Wassira kama Tyson, aandaa kuumiza Taifa aingie Ikulu!

Wassira kama Tyson, aandaa kuumiza Taifa aingie Ikulu!

Hon.MP

Senior Member
Joined
Jul 15, 2012
Posts
153
Reaction score
86
WASSIRA KAMA TYSON AANDAA KUUMIZA TAIFA AINGIE IKULU!

Kama alivyofanya wajina wake Tyson kwa kumngáta sikio Evander katika mpambano wa 1997, Mzee Stephen Wassira, naye anajiandaa kutumia meno yake aliyonayo kungáta kwa nguvu zote ilimuradi atangazwe mshindi katika kinyangányoro cha Urais 2015. Andalio la faulo hiyo liko katika kukusanya fedha nyingi za kutosha kwa ajili ya kampeni yake hata kama Taifa litakuwa linaumia kwa maumivu makali ya kungátwa. Habari ndio hii:-

1. Kwa kushirikiana naWaziri mfukuzwa-William Ngeleja pamoja na Mmarekani David. Forley (CEO- Blackstone Energy Partners) wameanza kufanya kazi kubwa ya ushawishi World Bank na Ikulu yetu ili kuilazimisha TANESCO kuingia mkataba wa kifisadi na Kampuni ya Sithe Global Power LLP Unit ambayo inamilikiwa kwa 80% na Kampuni giant la Kibeberu la Kimarekani Blackstone Group amabalo pia lilihusika katika skandali kubwa ya Enron. Sithe Global Power ambapo Kijana wa Wassira anafanya kazi wanaandaa kuzalisha umeme (Ruhudji Hydropower Plant- Iringa) kuzalisha yapata Megawatt 360. Mwanzoni tangu mradi huu uanze ilikuwa katika makubaliano ya thamani ya USD Milioni 200 lakini sasa Tyson anajiandaa kungáta kwa kulazimisha iwe USD Bilioni 1.5. Habari za kuaminika zinaonyesha kuwa endapo watafanikiwa; Tyson ameahidiwa kupewa mchango wa USD Milioni 2 kama kianzio cha mchango wa Kampeni ya Urais na mwendelezo wa mgao wake kama kawaida akifaulu kuingia Ikulu. Wakati Ngeleja yeye kaahidiwa kupewa share 10% katika Kampuni hiyo. So far kianzio cha USD 500,000 kimetolewa kwao kwa ajili ya kuhakikisha kuwa ushawishi unafanyika kwa namna yoyote ili mpango huu utimie.

2. Tyson tena kwa kushirikiana na ndg. Haruma Masebu wa EWURA wanatumia nguvu zote ili Kampuni iliyoingiza nchini mafuta yaliyo chini ya kiwango yakubalike na kuendelea kutumiwa nchini kinyume na agizo la EWURA. Inasemekana kuwa hapo Tyson, Masebu na yeyote atakayesaidia wameahidiwa dau la USD Milioni 1. Ikumbuke kuwa EURA (na Wizara) imeshatoa agizo kuyakataa hayo mafuta kuwa hayafai. Tyson hapo anaamua tena kungáta injini za Watanzania zitakazotumia mafuta hayo mabaya ukiachilia mbali uchafuzi wa mazingira utakaosababishwa, kisa mzee huyu akusanye fedha ya kutosha katika kampeni!

Je, Tyson anafanya haya kwa kujiaminisha kung'ata kwa meno ya aina gani kutekeleza azima yake:

1. Ukaribu wake na Rais wetu na Ofisi yake (iliyopachikwa) iko ndani ya ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) na anakaribishwa kila mahala alipo Rais yaani role yake imekuwa ni zaidi hata ya Makamu wa Rais na hata Waziri Mkuu!

2. Zile kura 2,135 zilizompa kuongoza katika kinyangányiro U-NEC wa CCM zimempa bichwa kichwa kikubwa (bichwa) anadhani kuwa yeye ndiye kipenzi cha wengi (ndani ya CCM), na mwenye akili nyingi, shujaa na mwenye mikakati madhubuti ya kuudhibiti upinzani!

3. Urafiki wake na baadhi ya Viongozi na Mafisadi ndani ya nchi akiwemo mfukuzwa Ngeleja na wenzake ambao wanatumia mbinu zote za kuwashawishi Viongozi wa juu wa Serikali, Mawaziri, Wabunge na Watumishi wasio na huruma na Taifa letu. Aidha katika kulitekeleza hili vyema wameungana na wale mafisadi kuamua kuendeleza siasa za kuwachafua Watumishi wowote watakaoonekana kutetea maslahi ya nchi walioko TANESCO, EWURA na Wizara ya Nisahati na Madini.

4. Ni hakika (kama huamini tulia, tafakari na usubiri uone) kuwa kuna makubaliano ya kifamilia yalifanyika kwamba 2015 yule Kijana wa Wassira atagombea Ubunge Bunda kupitia CCM wakati Binti wa kaka yake mkubwa aitwaye Esther Wassira agombee kupitia CHADEMA. Tusiona mbali ghafla tunamshangilia sana huyu Mwanasheria kumbe ni yale mazingaombwe ya Mwanakijiji na tunaanzisha thread za kumlimganisha sijui na Ester Bulaya, na kumpa jukwaa Nkrumah Hall apande chati haraka haraka kumbe haya ndio sehemu ya meno ya kutung'ata yanayonolewa na babaye anayemezea mate magogoni!! Watanzania ni nani aliyewaroga kushangilia zile headline news za keusi-keupe eti sijui "Wassira awakana wanawe" au "Watoto wa Wassira watoa ufafanuzi / wamjibu baba yao" n.k?" Watu watachaguliwa kwa sifa zao za uongozi bora na si kwa mbinu za kifisadi!

Chochote anachopanga kufanya huyu mzee; wenye hekima na wazalendo wa nchi hii hatumkubali Stephen Wassira kutuongoza tena hata katika ngazi ya Ubunge na hatutakubali TANESCO wala EWURA kulazimishwa kukukubali upuuzi wa ama kutuingiza katika madeni makubwa ya Taifa au Wananchi kulazimishwa kutumia huduma na bidhaa zilizo chini ya viwango vinavyokubalika eti kwa sababu huyu mzee anatembeza bakuli kifisadi kujiandaa kuingia Ikulu ambako hakika hataingia hata kwa madunguli!
 
Hawa wanaojiita vigogo wa serikali wanafanya haya maovu pasipo uzalendo kwa nchi yao kwa sababu wameshagundua muda wao wa kufungasha virago umefika hivyo wanaona maslahi yao kwa sasa ni bora kuliko maslahi ya taifa."HATA WAKOLONI WALICHUKUA MALI ZETU WAKIJUA IPO SIKU WATAONDOKA KWETU"

Hivyo basi changamoyo tuliyonayo ni kuhakikisha hawondoki na kitu. Mwl. NYERERE alisimama kidete kulejesha uhuru wa bendera jukumu tulilo nalo kwa sasa ni kuiisafisha nchi na kulejesha uhuru miongoni mwa watu ndani ya nchi yao. Wasira anafanya haya ni kwasababu anajua hana chake jimboni kwake Bunda.

B
y UPRISING ACTVIST from BUNDA.
 
Naona sasa urais umekuwa wa kuchezea sasa. Rais Kikwete kama amiri jeshi Mkuu na Mkuu wa nchi katika hotuba yako ya kufunga mwaka usiache kuongelea kwa kina yafuatayo maana ama yanatuchafulia nchi yetu au yanakuchafua wewe:

1. Hawa watu wanaoanza kujitangaza kugombea Urais wakati wewe uko madarakani na tume haijatoa ruksa za kujitangaza. Wote waliotangaza na wanaopiga kampeni wanajulikana
2. Maneno ya kibaguzi, kejeli na mashambulio yenye mielekeo ya kidini nchini
3. Maandamano ya kusini juu ya gesi
4. Mafisadi hata ndani ya chama chetu cha Mapinduzi wanaodhoofisha juhudi za watendaji waaminifu na wachapa kazi Mawizarani, Mikoani, katika Halmashauri na Taasisi mbalimbali za Umma.
 
ataaibika,ati urais kwa wassira!! AJIANGALIE asije akamwaga senti bure kama Malecela.
 
Natamani mwandishi aseme jamani hii ni ndoto tu.
Yaani bado watu kumbe hawajachoka tu kuifisadi nchi hii,inawezekana siyo huyo tu anayefanya mbinu hizo chafu.
 
mchezo wa wataka urais kutafuta pesa kwa njia zozote ili wateuliwe kugombea urais na waupate huo urais utaendelea. wengine tutawashtukia na wengne hawatashtukiwa. wengine watatangazwa hadharan wakat wengine hawatatangazwa. wakuu, NI LAZIMA TUANDAE KANUNI, SHERIA, MIONGOZO or whatever u name it AMBAZO ZITAMBANA RAIS ASIWEZE KUFISADI AKIWA MADARAKANI. wakishajua wakipata urais hawawez kufisad hawatahangaika kihvo na wahongaj hawatataka kuhonga.
 
Habari ya Wassira kugombea urais nilishaisikia kitambo nikadhani utani. Mojawapo ya watu walio nyuma ya mpango huo ni mbunge wa Tarime Mh. Nyambari Mariba Nyangwine.
 
duh! Huyu jamaa akiwa rais 2015 nitaomba uraia wa kenya

Hakuna haja ya kukimbia wananchi wote wazalendo wapenda mema tubanane hapa hapa na tukatae watu kama hawa. Yaani TANESCO yenyewe iko hoi halafu bado huyu anapanga kuimalizia kabisa!
 
Natamani mwandishi aseme jamani hii ni ndoto tu.
Yaani bado watu kumbe hawajachoka tu kuifisadi nchi hii,inawezekana siyo huyo tu anayefanya mbinu hizo chafu.

Fige tufunguke hakuna ndoto tukinyamaza Tyson atafanya kweli na sisi kama marefa tusipoona hii faulo basi sikio litakuwa limeshaumwa na anaweza sema kuwa sikio linavuja damu kwa sababu yeye mwenyewe (mpinzani) ndiye kajigonga kwenye jino langu kwani hukumbuki msemo wa "kapigwa na kitu chenye ncha?"

Mafisadi sasa hawana aibu wala hawaogopi chochote kutokana na ukimya wetu!!
 
Hivi ni nani ameshusha hadhi ya uraisi? naona kila mtu anautaka
 
Mh wassira aka Tyson anayo haki ya kugombea cheo chochote ndani ya chama chake na ndani ya Tanzania, ili mradi havunji sheria.

Hizo hapo juu ni tuhuma zisizothibitishwa, tungepenga kupata uhakika wa kuonesha kwamba Wassira ni mchafu. Vinginevyo mwacheni wassira atumie haki yake kikatiba.
 
Back
Top Bottom