Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,576
- 2,499
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira Machi 16, 2025, akizungumza na wanachama wa CCM katika Wilaya ya Ileje, amesisitiza kuwa chama hicho kimeweka utaratibu wa wazi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Katika hotuba yake, Wasira alifafanua kuwa hakutakuwa na utaratibu wa wagombea kupita bila kupingwa katika chaguzi za ndani ya chama, akisisitiza umuhimu wa demokrasia na ushindani wa haki.
Aidha, aliwahimiza vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za udiwani na ubunge, akisema kuwa CCM ni chama kinachojengwa na vijana.
"Tunataka kuona vijana wanajitokeza kwa wingi katika mchakato wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
"CCM ni chama chenye misingi ya ushirikishwaji, na tunahitaji damu mpya kuendeleza mafanikio tuliyoyapata," alisema Wasira.
Pia, alisisitiza kuwa CCM imejipanga kuhakikisha uchaguzi wake unakuwa wa uwazi, haki, na ushindani wa kweli, ili kutoa fursa kwa wanachama wote wenye sifa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya chama na taifa kwa jumla.
Katika mkutano huo, viongozi na wanachama wa CCM walionyesha hamasa kubwa, huku wakiahidi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.
Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze