Wassira, ninamleta kwako Abasalom Kibanda

tunduruboy

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
423
Reaction score
218
WASIFU wa watu wakubwa hutolewa na watu wadogo. Kiongozianapochaguliwa wasifu wake huandikwa au kusomwa na watu walio chini yake, iliwaliomchangua kuwaongoza ambao ni watu wadogo kwake, wamfahamu vema.

Huu ni utaratibuwa kawaida kabisa na unatumika karibu duniani kote. Ndivyo ilivyokuwa kwarafiki yangu, Rais Jakaya Kikwete na wale waliomtangulia Ikulu. Na imekuwahivyo kwa watu wengine wakubwa.

Kwa kufuatautaratibu huo huo, ninaandika kwa mbwembwe zote za kichokonozi wasifu waAbsalom Kibanda, mtu mkubwa sanahapa nchini ambaye watu wadogo wa aina ya Steven Masatu Wassira, hawamfahamu!Ninaandika wasifu huu kwa lugha adhimu ya kichokonozi, ili Wassira amueleweKibanda vizuri.

Nieleweke hapakuwa ukubwa ninaouzungumzia siyo wa nyama za mwilini, huo hauna maana sana kwa sababu hatasambusa zilizonona zimetengenezwa kwa nyama. Ninachomaanisha ni ukubwa wawadhifa.

NinakuandikiaWassira wasifu wa Absalom Kibanda, ili siku nyingine usihoji ni nani. Ninatakaufahamu kuwa Kibanda ni mtu mkubwa, maarufu na anayeheshimika sana hapa kwetu na hata kwa wenzetu.

Wassira,ninakuandikia wasifu wa mwandishi anayeheshimiwa na wakubwa kiasi cha heshimahiyo kupitiliza na kuwa woga. Wapo wakubwa wenzie wanaomuogopa. Wassira,Kibanda anaogopwa na wakubwa na wanamtambua.

NinakuandikiaWassira wasifu wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania,ambao nao ni watu wakubwa pia, hivyo ili kuwa mkubwa wao ni lazima uwe mkubwakweli kweli kama alivyo Kibanda.

Wassira, ninakuandikiawasifu wa Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd.Ninakuandikia wasifu wa mwalimu na bosi wa wachokonozi, watu adimu sana kupatikana hapaduniani, hivyo kuwa mwalimu au bosi wao shurti nawe uwe wa aina hiyo.

Ninafanya hivi kwasababu yako Wassira, mtu mdogo kiwadhifa usiyemfahamu mtu mkubwa anayeheshimiwana wakubwa. Ninakuandika kukusaidia wewe Wassira umfahamu kiongozianayeheshimiwa na wengi wenye akili, ambao kamwe hawawezi kuhoji Kibanda ninani kama ulivyofanya wewe!

Ninaanza; Wassira,sina sababu ya kukujuza Kibanda alizaliwa wapi, baba na mama yake ni akinanani, ni mtoto wa ngapi kuzaliwa na anao ndugu wangapi aliozaliwa nao tumbomoja, kwa sababu sikuamini sana.Siku nikikuamini nitafanya hivyo.

Muhimu kwako kujuani kwamba, Kibanda sasa ana umri wa Miaka 47. Ni mhariri mwenye nguvu kati yawachache waliopata kutokea hapa nchini. Ni mchambuzi mahiri wa masuala ya siasana amekuwa mshauri na mkufunzi kwa muda wa miaka ipatayo 19 sasa. Kwa sababuhiyo anaheshimika na kufahamika sana.

Wassira, Kibandani Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania. Nafasi ambayo aliipatakatika uchaguzi wa 2010, baada ya kuwabwanga waandishi wengine nguli kwelikweli waliokuwa wakiwania nafasi hiyo katika uchaguzi ambao haukuwa na uchakachuajiwa kura kama ule ambao wewe unaujua.

Kwa nafasi hiyo,Kibanda anaongoza watu wenye akili nyingi, wana utaalamu ambao bosi wako,rafiki yangu Rais Jakaya Kikwete anawaheshimu kupindukia, kwa sababu anatambuamchango wao kwake uliofanikisha ndoto yake ya miaka kumi ya kuwa Rais wa Tanzania.

Wassira, Kibandani mwanzilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania na kabla ya kuchaguliwakuwa Mwenyekiti, alikuwa akikaimu nafasi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Wassira,ninapokuandikia wasifu wa mtu huyu mkubwa, nataka uwe unaulinganisha na ule wakwako ili uone jinsi mlivyo tofauti. Nataka utambue kuwa kwa wasifu wake,unastahili kumuheshimu na kumtambua. Ukifanya hivyo, itakusaidia sana katika kipindi hikicha kuelekea mwaka 2015.

Kibanda amekuwaMhariri Mtendaji Kampuni ya Free Media Ltd, inayochapisha gazeti la TanzaniaDaima na Sayari kwa muda wa miaka sita, tangu mwaka 2006 hadi mwaka janamwishoni. Nadhani unalijua vema gazeti hili.

Ni Mkurugenzi Mkuuwa Kampuni ya Leap Media Management Ltd, inayochapisha Jarida pekee la siasalinaloitwa Umoja, ambalo hutoka mara moja kwa mwezi, jarida hili ni mithili yamajarida makubwa duniani kama Time, News Weekna mengine.

Amekuwa mwandishiwa habari tangu mwaka 1992, amefundisha masomo ya Histori na ‘Literature’katika Shule ya Sekondari Shaaban Robert kati ya mwaka 1995 hadi 1996, kablahajajiunga na Kampuni ya Habari Corporation Ltd mwaka 1996. Hivyo tambua kuwaanao uwezo mkubwa wa kumwaga ngeli. Akiwa na wazungu anakuwa mzungu, akiwa nawaswahili anakuwa kama walivyo.

Katika umri wakowa utu uzima Wassira, ninaamini kumbukumbu bado unazo hivyo unakumbuka kwambawakati huo, Habari Corporation ilikuwa Kampuni yenye nguvu kubwa miongoni mwakampuni zilizokuwa zikimiliki vyombo vya habari, hivyo kujiunga nayo halikuwajambo rahisi.

Kibanda, akiwa navijana wenzake wenye akili, Marehemu Danny Mwakiteleko na Jesse Kwayu ambayesasa ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe, walinyakuliwa na HabariCorporation baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampunihiyo, Jenerali Ulimwengu, kuutamani uwezo wao wa kazi na hasa akili za vijanahao.

Wassira sijuikwako wewe ni wangapi wenye akili waliowahi kutamani akili na uwezo wako wakazi hadi wakaamua kukufuata ufanye nao kazi.

Siyo jambo rahisikuandika wasifu wa mtu wa aina ya Kibanda kwa ukamilifu pasipo kuacha nyamanyama za kuunenepesha kwa sababu una mambo mengi mno. Kwa sababu hiyo,ninaandika kwa uchache yale yanayofahamika na wengi ambayo wewe Wassira unadaikuwa huyajui wakati ni uongo.

Wassira, Desemba1999 Kibanda alijiunga na Kampuni ya Media Communication Ltd, sasa MwananchiCommunications Ltd, akiwa mwandishi mwandamizi katika jarida la siasa la WIKIHII. Alikuwa na jukumu kubwa la kuanzisha gazeti la Kiswahili la Mwananchi.

Wakati Kampuni yaNation Media Group kutoka Nairobi iliponunuahisa za Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Kibanda alikuwa mwandishi wakwanza kutoka Tanzania,ambaye aliweza kuandika makala katika gazeti la Nation la nchini Kenya na The Monitor la Uganda kwalugha ya fasaha ya kimombo, hivyo maandishi yake yamekuwa yakisomeka nje yanchi tangu miaka hiyo.

Akifanya kazikatika gazeti la Mwananchi, alishika nyadhifa mbalimbali za Mhariri wa Makala,Mhariri wa Biashara na Mhariri wa gazeti la Mwananchi Jumapili, ambalo wakatiakiliongoza, ndilo lililokuwa likishika nambari wani katika mauzo hapa nchini.

Ni wakati huoWassira, ukiwa unatangatanga katika vyama vya siasa, ukiwa umechoka sana kimaisha, mwaka2003, ukiwa mwanachama wa Chama cha NCCR- Mageuzi uliyekuwa ukibembelezakuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulikutana na Kibanda, akakuinua kutoka kwenyeuhohehahe uliokuwa ukikuandama.

Wassira, kwa niniunakuwa msahaulifu? Au ni ulevi wa madaraka. Umepata sasa umesahau shidaulizokuwa nazo na kwamba Kibanda ni mmoja wa watu waliokunusuru katika dhikiulizokuwa nazo.

NikukumbusheWassira, mwaka 2003, wakati unahaha kujiunga na CCM, ulifunga safari kutokaunakokujua, ulisafiri kwa daladala, ukashuka Kinondoni Makaburini, mvua ikiwainanyesha, ukakanyaga kwa mguu kutoka hapo hadi Kenyatta Drive, Nyumba namba10.

Ulifika ukiwahutamaniki, umelowa chapa chapa, ulikutana na Kibanda, akakufanyia mahojianoambayo uliyatumia kujenga hoja kuwa rais wa Tanzaniasiyo lazima atoke Zanzibar.Ni mahojiano hayo baina yako na Kibanda, ambayo yalikusaidia kuanza kufahamikamiongoni mwa wachambuzi wa mambo kuwa na wewe upo.

Wassira, usisahaukuwa baada ya mahojiano yako na Kibanda, viongozi wa CCM walikukabidhi kwa AmosMakala ili awe anafanya mawasiliano nawe ya mara kwa mara kabla hujarejea rasmiCCM. Wassira unaijua hali ya mfuko wako ilivyokuwa wakati huo. Umesahau?

Leo baada yakuingia bungeni na kuzawadiwa uwaziri, unahoji Kibanda ni nani? Wassira! WeweWassira ambaye sisi wachokonozi tumetunza mizigo ya faili zako.

Wassira, Kibandaunayehoji ni nani, ndiye uliyekutana naye Dodomakwa rafiki yangu rais Kikwete miaka ile unaanza kutizamika kidogo kuwa na weweni mtu.

Ulikutana naKibanda akiwa na mwandishi mwenzake, Muhingo Rweyemamu ambaye sasa ni Mkuu waWilaya, naamini unaijua wilaya anayoiongoza. Kibanda na Rweyemamu walikwendakwa rafiki yangu rais Kikwete kufanya naye mahojiano. Wewe uliwakuta hapo,wakati huo ndiyo umepata gari, Land Cruiser nyeupe ya kizamani. Mlisalimiani.

Wassira, Kibandandiye aliyeshitakiwa mahakamani kwa uchochezi. Kisa uhariri mkuu wake!Mwandishi wa makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi siyo yeye, mhariri wa makalasiyo yeye, mhariri siyo yeye, ni Mhariri Mtendaji. Sijui kama hapo unanielewa.

Aidha, mtu huyuKibanda, ndiye aliyetaka kuuawa kwa kusababishiwa ajali ya gari mwaka jana,lakini taarifa za kusudio la kumuua zilivuja kabla.

Kibanda ndiyealiyekuwa akiandika habari zako ukiwa bungeni na sasa yuko nchini Afrika Kusinianatibiwa, baada ya kuumizwa na watu fulani wanaodaiwa kuwa na wewe karibulakini wewe unakataa kuwa hawawezi kumuumizwa kwa sababu yeye Kibanda ni nani?

Wassira, au kama unavyoitwa na wengine Tyson, huyo ndiye AbsalomKibanda.

MTANZANIA
 
If a poor man is given an opportunity he thinks he has it all Wassira remember where you are coming from
 
Mengine unasoma,unatuliza kichwa kwa mda then unatafakali na kisha unachangia.............Ngoja wassira akune kichwa kwanza na badae vijana wake utawaona hapa
 
Jamaa alichoka kwelikweli huyu mzee usipime, sasa anapendeza mpaka anapigiwa kampeni
na ndugu zake ati naye awe Rais wa TZ (aaaah........ Jamani). Akichoka tena baada ya
mwaka 2015 lazima atamjua Ndugu Kibanda ni nani.
 
Wasira usisahau mbachao kwa msaala upitao, Haya mambo hayoo hadharani ipo siku mtadaiwa maumivu ya Kibanda
 
...aisee huyu Wasira simshangai hata watoto wake waliojiunga na CHADEMA aliwakana,kulipa fadhila ni adhabu mbaya sana..
 
Mengine unasoma,unatuliza kichwa kwa mda then unatafakali na kisha unachangia.............Ngoja wassira akune kichwa kwanza na badae vijana wake utawaona hapa

mkuu hawana chakuwambia wa tz

duh Amakweli nimekubali uzee siyo busara wassira unasitahili kuchapwa fimbo kumi asubuhi na jioni kumi kwa muda wa siku 360 nadhani zitapunguza makali ya ulimi wako kama ndivyo basi usiwaze sana juwa tu kuwa ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga.
Nikukumbushe tu kuwa mwenye jina lako la utani tyson je adi sasa anaweza kupigana makonde yake ya awali sasa wassira ukitaka kujuwa unako kwenda muulize anaye tokea hko na kama hutuwi siasa milele haina dhamana duniani wako wapi wana siasa walio kuwa na maneno ya dharau kama wewe yupo wapi aliye simama kwa mbwembwe na kutuambia tutakula nyasi ndege lazima inunuliwe bdo kdogo atashikwa pabaya kaulize na hurudi bungeni chamoto utakiona Tafakari chukuwa hatuwa
 
Watu wamelewa madaraka......nahamu 2015 iwe kesho...
 
Daaah.............yaani hii ni sawa na kumchukua house girl kisha siku moja mkikosana anatamka mbele ya mkeo ndo maana ulinilala tena kwenye tiqo loh.............Aibuuuuuuuuuuuuuu
 
NikukumbusheWassira, mwaka 2003, wakati unahaha kujiunga na CCM, ulifunga safari kutokaunakokujua, ulisafiri kwa daladala, ukashuka Kinondoni Makaburini, mvua ikiwainanyesha, ukakanyaga kwa mguu kutoka hapo hadi Kenyatta Drive, Nyumba namba10.

Ulifika ukiwahutamaniki, umelowa chapa chapa, ulikutana na Kibanda, akakufanyia mahojianoambayo uliyatumia kujenga hoja kuwa rais wa Tanzaniasiyo lazima atoke Zanzibar.Ni mahojiano hayo baina yako na Kibanda, ambayo yalikusaidia kuanza kufahamikamiongoni mwa wachambuzi wa mambo kuwa na wewe upo.
Nadhani mhusika akisoma hapo kwenye red atatoa machozi ya uchungu.
 
Unamwandikia Masatu Wasira huyu ninayemfahamu mimi au Mwingine ? Huyo Mzee mbona hajitambui siku nyingi sana ! wala hawezi kukuelewa , Amelewa madaraka .
 
Kwani wewe huoni hata chemistry ya uumbaji wake haiko sawa?ukimuangalia kafanana na kiumbe gani?hata akili zake ziko kama hicho kiumbe!
 
Wasira amepata uwaziri sasa anadiriki kuwatukana Watanzania? Kweli ni bora kulewa mwili lakini sio kulewa madaraka.
 
WASIFU wa watu wakubwa hutolewa na watu wadogo. Kiongozianapochaguliwa wasifu wake huandikwa au kusomwa na watu walio chini yake, iliwaliomchangua kuwaongoza ambao ni watu wadogo kwake, wamfahamu vema.

Huu ni utaratibuwa kawaida kabisa na unatumika karibu duniani kote. Ndivyo ilivyokuwa kwarafiki yangu, Rais Jakaya Kikwete na wale waliomtangulia Ikulu. Na imekuwahivyo kwa watu wengine wakubwa.

Kwa kufuatautaratibu huo huo, ninaandika kwa mbwembwe zote za kichokonozi wasifu waAbsalom Kibanda, mtu mkubwa sanahapa nchini ambaye watu wadogo wa aina ya Steven Masatu Wassira, hawamfahamu!Ninaandika wasifu huu kwa lugha adhimu ya kichokonozi, ili Wassira amueleweKibanda vizuri.

Nieleweke hapakuwa ukubwa ninaouzungumzia siyo wa nyama za mwilini, huo hauna maana sana kwa sababu hatasambusa zilizonona zimetengenezwa kwa nyama. Ninachomaanisha ni ukubwa wawadhifa.

NinakuandikiaWassira wasifu wa Absalom Kibanda, ili siku nyingine usihoji ni nani. Ninatakaufahamu kuwa Kibanda ni mtu mkubwa, maarufu na anayeheshimika sana hapa kwetu na hata kwa wenzetu.

Wassira,ninakuandikia wasifu wa mwandishi anayeheshimiwa na wakubwa kiasi cha heshimahiyo kupitiliza na kuwa woga. Wapo wakubwa wenzie wanaomuogopa. Wassira,Kibanda anaogopwa na wakubwa na wanamtambua.

NinakuandikiaWassira wasifu wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania,ambao nao ni watu wakubwa pia, hivyo ili kuwa mkubwa wao ni lazima uwe mkubwakweli kweli kama alivyo Kibanda.

Wassira, ninakuandikiawasifu wa Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd.Ninakuandikia wasifu wa mwalimu na bosi wa wachokonozi, watu adimu sana kupatikana hapaduniani, hivyo kuwa mwalimu au bosi wao shurti nawe uwe wa aina hiyo.

Ninafanya hivi kwasababu yako Wassira, mtu mdogo kiwadhifa usiyemfahamu mtu mkubwa anayeheshimiwana wakubwa. Ninakuandika kukusaidia wewe Wassira umfahamu kiongozianayeheshimiwa na wengi wenye akili, ambao kamwe hawawezi kuhoji Kibanda ninani kama ulivyofanya wewe!

Ninaanza; Wassira,sina sababu ya kukujuza Kibanda alizaliwa wapi, baba na mama yake ni akinanani, ni mtoto wa ngapi kuzaliwa na anao ndugu wangapi aliozaliwa nao tumbomoja, kwa sababu sikuamini sana.Siku nikikuamini nitafanya hivyo.

Muhimu kwako kujuani kwamba, Kibanda sasa ana umri wa Miaka 47. Ni mhariri mwenye nguvu kati yawachache waliopata kutokea hapa nchini. Ni mchambuzi mahiri wa masuala ya siasana amekuwa mshauri na mkufunzi kwa muda wa miaka ipatayo 19 sasa. Kwa sababuhiyo anaheshimika na kufahamika sana.

Wassira, Kibandani Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania. Nafasi ambayo aliipatakatika uchaguzi wa 2010, baada ya kuwabwanga waandishi wengine nguli kwelikweli waliokuwa wakiwania nafasi hiyo katika uchaguzi ambao haukuwa na uchakachuajiwa kura kama ule ambao wewe unaujua.

Kwa nafasi hiyo,Kibanda anaongoza watu wenye akili nyingi, wana utaalamu ambao bosi wako,rafiki yangu Rais Jakaya Kikwete anawaheshimu kupindukia, kwa sababu anatambuamchango wao kwake uliofanikisha ndoto yake ya miaka kumi ya kuwa Rais wa Tanzania.

Wassira, Kibandani mwanzilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania na kabla ya kuchaguliwakuwa Mwenyekiti, alikuwa akikaimu nafasi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Wassira,ninapokuandikia wasifu wa mtu huyu mkubwa, nataka uwe unaulinganisha na ule wakwako ili uone jinsi mlivyo tofauti. Nataka utambue kuwa kwa wasifu wake,unastahili kumuheshimu na kumtambua. Ukifanya hivyo, itakusaidia sana katika kipindi hikicha kuelekea mwaka 2015.

Kibanda amekuwaMhariri Mtendaji Kampuni ya Free Media Ltd, inayochapisha gazeti la TanzaniaDaima na Sayari kwa muda wa miaka sita, tangu mwaka 2006 hadi mwaka janamwishoni. Nadhani unalijua vema gazeti hili.

Ni Mkurugenzi Mkuuwa Kampuni ya Leap Media Management Ltd, inayochapisha Jarida pekee la siasalinaloitwa Umoja, ambalo hutoka mara moja kwa mwezi, jarida hili ni mithili yamajarida makubwa duniani kama Time, News Weekna mengine.

Amekuwa mwandishiwa habari tangu mwaka 1992, amefundisha masomo ya Histori na ‘Literature’katika Shule ya Sekondari Shaaban Robert kati ya mwaka 1995 hadi 1996, kablahajajiunga na Kampuni ya Habari Corporation Ltd mwaka 1996. Hivyo tambua kuwaanao uwezo mkubwa wa kumwaga ngeli. Akiwa na wazungu anakuwa mzungu, akiwa nawaswahili anakuwa kama walivyo.

Katika umri wakowa utu uzima Wassira, ninaamini kumbukumbu bado unazo hivyo unakumbuka kwambawakati huo, Habari Corporation ilikuwa Kampuni yenye nguvu kubwa miongoni mwakampuni zilizokuwa zikimiliki vyombo vya habari, hivyo kujiunga nayo halikuwajambo rahisi.

Kibanda, akiwa navijana wenzake wenye akili, Marehemu Danny Mwakiteleko na Jesse Kwayu ambayesasa ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe, walinyakuliwa na HabariCorporation baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampunihiyo, Jenerali Ulimwengu, kuutamani uwezo wao wa kazi na hasa akili za vijanahao.

Wassira sijuikwako wewe ni wangapi wenye akili waliowahi kutamani akili na uwezo wako wakazi hadi wakaamua kukufuata ufanye nao kazi.

Siyo jambo rahisikuandika wasifu wa mtu wa aina ya Kibanda kwa ukamilifu pasipo kuacha nyamanyama za kuunenepesha kwa sababu una mambo mengi mno. Kwa sababu hiyo,ninaandika kwa uchache yale yanayofahamika na wengi ambayo wewe Wassira unadaikuwa huyajui wakati ni uongo.

Wassira, Desemba1999 Kibanda alijiunga na Kampuni ya Media Communication Ltd, sasa MwananchiCommunications Ltd, akiwa mwandishi mwandamizi katika jarida la siasa la WIKIHII. Alikuwa na jukumu kubwa la kuanzisha gazeti la Kiswahili la Mwananchi.

Wakati Kampuni yaNation Media Group kutoka Nairobi iliponunuahisa za Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Kibanda alikuwa mwandishi wakwanza kutoka Tanzania,ambaye aliweza kuandika makala katika gazeti la Nation la nchini Kenya na The Monitor la Uganda kwalugha ya fasaha ya kimombo, hivyo maandishi yake yamekuwa yakisomeka nje yanchi tangu miaka hiyo.

Akifanya kazikatika gazeti la Mwananchi, alishika nyadhifa mbalimbali za Mhariri wa Makala,Mhariri wa Biashara na Mhariri wa gazeti la Mwananchi Jumapili, ambalo wakatiakiliongoza, ndilo lililokuwa likishika nambari wani katika mauzo hapa nchini.

Ni wakati huoWassira, ukiwa unatangatanga katika vyama vya siasa, ukiwa umechoka sana kimaisha, mwaka2003, ukiwa mwanachama wa Chama cha NCCR- Mageuzi uliyekuwa ukibembelezakuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulikutana na Kibanda, akakuinua kutoka kwenyeuhohehahe uliokuwa ukikuandama.

Wassira, kwa niniunakuwa msahaulifu? Au ni ulevi wa madaraka. Umepata sasa umesahau shidaulizokuwa nazo na kwamba Kibanda ni mmoja wa watu waliokunusuru katika dhikiulizokuwa nazo.

NikukumbusheWassira, mwaka 2003, wakati unahaha kujiunga na CCM, ulifunga safari kutokaunakokujua, ulisafiri kwa daladala, ukashuka Kinondoni Makaburini, mvua ikiwainanyesha, ukakanyaga kwa mguu kutoka hapo hadi Kenyatta Drive, Nyumba namba10.

Ulifika ukiwahutamaniki, umelowa chapa chapa, ulikutana na Kibanda, akakufanyia mahojianoambayo uliyatumia kujenga hoja kuwa rais wa Tanzaniasiyo lazima atoke Zanzibar.Ni mahojiano hayo baina yako na Kibanda, ambayo yalikusaidia kuanza kufahamikamiongoni mwa wachambuzi wa mambo kuwa na wewe upo.

Wassira, usisahaukuwa baada ya mahojiano yako na Kibanda, viongozi wa CCM walikukabidhi kwa AmosMakala ili awe anafanya mawasiliano nawe ya mara kwa mara kabla hujarejea rasmiCCM. Wassira unaijua hali ya mfuko wako ilivyokuwa wakati huo. Umesahau?

Leo baada yakuingia bungeni na kuzawadiwa uwaziri, unahoji Kibanda ni nani? Wassira! WeweWassira ambaye sisi wachokonozi tumetunza mizigo ya faili zako.

Wassira, Kibandaunayehoji ni nani, ndiye uliyekutana naye Dodomakwa rafiki yangu rais Kikwete miaka ile unaanza kutizamika kidogo kuwa na weweni mtu.

Ulikutana naKibanda akiwa na mwandishi mwenzake, Muhingo Rweyemamu ambaye sasa ni Mkuu waWilaya, naamini unaijua wilaya anayoiongoza. Kibanda na Rweyemamu walikwendakwa rafiki yangu rais Kikwete kufanya naye mahojiano. Wewe uliwakuta hapo,wakati huo ndiyo umepata gari, Land Cruiser nyeupe ya kizamani. Mlisalimiani.

Wassira, Kibandandiye aliyeshitakiwa mahakamani kwa uchochezi. Kisa uhariri mkuu wake!Mwandishi wa makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi siyo yeye, mhariri wa makalasiyo yeye, mhariri siyo yeye, ni Mhariri Mtendaji. Sijui kama hapo unanielewa.

Aidha, mtu huyuKibanda, ndiye aliyetaka kuuawa kwa kusababishiwa ajali ya gari mwaka jana,lakini taarifa za kusudio la kumuua zilivuja kabla.

Kibanda ndiyealiyekuwa akiandika habari zako ukiwa bungeni na sasa yuko nchini Afrika Kusinianatibiwa, baada ya kuumizwa na watu fulani wanaodaiwa kuwa na wewe karibulakini wewe unakataa kuwa hawawezi kumuumizwa kwa sababu yeye Kibanda ni nani?

Wassira, au kama unavyoitwa na wengine Tyson, huyo ndiye AbsalomKibanda.

MTANZANIA

habari hii yote naweza ipunguza na kuwa Kibanda na wassira ni wapuuzi tuu walioamua kuwa na project ya kujenga umaarufu nje ili wapate nafasi CCM.Hakuna tofauti na majambazi kulipana.
 
WASSIRA Vs KIBANDA

Sokwe wetu ni salama kuliko Kibanda?​

Msomaji Raia

Toleo la 291
24 Apr 2013

VIROJA ndani ya Bunge vinaendelea huko Dodoma. Minyukano imeshamiri na kuzua gumzo kila kona. Minyukano ya mabunge yote duniani huwa ni kati ya upande wa serikali na upande wa wabunge wote bila kujali itikadi zao.
Yaani wabunge wote wakiwatetea wananchi na kuisimamia serikali huku serikali ikijilinda na kujitetea mbele ya wabunge wote. Mnyukano wa namna hii huvutia na kutia hamu kuuangalia na hata kufuatilia mijadala mbalimbali baina ya wabunge na serikali.

Mnyukano kati ya wabunge wa chama tawala dhidi ya wabunge wa vyama vingine ndani ya bunge huwa unatokea lakini hauvutii katika mabunge yaliyostaarabika. Hii ni kwa sababu mnyukano huo una maslahi ya vyama na itikadi zao. Si wakati wote maslahi ya vyama yakawa maslahi ya wananchi na taifa. Huu ndio mnyukano unaoonekana zaidi katika bunge letu.

Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiiponda serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), wabunge wa CCM wakitukana na kuwapiga vijembe wabunge wa CHADEMA. Refa wa mnyukano huu ni Spika na Naibu wake ambao nao wanatuhumiwa kulalia upande wa chama tawala.

Wiki iliyopita wabunge wa upinzani waliibana Serikali dhidi ya kile kinachodaiwa ni tabia ya Serikali kutumia vyombo vya dola kuwateka na kuwatesa baadhi ya wananchi wanaofikiriwa kuwa ni hatari kwa maslahi ya Serikali na chama tawala. Mnyukano ulipokuwa mkali, Serikali kwa kutumia kiti cha Spika na wingi wa wabunge wa chama tawala, ililazimisha kambi ya Upinzani kufuta baadhi ya kurasa za hotuba iliyosheheni tuhuma dhidi ya Serikali.
Hata baada ya kubaini kuwa hatua hiyo haijasaidia sana, jitihada zilifanyika kuwatumia baadhi ya mawaziri waandamizi kutoa maelezo ya kuilinda Serikali dhidi ya tuhuma hizi mbaya za kuteka na kutesa wananchi wake. Mawaziri Profesa Mark Mwandosya na Stephen Wassira walifanya kazi hiyo.

Hilo liliposhindikana ndipo kiti cha Spika kilipoamua kuwatoa nje kwa nguvu wabunge sita wa chama cha Upinzani. Haya yote niliyoyataja hapo juu yanahitaji uchambuzi wa pekee lakini makala hii ijikite katika kauli aliyoitoa Waziri Wassira kuhusu kutekwa na kuteswa kwa mwanahabari Absalom Kibanda.

Mzee Wassira anakana katakata kuwa Idara ya Usalama wa Taifa haihusiki na utekaji na utesaji wa namna hii. Sina tatizo na kanusho hili na sikutegemea aseme idara hiyo inahusika. Nina shida na matamshi yake kuwa “kwani Kibanda ni nani hadi atekwe?”. Nina shida pia na kauli yake iliyoashiria kuwa kama angekuwa Mbowe (Freeman, Mwenyekiti wa CHADEMA) au Dk. Slaa ( Wilbroad, Katibu Mkuu wa CHADEMA) hilo wenlingewezekana na kueleweka kwa sababu hao ni watu wakubwa.

Kwangu mimi nilielewa kwa yakini kuwa kama Kibanda angekuwa ni Mbowe au Dk. Slaa kungekuwa na sababu ya Idara ya Usalama kuwateka na kuwatesa. Kimsingi, mzee Wassira anatuhakikishia kuwa idara hiyo inaweza kuteka na kutesa raia na hata kuwaua ilimradi wawe ni watu wakubwa au wa hatari kwa maslahi ya kisiasa ya watu walio vipenzi wa idara hiyo. Kauli ya Wassira ikikubalika, italiweka Taifa mashakani na kuiweka Serikali kuwa mateka wa idara hiyo badala ya Serikali kuwa mateka wa wananchi walioiweka madarakani.

Katiba ya Jamhuri yetu bila kigugumizi chochote inatoa uhuru wa kuishi. Aidha inatoa uhuru wa kujieleza, kutoa maoni, kushiriki, kuabudu na kulindwa bila kigugumizi chochote. Chini ya mamlaka nyingine zilizo chini ya serikali yetu, sheria nyingine zimetungwa kulinda viumbe hasa vile vilivyo hatarini kutoweka. Ndiyo maana wanyama kama sokwe mtu, faru, kakakuona, mbwa mwitu na aina fulani za ndege na viumbe wa majini wanalindwa kwa kutumia fedha na raslimali nyingi. Wanyama hawa wanatunzwa katika maeneo maalumu tengefu na ni marufuku kuwawinda au hata kuwaua kwa bahati mbaya.

Hata pale inapotokea wanyama kama sokwe mtu na wengine walio katika hatari ya kutoweka, wakavuka mipaka yao ya makazi na kuingia katika makazi ya watu na kufanya uharibifu, hairuhusiwi kwa mtu yeyote kujichukulia sheria mkononi kuwadhuru hao wanyama. Adhabu kali inaweza kuchukuliwa dhidi ya mtu huyo.

Watu wengi na hasa wakulima wanalalamika sana dhidi ya Serikali pale Serikali inaposhindwa hata kuwafidia dhidi ya
uharibifu unaofanywa na wanyama kama hao wanapoingia katika makazi ya watu. Wanavijiji wanaoishi kando kando ya mbuga za wanyama wana tatizo kubwa la namna hii.

Ukienda katika wilaya za Bunda, Serengeti, Ngorongoro, Hai, Rombo na Arusha utasikia watu wanalalamika kuwa uhai wa wanyama unaheshimika kuliko uhai wa watu na mimea. Wananchi wanaoishi kandokando ya hifadhi ya Gombe huko Kigoma wamewahi kulalamika kuwa sokwe ni tishio hasa kwa watoto wadogo wa kike wanaonusurika hata kubakwa na wanyama hao wanaopendwa sana na watalii.

Hii inaonyesha kuwa uhai wa wanyama na viumbe wengine wanavyoweza kuonewa na wanadamu, unalindwa vema na Katiba ya nchi yetu. Uhai wa binadamu una thamani sana na ndiyo maana hata Katiba yetu inatamka wazi kuulinda na kuuthamini uhai huo bila kujali hali ya mtu kiuchumi, jinsia, rangi yake, itikadi yake na hata kabila lake. Chini ya tamko hili la Katiba, hata vibaka, wezi, wabakaji, mafisadi na hata wauaji wana haki ya kulindwa uhai wao. Kazi ya kuulinda uhai wa raia ni ya Serikali na vyombo vyake. Wanaolindwa ni raia bila kujali kama wanaipinga au kuiunga mkono Serikali iliyo madarakani.

Ni kwa sababu hiyo matamshi ya mzee Wassira kuhusu utekaji na utesaji wa Kibanda yameacha huzuni kubwa miongoni mwa Watanzania wapenda haki na amani. Udogo na u-kawaida wa Kibanda kisiwe kigezo cha kupuuza mateso aliyoyapata na ulemavu alioachiwa na waliomteka na kumtesa.

Hata kama Kibanda angekuwa ameandika makala au kutoa maoni yanayoiudhi Serikali bado Serikali hiyo ina wajibu wa kumlinda Kibanda na kumhakikishia usalama. Kitendo hicho cha Kibanda kuandika makala mbaya (kama ipo) kinapaswa kufananishwa na pale mnyama anayelindwa na sheria anapoingia katika makazi ya watu.

Si ruhusa kwa watu kumuua mnyama huyo. Jitihada zitafanyika na maafisa wa wanyamapori kumuondoa bila kumdhuru. Hata leo hii tungekuta mathalani, sokwe ametoka Gombe na kukalia kiti cha Waziri Mkuu ndani ya ukumbi wa Bunge, jitihada zitafanyika kumwondoa kwenye kiti bila kumdhuru kwa sababu sheria ya kulinda wanyama maalumu inamhakikishia ulinzi.

Binadamu ni mmoja wa viumbe maalumu na anayetishiwa uhai wake (endangered species). Hii ndiyo sababu ya serikali zote duniani kuweka ulinzi maalumu kikatiba na kisheria kumlinda binadamu. Inapofika waziri wa serikali anamthamini sana sokwe kuliko binadamu inatupa mashaka. Ni nani atawalinda raia dhidi ya serikali yao endapo uhai wao utaanza kuwindwa na serikali yao? Ubaguzi wa namna ya mzee Wassira kwa Kibanda unatishia uhai wa binadamu hasa pale tunapoanza kulindwa kwa madaraja na matabaka.

WASIFU wa watu wakubwa hutolewa na watu wadogo. Kiongozianapochaguliwa wasifu wake huandikwa au kusomwa na watu walio chini yake, iliwaliomchangua kuwaongoza ambao ni watu wadogo kwake, wamfahamu vema.

Huu ni utaratibuwa kawaida kabisa na unatumika karibu duniani kote. Ndivyo ilivyokuwa kwarafiki yangu, Rais Jakaya Kikwete na wale waliomtangulia Ikulu. Na imekuwahivyo kwa watu wengine wakubwa.

Kwa kufuatautaratibu huo huo, ninaandika kwa mbwembwe zote za kichokonozi wasifu waAbsalom Kibanda, mtu mkubwa sanahapa nchini ambaye watu wadogo wa aina ya Steven Masatu Wassira, hawamfahamu!Ninaandika wasifu huu kwa lugha adhimu ya kichokonozi, ili Wassira amueleweKibanda vizuri.

Nieleweke hapakuwa ukubwa ninaouzungumzia siyo wa nyama za mwilini, huo hauna maana sana kwa sababu hatasambusa zilizonona zimetengenezwa kwa nyama. Ninachomaanisha ni ukubwa wawadhifa.

NinakuandikiaWassira wasifu wa Absalom Kibanda, ili siku nyingine usihoji ni nani. Ninatakaufahamu kuwa Kibanda ni mtu mkubwa, maarufu na anayeheshimika sana hapa kwetu na hata kwa wenzetu.

Wassira,ninakuandikia wasifu wa mwandishi anayeheshimiwa na wakubwa kiasi cha heshimahiyo kupitiliza na kuwa woga. Wapo wakubwa wenzie wanaomuogopa. Wassira,Kibanda anaogopwa na wakubwa na wanamtambua.

NinakuandikiaWassira wasifu wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania,ambao nao ni watu wakubwa pia, hivyo ili kuwa mkubwa wao ni lazima uwe mkubwakweli kweli kama alivyo Kibanda.

Wassira, ninakuandikiawasifu wa Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd.Ninakuandikia wasifu wa mwalimu na bosi wa wachokonozi, watu adimu sana kupatikana hapaduniani, hivyo kuwa mwalimu au bosi wao shurti nawe uwe wa aina hiyo.

Ninafanya hivi kwasababu yako Wassira, mtu mdogo kiwadhifa usiyemfahamu mtu mkubwa anayeheshimiwana wakubwa. Ninakuandika kukusaidia wewe Wassira umfahamu kiongozianayeheshimiwa na wengi wenye akili, ambao kamwe hawawezi kuhoji Kibanda ninani kama ulivyofanya wewe!

Ninaanza; Wassira,sina sababu ya kukujuza Kibanda alizaliwa wapi, baba na mama yake ni akinanani, ni mtoto wa ngapi kuzaliwa na anao ndugu wangapi aliozaliwa nao tumbomoja, kwa sababu sikuamini sana.Siku nikikuamini nitafanya hivyo.

Muhimu kwako kujuani kwamba, Kibanda sasa ana umri wa Miaka 47. Ni mhariri mwenye nguvu kati yawachache waliopata kutokea hapa nchini. Ni mchambuzi mahiri wa masuala ya siasana amekuwa mshauri na mkufunzi kwa muda wa miaka ipatayo 19 sasa. Kwa sababuhiyo anaheshimika na kufahamika sana.

Wassira, Kibandani Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania. Nafasi ambayo aliipatakatika uchaguzi wa 2010, baada ya kuwabwanga waandishi wengine nguli kwelikweli waliokuwa wakiwania nafasi hiyo katika uchaguzi ambao haukuwa na uchakachuajiwa kura kama ule ambao wewe unaujua.

Kwa nafasi hiyo,Kibanda anaongoza watu wenye akili nyingi, wana utaalamu ambao bosi wako,rafiki yangu Rais Jakaya Kikwete anawaheshimu kupindukia, kwa sababu anatambuamchango wao kwake uliofanikisha ndoto yake ya miaka kumi ya kuwa Rais wa Tanzania.

Wassira, Kibandani mwanzilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania na kabla ya kuchaguliwakuwa Mwenyekiti, alikuwa akikaimu nafasi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Wassira,ninapokuandikia wasifu wa mtu huyu mkubwa, nataka uwe unaulinganisha na ule wakwako ili uone jinsi mlivyo tofauti. Nataka utambue kuwa kwa wasifu wake,unastahili kumuheshimu na kumtambua. Ukifanya hivyo, itakusaidia sana katika kipindi hikicha kuelekea mwaka 2015.

Kibanda amekuwaMhariri Mtendaji Kampuni ya Free Media Ltd, inayochapisha gazeti la TanzaniaDaima na Sayari kwa muda wa miaka sita, tangu mwaka 2006 hadi mwaka janamwishoni. Nadhani unalijua vema gazeti hili.

Ni Mkurugenzi Mkuuwa Kampuni ya Leap Media Management Ltd, inayochapisha Jarida pekee la siasalinaloitwa Umoja, ambalo hutoka mara moja kwa mwezi, jarida hili ni mithili yamajarida makubwa duniani kama Time, News Weekna mengine.

Amekuwa mwandishiwa habari tangu mwaka 1992, amefundisha masomo ya Histori na ‘Literature'katika Shule ya Sekondari Shaaban Robert kati ya mwaka 1995 hadi 1996, kablahajajiunga na Kampuni ya Habari Corporation Ltd mwaka 1996. Hivyo tambua kuwaanao uwezo mkubwa wa kumwaga ngeli. Akiwa na wazungu anakuwa mzungu, akiwa nawaswahili anakuwa kama walivyo.

Katika umri wakowa utu uzima Wassira, ninaamini kumbukumbu bado unazo hivyo unakumbuka kwambawakati huo, Habari Corporation ilikuwa Kampuni yenye nguvu kubwa miongoni mwakampuni zilizokuwa zikimiliki vyombo vya habari, hivyo kujiunga nayo halikuwajambo rahisi.

Kibanda, akiwa navijana wenzake wenye akili, Marehemu Danny Mwakiteleko na Jesse Kwayu ambayesasa ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe, walinyakuliwa na HabariCorporation baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampunihiyo, Jenerali Ulimwengu, kuutamani uwezo wao wa kazi na hasa akili za vijanahao.

Wassira sijuikwako wewe ni wangapi wenye akili waliowahi kutamani akili na uwezo wako wakazi hadi wakaamua kukufuata ufanye nao kazi.

Siyo jambo rahisikuandika wasifu wa mtu wa aina ya Kibanda kwa ukamilifu pasipo kuacha nyamanyama za kuunenepesha kwa sababu una mambo mengi mno. Kwa sababu hiyo,ninaandika kwa uchache yale yanayofahamika na wengi ambayo wewe Wassira unadaikuwa huyajui wakati ni uongo.

Wassira, Desemba1999 Kibanda alijiunga na Kampuni ya Media Communication Ltd, sasa MwananchiCommunications Ltd, akiwa mwandishi mwandamizi katika jarida la siasa la WIKIHII. Alikuwa na jukumu kubwa la kuanzisha gazeti la Kiswahili la Mwananchi.

Wakati Kampuni yaNation Media Group kutoka Nairobi iliponunuahisa za Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Kibanda alikuwa mwandishi wakwanza kutoka Tanzania,ambaye aliweza kuandika makala katika gazeti la Nation la nchini Kenya na The Monitor la Uganda kwalugha ya fasaha ya kimombo, hivyo maandishi yake yamekuwa yakisomeka nje yanchi tangu miaka hiyo.

Akifanya kazikatika gazeti la Mwananchi, alishika nyadhifa mbalimbali za Mhariri wa Makala,Mhariri wa Biashara na Mhariri wa gazeti la Mwananchi Jumapili, ambalo wakatiakiliongoza, ndilo lililokuwa likishika nambari wani katika mauzo hapa nchini.

Ni wakati huoWassira, ukiwa unatangatanga katika vyama vya siasa, ukiwa umechoka sana kimaisha, mwaka2003, ukiwa mwanachama wa Chama cha NCCR- Mageuzi uliyekuwa ukibembelezakuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulikutana na Kibanda, akakuinua kutoka kwenyeuhohehahe uliokuwa ukikuandama.

Wassira, kwa niniunakuwa msahaulifu? Au ni ulevi wa madaraka. Umepata sasa umesahau shidaulizokuwa nazo na kwamba Kibanda ni mmoja wa watu waliokunusuru katika dhikiulizokuwa nazo.

NikukumbusheWassira, mwaka 2003, wakati unahaha kujiunga na CCM, ulifunga safari kutokaunakokujua, ulisafiri kwa daladala, ukashuka Kinondoni Makaburini, mvua ikiwainanyesha, ukakanyaga kwa mguu kutoka hapo hadi Kenyatta Drive, Nyumba namba10.

Ulifika ukiwahutamaniki, umelowa chapa chapa, ulikutana na Kibanda, akakufanyia mahojianoambayo uliyatumia kujenga hoja kuwa rais wa Tanzaniasiyo lazima atoke Zanzibar.Ni mahojiano hayo baina yako na Kibanda, ambayo yalikusaidia kuanza kufahamikamiongoni mwa wachambuzi wa mambo kuwa na wewe upo.

Wassira, usisahaukuwa baada ya mahojiano yako na Kibanda, viongozi wa CCM walikukabidhi kwa AmosMakala ili awe anafanya mawasiliano nawe ya mara kwa mara kabla hujarejea rasmiCCM. Wassira unaijua hali ya mfuko wako ilivyokuwa wakati huo. Umesahau?

Leo baada yakuingia bungeni na kuzawadiwa uwaziri, unahoji Kibanda ni nani? Wassira! WeweWassira ambaye sisi wachokonozi tumetunza mizigo ya faili zako.

Wassira, Kibandaunayehoji ni nani, ndiye uliyekutana naye Dodomakwa rafiki yangu rais Kikwete miaka ile unaanza kutizamika kidogo kuwa na weweni mtu.

Ulikutana naKibanda akiwa na mwandishi mwenzake, Muhingo Rweyemamu ambaye sasa ni Mkuu waWilaya, naamini unaijua wilaya anayoiongoza. Kibanda na Rweyemamu walikwendakwa rafiki yangu rais Kikwete kufanya naye mahojiano. Wewe uliwakuta hapo,wakati huo ndiyo umepata gari, Land Cruiser nyeupe ya kizamani. Mlisalimiani.

Wassira, Kibandandiye aliyeshitakiwa mahakamani kwa uchochezi. Kisa uhariri mkuu wake!Mwandishi wa makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi siyo yeye, mhariri wa makalasiyo yeye, mhariri siyo yeye, ni Mhariri Mtendaji. Sijui kama hapo unanielewa.

Aidha, mtu huyuKibanda, ndiye aliyetaka kuuawa kwa kusababishiwa ajali ya gari mwaka jana,lakini taarifa za kusudio la kumuua zilivuja kabla.

Kibanda ndiyealiyekuwa akiandika habari zako ukiwa bungeni na sasa yuko nchini Afrika Kusinianatibiwa, baada ya kuumizwa na watu fulani wanaodaiwa kuwa na wewe karibulakini wewe unakataa kuwa hawawezi kumuumizwa kwa sababu yeye Kibanda ni nani?

Wassira, au kama unavyoitwa na wengine Tyson, huyo ndiye AbsalomKibanda.

MTANZANIA

Ma CCM bwana kila kukicha yanachapwa .Haya Wassira na genge lako njooni mjiteteee hapa .Kama Nchimbi jana ana hoji juunya Chadema kupewa Nchi .Eti tukiwapa Nchi hakika I was amazed uwezo wa huyu jamaa
 
Mkuu Tunduruboy, political life story ya smw ni story ambayo hata kijana kizazi kipya aliyekata tamaa anaweza kupata inspiration tumaini jipya kuwa usikate tamaa in life..Wassira huyu ni jembe aliwahi kupanda sana na kweli akashuka sana hata pengine kunyeshewa mvua akielekea kwa Mkuu Kibanda, sio hilo tu, na pia alishafanya hata biashara ya fish-Namanga.Ila kwa kutokukata tamaa, akarudi, in english wanasema, alifanya comeback katika siasa ya Tanzania, na haya sishangai ni because hivi sasa yuko juu in CCM. Kwa vijana wasiokuwa na ajira au tumaini, au vijana waliomaliza form four usahishaji umewaleta division zero--nasema: "dont give up" Amini si mwisho. Muige kwa babu yenu mzee Wassira "kwa kichwa", "sio kwa ufisadi' hajanunua mtu na akarudisha ramani yake binafsi iliyopotea katika kilele cha siasa Tanzania..

Matatizo yapo mengi Tanzania, Swala la Kibanda linatumika kuchanganya watu kwa maksudi sababu alichosema juu ya Kibanda alikuwa haongei kama yeye Wasira, aliongea kama msemaji wa Serikali ikizushiwa mambo mengi naye kama Waziri wa Mahusiano, refuting kwa kutumia commonsense, akihoji mantiki for the State of TZ to wage a war on Mr. Kibanda. Why? Yeye kumjua au kutomjua binafsi Abasalom Kibanda sio Mastakabali wa Nchi kihivyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wa sasa, Bwana John Kerry, aliwahi kugombea Urais wa Marekani mwaka 2004 dhidi ya George W. Bush, Rais wa 43 wa USA. Kwa ustadi mkubwa, wakati wa kampeni, aliandamwa na mbinu chafu za kubadilisha maneno, upotoshwaji wa matamshi au hoja mpwitompwito za aina ya "Kibanda ni nani?" dhidi ya Kerry hadi kupoteza uchaguzi ule na huku pengine angewafaa Wamarekani kuliko George W. Bush na Vita zake Iraq zilizoharibu Uchumi, Rais Obama asingempa John Kerry kazi kubwa aliyonayo kama kweli ni mtu asiyefaa kiuongozi

Nasi tunaelekea Uchaguzi 2015, watanzania kama wachina tutacopy and paste mbinu nyingi tupate ili Nani awe nanhii wetu. Bado guys.CHUKUENI POPCORN HII KIBANDA MOVIE NI TRELA TU, SINEMA YENYWE HAIJAANZA
 
Kwani wewe huoni hata chemistry ya uumbaji wake haiko sawa?ukimuangalia kafanana na kiumbe gani?hata akili zake ziko kama hicho kiumbe!
kweli aise tena wanyama hawa wanadhalau sana hasa kwa wanawake ***we
 
Back
Top Bottom