Wassira azomewa vibaya mkutanoni na kuondolewa chini ya ulinzi mkali wa Polisi!

Ester Bulaya amemmaliza mzee Wassira kwa kuanzisha ligi yake ya Ester Cup. Amewakamata vijana.

Hivi mbona nakumbuka kwamba wakati akiwa Waziri wa Maji Wassira aliwahi kushutumiwa kwa kulipendelea jimbo lake kwa kupeleka mradi mkubwa wa maji huko? Huo mradi uliishia wapi kama Bunda haina maji?

Simply kala pesa hapo hakuna jingine mkuu.
 
Huyu ndiye Steven Hasira alikipa CDM one year to death sasa ataanza kufa yeye na wanabunda wanadhihirisha.
 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mahusiano Stephen Wassira amezomewa vibaya na mamia ya wananchi akiwa katika mkutano wa hadhara jimboni kwake Bunda.

Wassira alikumbwa na balaa hilo alipoanza kukishambulia chama cha demokrasia na maendeleo-CDM.

Wassira alianza kumshutumu mkurugenzi wa mambo ya nje na Mbunge wa nyamagana Ezekiah Wenje kwamba haelewi ni nini kilimpeleka Bunda kufanya mkutano kwenye jimbo lake. Wassira pia alidai Wenje sio raia wa Tanzania bali ni wa nchi jirani.

Katika mkutano Wenje aliofanya jimboni Bunda mamia ya watu wakiwemo makada mashuhuri waliihama CCM na kujiunga na CDM.

Wassira alienda mbali zaidi na kuvishutumu vikali vyombo vya habari vinadanganya vinapozungumzia habari za CDM.

Alidai ni uongo mkubwa kusema huko Arusha maelfu ya wanaCCM wanakimbilia CDM. Alisema yeye ni mlezi wa CCM Arusha na ni wanachama watatu tu waliohama CCM na kujiunga CDM na haelewi vyombo vya habari vina agenda gani na CDM.

Baada ya kusema hayo wananchi walianza kupaaza sauti kubwa za kuzomea na kumtaka Wassira aseme amefanya nini tangu awe mbunge na sio kukashifu CDM.

Wassira alipandwa na hasira kubwa ndipo wananchi walizidisha makelele ya kuzomea huku uwanja mzima ukinyoosha vidole viwili na kuimba kwa sauti kubwa Peopleeeeees Power.

Wassira kuona hivyo alishuka haraka Jukwaani na kupanda gari na kuondoka chini ya ulinzi mkali wa Polisi.


Source: Nipashe Jumatano/Tanzania Daima Jumatano.

===============
Kutoka Gazeti la Tanzania Daima:

JINAMIZI la zomeazomea limezidi kumwandama mbunge wa jimbo la Bunda, Steven Wasira, ambapo jana tena alizomewa na wananchi baada ya kushindwa kujibu maswali waliyomuuliza.

Wassira alikumbwa na zahma hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani ya mjini Bunda.
Katika mkutano huo, Wasira aliulizwa maswali matatu na kijana mmoja aitwaye Joashi Kunaga ambayo baadhi yalionekana kumkasirisha.

Maswali hayo pamoja na kumtaka aeleze ni kwa nini eneo la Shule ya Msingi Balili limechukuliwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya, Chiku Galawa, ambaye sasa ni mkuu wa mkoa wa Tanga na wananchi walishalalamika lakini yeye hajawahi kulizungumzia.

Swali la pili kijana huyo alitaka kufahamu ukosefu wa maji katika Hospital ya DDH Bunda ambako sasa hivi wagonjwa wanalazimika kutoa maji majumbani mwao huku wakati ziwa liko km 11 toka mjini Bunda.

Katika swali lake la tatu alimuuliza kuwa katika mkutano huo alikuwa anahutubia kama mbunge, waziri au kada wa CCM kwani alitakiwa kufahamu kuwa Bunda ina wachama wa vyama vingi.

Mwingine aliyeuliza swali ni mwenyekiti wa mtaa wa Nyerere, Maxmilian, aliyetaka kujua ni kwani nini halmashauri imetengeneza milango ya shule za sekondari za kata kwa shilingi laki nne kwa kila mlango.

Baada ya kuulizwa maswali hayo Wassira alisimama katika hali iliyoonyesha kuwa ana hasira na kuaanza kujibu maswali hayo kwa ukali.

Wassira alianza kujibu swali la kwanza la Kunaga akisema kuwa hawezi kulisemea hilo ni la watu wa ardhi kwa madai kuwa kama mtu alikuwa na pesa zake akaomba akapewa yeye hawezi kulizungumzia.

Kuhusu suala la maji alisema kuwa maji yapo katika mchakato na kwamba wananchi watarajie kupata maji muda si mrefu jibu ambalo wananchi walilikataa na kudai kuwa ahadi zake kuhusu maji zimekuwa za uongo tangia mwaka 2007 hadi leo amekuwa akisema uongo.

Akijibu kuhusu hoja ya yeye kuhutubia kama mbunge au waziri, Wassira alionekana kujawa na hasira na kuuliza kwa ukali, “Kwani Wenje alikuja kuhutubia hapa hivi karibuni kama nani?”

Jibu hilo lilizidi kuwachefua wananchi ambao walianza kuzomea huku wakiimba: “People’s Power.”

Wengine walisikika wakisema: “Afadhali Esther Bulaya kuliko wewe.”

Jambo ambalo lilifanya polisi waliokuwepo kuanza kujiandaa kwa lolote na ndipo Wasira alipochukia na kuamua kuondoka majira ya saa 11 huku akiacha wananchi wakiwa bado na maswali ya kumuuliza.

Hata hivyo baada ya kuondoka wananchi hususan kundi kubwa la vijana lililokuwepo mkutanoni hapo liliendelea kuimba: “People’s Power.” Huku wakinyoosha vidole viwili vinavyotumiwa na Chama cha CHADEMA na wengine wakilitaja sana jina la mbunge wa viti maalumu vijana Bulaya ambaye sasa anaonekana kuwa kipenzi cha Wanabunda kutokana na msimamo wake bungeni wa kutetea mambo mbalimbali likiwemo suala la kero ya maji ambalo ni tatizo kubwa kwa wananchi wa mji wa Bunda na vitingoji vyake.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya Wassira kuondoka,

Jaman huyu siasisema CDM itasambaratika soon? Alidhani ni nguvu ya soda eh! Hii ndo nguvu ya UMMA bwana.
 
hapo red umetengua mbav mbili kwa kicheko!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
huyu mzee alistahili kabisa kuzomewa. majibu yake kama sura yake.Ester bulaya kashawateka vijana kuna kipindi niliwahi kusoma kama ester 2015 anataka agombee jimboni si viti maalum kama Halima mdee. hahaha kazi kweli kweli amchukue lusinde wakatukane
 
Wassira alishinda Bunda by a landslide and a half. Miaka miwili baadae iweje watu wale wale wamekuja kumzomea? Unless alifanya mkutano pembeni ya makao makuu ya CHADEMA jimboni. Itisha uchaguzi kesho Bunda uone itakuwaje kwenye ballot box!

Taarifa hizi za true lies ndio zinafanya wapinzania wanaendelea kupigwa bao sehemu ambazo wanategemea kushinda mpaka dakika ya mwisho, hakuna technical polling wala scientific survey wala in-depth analysis of citizen sentiment. What has happened to change these people's minds all of a sudden?

I think Bunda is not an island that the residents do not hear what is happening in other areas of the country. political waves will usually change the atmosphere within no time as opposed to what you put forward. Kumbuka wazo la kumng'oaWaziri mkuu mstaafu EL na hata mawaziri hivi karibuni. Haikuchukua muda mrefu jamii kubadilika na kuwa against wao.
 
Mh Waziri.jpg
Photo Source: Nipashe Jumatano May 23 2012.
Frontpage

Sasa wewe mshimiwa Waziri si ungejibu tu hoja vizuri, ona sasa umezomewa.
 
Wasira bado hajaacha uongo tu, yalomtokea Arumeru kwa kumsingizia Dr wa ukweli bado tu hajakoma. Ama kweli nimeamini jasiri aachi ASILI
 
Inasemekana kabila la Wasonjo wanaishi mkoa wa Mara
Inasemekana pia kuwa Wasonjo ndio wanyama wa mwisho kuwa binadamu kamili hivi karibuni.
Wassira ni kabila gani huko Mara?
View attachment 54469
Photo Source: Nipashe Jumatano May 23 2012.
Frontpage

Sasa wewe mshimiwa Waziri si ungejibu tu hoja vizuri, ona sasa umezomewa.
 
ni dalili kwamba huyu mteule wa rais hakubaliki popote pale maana kama ndni ya jimbo lake hakubaliki ni wap sasa pa kukubalika tena. asubiri kipindi cha bunge kifike akalale tu mana naona kwa sasa hana kazi

arusha tuna bifu naye...hawezi kututoroka kimyakimya
 
Tatizo kuwa la JF ni ushabiki na uongo. Mimi mwandishi wa habari hii nilihudhulia mutant aw wasira pale Bunda. Mkurya no Iliana saa 9 alasili Hadi saa 12 jioni. Wasira alieleza mambo mengine ya kitaifa. Vyombo vinginevyo vya habari vilikuwepo Kama vile ITV, star TV, channel ten na TBC1 . Vito hivi vote vimetangaza uhalisia uliokuwepo hapo mkutanoni. Kama ilivyo kawaida mikutano mikubwa kama ilivyo kuwa mkutano huo aw Bunda , hapakosi walevi ambao nao waliotaka waonekane wapo. Na kwa walevi waliokuwepo kupigisha make lee ni kawaida. Baada ya hotuba yake ya kusisimua, alijuibu maswali 10. Baada ya kufungwa kwa mkutano majira ya saa 12, wasira alibaki hapo uwanjani akisalimiana na Watu wengi waliomfuata kumsalimu na kumpongeza. Sasa habari ya kuondolewa china ya ulinzi ili tokea wapi? Tukiacha uongo na ushabiki JF itakuwaj combo cha maana cha kupeana habari za kweli.

Nachelea kuamini na wewe ni mwandishi wa habari, ningekua na pc ningekutoa makosa mengi sana ya uandishi, anyway naheshmu haki yako ya kikatiba.
 
Tatizo kuwa la JF ni ushabiki na uongo. Mimi mwandishi wa habari hii nilihudhulia mutant aw wasira pale Bunda. Mkurya no Iliana saa 9 alasili Hadi saa 12 jioni. Wasira alieleza mambo mengine ya kitaifa. Vyombo vinginevyo vya habari vilikuwepo Kama vile ITV, star TV, channel ten na TBC1 . Vito hivi vote vimetangaza uhalisia uliokuwepo hapo mkutanoni. Kama ilivyo kawaida mikutano mikubwa kama ilivyo kuwa mkutano huo aw Bunda , hapakosi walevi ambao nao waliotaka waonekane wapo. Na kwa walevi waliokuwepo kupigisha make lee ni kawaida. Baada ya hotuba yake ya kusisimua, alijuibu maswali 10. Baada ya kufungwa kwa mkutano majira ya saa 12, wasira alibaki hapo uwanjani akisalimiana na Watu wengi waliomfuata kumsalimu na kumpongeza. Sasa habari ya kuondolewa china ya ulinzi ili tokea wapi? Tukiacha uongo na ushabiki JF itakuwaj combo cha maana cha kupeana habari za kweli.

Halafu hata Channel 10, tbc na star tv ni makada waaminifu wa magamba, je wewe ungetegemea wahariri waruhusu habari kama hii iliyo negative kwa mgamba halafu waweke rehani vibarua vyao?
 
Hii jamii forum sasa inaonekana ina Fungamana na chadema,haitoi habari kwa usawa,juzi juzi hapa kuna wanachama wa chadema wamehamia Ccm hamjasema!!!

Ayaa.....wewe kama CCM ulitaka nani akusemee? Mwaka mzima una post 10 tu?
 
Mkuu dunia inabadilika haraka kuliko unavyoweza kufikiria. Jaribu kusoma views of the people -report zinazotolewa na REPOA harafu tafuta the most recent one. Utajua kuwa suala la Wasira kuchaguliwa kwa landslide miaka 2 leo hii inaonekana kama historia ni dhahiri kuwa media imehabarisha watu, na mwamko ni mkubwa sana hasa miongoni mwa vijana. Hawadanganyiki tena kirahisi kwa ahadi za kofia na tshirt!
Wassira alishinda Bunda by a landslide and a half. Miaka miwili baadae iweje watu wale wale wamekuja kumzomea? Unless alifanya mkutano pembeni ya makao makuu ya CHADEMA jimboni. Itisha uchaguzi kesho Bunda uone itakuwaje kwenye ballot box!

Taarifa hizi za true lies ndio zinafanya wapinzania wanaendelea kupigwa bao sehemu ambazo wanategemea kushinda mpaka dakika ya mwisho, hakuna technical polling wala scientific survey wala in-depth analysis of citizen sentiment. What has happened to change these people's minds all of a sudden?
 
1. Amekuwa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani-IDARA YA UHAMIAJI?

2. Kama ni watatu si awataje Majina...?

Tatizo la magamba ni ulevi wa madaraka kwani kila mmoja anajihisi ndiyo serikali yenyewe. Mpuuzi huyu amejitwalia mamlaka ya kumtangaza mtanzania mwenzie ati kuwa si raia! Akamuulize mwenzake aliyekuwa mbunge wa Nyamagana yaliyomkuta baada ya arrogance ya aina hiyo. Natabiri hukumu ya umma kumfikia mwaka 2015 kwa hiyo ajiandae kuwa mtazamaji. Sijaona mzee mwenye ufinyu wa fikra kama huyu Bwana.
 
Inasemekana kabila la Wasonjo wanaishi mkoa wa Mara
Inasemekana pia kuwa Wasonjo ndio wanyama wa mwisho kuwa binadamu kamili hivi karibuni.
Wassira ni kabila gani huko Mara?

Mh kwa nini unauliza kabila lake ni Mtanzania
 
Back
Top Bottom