika na kufahamika sana.

Wassira, Kibandani Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania. Nafasi ambayo aliipatakatika uchaguzi wa 2010, baada ya kuwabwanga waandishi wengine nguli kwelikweli waliokuwa wakiwania nafasi hiyo katika uchaguzi ambao haukuwa na uchakachuajiwa kura kama ule ambao wewe unaujua.

Kwa nafasi hiyo,Kibanda anaongoza watu wenye akili nyingi, wana utaalamu ambao bosi wako,rafiki yangu Rais Jakaya Kikwete anawaheshimu kupindukia, kwa sababu anatambuamchango wao kwake uliofanikisha ndoto yake ya miaka kumi ya kuwa Rais wa Tanzania.

Wassira, Kibandani mwanzilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania na kabla ya kuchaguliwakuwa Mwenyekiti, alikuwa akikaimu nafasi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Wassira,ninapokuandikia wasifu wa mtu huyu mkubwa, nataka uwe unaulinganisha na ule wakwako ili uone jinsi mlivyo tofauti. Nataka utambue kuwa kwa wasifu wake,unastahili kumuheshimu na kumtambua. Ukifanya hivyo, itakusaidia sana katika kipindi hikicha kuelekea mwaka 2015.

Kibanda amekuwaMhariri Mtendaji Kampuni ya Free Media Ltd, inayochapisha gazeti la TanzaniaDaima na Sayari kwa muda wa miaka sita, tangu mwaka 2006 hadi mwaka janamwishoni. Nadhani unalijua vema gazeti hili.

Ni Mkurugenzi Mkuuwa Kampuni ya Leap Media Management Ltd, inayochapisha Jarida pekee la siasalinaloitwa Umoja, ambalo hutoka mara moja kwa mwezi, jarida hili ni mithili yamajarida makubwa duniani kama Time, News Weekna mengine.

Amekuwa mwandishiwa habari tangu mwaka 1992, amefundisha masomo ya Histori na ‘Literature’katika Shule ya Sekondari Shaaban Robert kati ya mwaka 1995 hadi 1996, kablahajajiunga na Kampuni ya Habari Corporation Ltd mwaka 1996. Hivyo tambua kuwaanao uwezo mkubwa wa kumwaga ngeli. Akiwa na wazungu anakuwa mzungu, akiwa nawaswahili anakuwa kama walivyo.

Katika umri wakowa utu uzima Wassira, ninaamini kumbukumbu bado unazo hivyo unakumbuka kwambawakati huo, Habari Corporation ilikuwa Kampuni yenye nguvu kubwa miongoni mwakampuni zilizokuwa zikimiliki vyombo vya habari, hivyo kujiunga nayo halikuwajambo rahisi.

Kibanda, akiwa navijana wenzake wenye akili, Marehemu Danny Mwakiteleko na Jesse Kwayu ambayesasa ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe, walinyakuliwa na HabariCorporation baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampunihiyo, Jenerali Ulimwengu, kuutamani uwezo wao wa kazi na hasa akili za vijanahao.

Wassira sijuikwako wewe ni wangapi wenye akili waliowahi kutamani akili na uwezo wako wakazi hadi wakaamua kukufuata ufanye nao kazi.

Siyo jambo rahisikuandika wasifu wa mtu wa aina ya Kibanda kwa ukamilifu pasipo kuacha nyamanyama za kuunenepesha kwa sababu una mambo mengi mno. Kwa sababu hiyo,ninaandika kwa uchache yale yanayofahamika na wengi ambayo wewe Wassira unadaikuwa huyajui wakati ni uongo.

Wassira, Desemba1999 Kibanda alijiunga na Kampuni ya Media Communication Ltd, sasa MwananchiCommunications Ltd, akiwa mwandishi mwandamizi katika jarida la siasa la WIKIHII. Alikuwa na jukumu kubwa la kuanzisha gazeti la Kiswahili la Mwananchi.

Wakati Kampuni yaNation Media Group kutoka Nairobi iliponunuahisa za Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Kibanda alikuwa mwandishi wakwanza kutoka Tanzania,ambaye aliweza kuandika makala katika gazeti la Nation la nchini Kenya na The Monitor la Uganda kwalugha ya fasaha ya kimombo, hivyo maandishi yake yamekuwa yakisomeka nje yanchi tangu miaka hiyo.

Akifanya kazikatika gazeti la Mwananchi, alishika nyadhifa mbalimbali za Mhariri wa Makala,Mhariri wa Biashara na Mhariri wa gazeti la Mwananchi Jumapili, ambalo wakatiakiliongoza, ndilo lililokuwa likishika nambari wani katika mauzo hapa nchini.

Ni wakati huoWassira, ukiwa unatangatanga katika vyama vya siasa, ukiwa umechoka sana kimaisha, mwaka2003, ukiwa mwanachama wa Chama cha NCCR- Mageuzi uliyekuwa ukibembelezakuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulikutana na Kibanda, akakuinua kutoka kwenyeuhohehahe uliokuwa ukikuandama.

Wassira, kwa niniunakuwa msahaulifu? Au ni ulevi wa madaraka. Umepata sasa umesahau shidaulizokuwa nazo na kwamba Kibanda ni mmoja wa watu waliokunusuru katika dhikiulizokuwa nazo.

NikukumbusheWassira, mwaka 2003, wakati unahaha kujiunga na CCM, ulifunga safari kutokaunakokujua, ulisafiri kwa daladala, ukashuka Kinondoni Makaburini, mvua ikiwainanyesha, ukakanyaga kwa mguu kutoka hapo hadi Kenyatta Drive, Nyumba namba10.

Ulifika ukiwahutamaniki, umelowa chapa chapa, ulikutana na Kibanda, akakufanyia mahojianoambayo uliyatumia kujenga hoja kuwa rais wa Tanzaniasiyo lazima atoke Zanzibar.Ni mahojiano hayo baina yako na Kibanda, ambayo yalikusaidia kuanza kufahamikamiongoni mwa wachambuzi wa mambo kuwa na wewe upo.

Wassira, usisahaukuwa baada ya mahojiano yako na Kibanda, viongozi wa CCM walikukabidhi kwa AmosMakala ili awe anafanya mawasiliano nawe ya mara kwa mara kabla hujarejea rasmiCCM. Wassira unaijua hali ya mfuko wako ilivyokuwa wakati huo. Umesahau?

Leo baada yakuingia bungeni na kuzawadiwa uwaziri, unahoji Kibanda ni nani? Wassira! WeweWassira ambaye sisi wachokonozi tumetunza mizigo ya faili zako.

Wassira, Kibandaunayehoji ni nani, ndiye uliyekutana naye Dodomakwa rafiki yangu rais Kikwete miaka ile unaanza kutizamika kidogo kuwa na weweni mtu.

Ulikutana naKibanda akiwa na mwandishi mwenzake, Muhingo Rweyemamu ambaye sasa ni Mkuu waWilaya, naamini unaijua wilaya anayoiongoza. Kibanda na Rweyemamu walikwendakwa rafiki yangu rais Kikwete kufanya naye mahojiano. Wewe uliwakuta hapo,wakati huo ndiyo umepata gari, Land Cruiser nyeupe ya kizamani. Mlisalimiani.

Wassira, Kibandandiye aliyeshitakiwa mahakamani kwa uchochezi. Kisa uhariri mkuu wake!Mwandishi wa makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi siyo yeye, mhariri wa makalasiyo yeye, mhariri siyo yeye, ni Mhariri Mtendaji. Sijui kama hapo unanielewa.

Aidha, mtu huyuKibanda, ndiye aliyetaka kuuawa kwa kusababishiwa ajali ya gari mwaka jana,lakini taarifa za kusudio la kumuua zilivuja kabla.

Kibanda ndiyealiyekuwa akiandika habari zako ukiwa bungeni na sasa yuko nchini Afrika Kusinianatibiwa, baada ya kuumizwa na watu fulani wanaodaiwa kuwa na wewe karibulakini wewe unakataa kuwa hawawezi kumuumizwa kwa sababu yeye Kibanda ni nani?

Wassira, au kama unavyoitwa na wengine Tyson, huyo ndiye AbsalomKibanda.

MTANZANIA
Unapoteza muda wako kumtaja mtu kama wasira!
 
Duh, chuki kwa kumtetea Wassira, kulikoni? Mtaje tu Wassira, chuki huyooo atagonga hodi! Ohoo, nimechokoza chuki, pole yangu.
 
Last edited by a moderator:
Mimi hapa naona kama mnamushambulia mhe wassira, kwani fadhila zake kwa kibanda lazima zionekana kwa kushuhudiwa na watu kama mtu anayepanda dala dala? Kibanda, alitaka asaidiwe nini kwa mhe. wassira ikashindikana? Je, kama kibanda alipandisha kisiasa wasira na sasa wasira ni kiongozi wa kitaifa haoni kuwa alifanya kitu kizuri tu mpaka alambwe mguu tena au wasira apande dala dala kukutana na kibanda?

Tanzania tuipendayo, hata mimi nilimsaidia sana kibanda kabla hajafika hatua hiyo lakini simulaumu ila namfurahia kwa kuwa anaweza kujitegemea!
 
Back
Top Bottom