Wassira azomewa vibaya mkutanoni na kuondolewa chini ya ulinzi mkali wa Polisi!

Tatizo kuwa la JF ni ushabiki na uongo. Mimi mwandishi wa habari hii nilihudhulia mutant aw wasira pale Bunda. Mkurya no Iliana saa 9 alasili Hadi saa 12 jioni. Wasira alieleza mambo mengine ya kitaifa. Vyombo vinginevyo vya habari vilikuwepo Kama vile ITV, star TV, channel ten na TBC1 . Vito hivi vote vimetangaza uhalisia uliokuwepo hapo mkutanoni. Kama ilivyo kawaida mikutano mikubwa kama ilivyo kuwa mkutano huo aw Bunda , hapakosi walevi ambao nao waliotaka waonekane wapo. Na kwa walevi waliokuwepo kupigisha make lee ni kawaida. Baada ya hotuba yake ya kusisimua, alijuibu maswali 10. Baada ya kufungwa kwa mkutano majira ya saa 12, wasira alibaki hapo uwanjani akisalimiana na Watu wengi waliomfuata kumsalimu na kumpongeza. Sasa habari ya kuondolewa china ya ulinzi ili tokea wapi? Tukiacha uongo na ushabiki JF itakuwaj combo cha maana cha kupeana habari za kweli.

Yupo mwenzio mwenye njaa Kama wewe aliwahi kutamka kuwa"huwa tunalipwa chochote tunapolwenda ktk mikutano yoyote ya siasa"Wewe ni mmoja wao endelea tu kuibadili mbili kuwa moja ipo siku utapata mshahara wako.
 
Tatizo ambalo ccm hawataki kulikubali kwamba MUNGU AMEWAACHA.hakuna mzee wala kijana wote ni tatizo,wamepigwa uziwi,upofu,wamefungwa ufahamu!bado kidogo watapigwa na ububu sijui nani atawasemea!pole za dhati kwa wasira
 
Namshauri mheshimiwa Ester bulayi ahamie chadema ili achukue jimbo kwani kwa sasa ndo kipenzi cha wananchi wa jimbo la Bunda ukilinganisha na wale wote wanao onyesha nia kgombea jimbo hilo.
 
1.jpg
 
Wassira acha Hassira mazee.

Mimi nimefurahishwa sana na habari hizi za zomeazomea kwa huyu Waziri kibuyu wa Serikali ya Magamba. Hii itakuwa imepeleka SALAMU ZA MJOMBA kwa Rais kwa vile Wassira anatoka Ofisi hiyohiyo ya Kiwete(akishughulikia Mahusiano ya Jamii).Wassira ni mmoja wa mawaziri bomu kabsa katika Baraza la Mawaziri wa Rais Kiwete. Huyu babu alitakiwa asiwepo kwenye Baraza jipya lakini kwa vile ANA KAZI MAALUMU YA KUIMALIZA CHADEMA katika mwaka mmoja kama alivyodai hivi karibuni ndiyo maana pengine Kiwete kambakisha. Lakini Wassira na Kiwete wanashindwa kusoma alama za Nyakati maana hii M4C inavyoenea kwa kasi ya MOTO WA NYIKA hawataiweza!!!

Naweza kuona kwamba Kiwete anaamini sana uongo wa huyu kibabu Wassira kwa vile sijui anaitwa Tyson basi anaweza kuisambaratisha CHADEMA kwa kutumia u-Tyson wake kwa mwaka 1 tu, kitu ambacho si kweli! Wassira kwa sasa ni Waziri anayesifika kwa KUCHAPA USINGIZI BUNGENI na UMBEYA mwingi. Tunakumbuka alivoanikwa na media akiwa ameuchapa usingizi Bungeni na alipoulizwa akadai alikuwa kwenye dozi ya MAFUA! Hata hivyo aliishutuma sana media kwa picha walizompiga na kuwaita kuwa ni WACHOCHEZI!!

Kwenye kampeni za Uchaguzi Arumeru East,Wassira alisikika akimzushia umbeya Katibu Mkuu CDM Dr.Slaa kuwa alifukuzwa upadre kwa kuiba sadaka za ujio wa Papa na Kanisa Catholic likamjia juu. Aliambiwa athibitishe na hajafanya hivo mpaka leo. Huyu ni mtu aliyechoka KIMWILI NA KIAKILI(Uzee) na ndiyo maana kila wakti anaongea utumbo. Mtu makini hawezi kuuliza ati Wenje alienda kuhutubia Bunda kama Nani??? Ebo! Wenje ni Mbunge wa CHADEMA anaweza kwenda kuhutubia mkutano mahali popote kwa ajili ya kuhamasisha Watz waikatae CCM. Yeye Wassira alienda Arumeru East na akahutubia mkutano wa Kampeni. Je alitaka wana Arumeru wamwuliza alikuwa akihutubi kama Nani???

Hata anapohoji Uraia wa Wenje ni upumbavu kwani Wenje aliwahi kuwekewa pingamizi na Lawrence Masha(Waziri wa Internal Afffairs wakti ule akiwa Mb wa Nyamagana akiwa na hofu ya nguvu ya CDM. Pingamizi hilo la Masha lilitupwa na NEC na ikawekwa wazi kuwa Wenje alikuwa ni Raia halali wa Tanzana na ndiyo maana aligombea akashinda. Sasa huyu mzee wa hasira anapoleta mambo ya Uraia wa Wenje anaonekana kuishiwa. Wazungu wanasema INTELLIGENT MIND DISCUSS ISSUES, BUT FOOLISH MIND DISCUSS PEOPLE!

Kwa hiyo Steven Wassira is nothing else but just a big FOOL!
 
What is the margin of a landslide?Before you throw words aimlessly check their meaning?
Sielewi maana ya kushinda by a landslide?

NATIONAL ELECTION COMMITTEE

STEPHEN WASSIRACCM27,50266%
ELIAS KAJERI MAARUGUCHADEMA12,22429%
WIREGI SONGAMBELECUF4341%

Let's do basic arithmetics for a second: Kura za CHADEMA zidisha mara mbili ongeza 7% ndio zingekaribia karibia zile za Wassira. Sasa hapo kweli jamani sijui maana ya maneno ninayotumia nikisema alishinda by a landslide kweli kaka??

Reporter mwingine wa JF aliandika hivi:

Wassira Ashinda Kwa Kishindo

Matokeo ubunge Bunda ni kama ifuatavyo:

CCM wamepata kura 27305
Chadema wamepata kura 12572

Kwa hiyo Stephen M. Wasira ameshinda jimbo la Bunda kwa asilimia 68

Habari ndio hiyo!

Kwa hiyo, kabla hatujakaa hapa tunafanyia kazi ripoti ya TANZANIA DAIMA, kwamba Wassira kazomewa Wassira kaondoka na polisi, let's go a little deeper than that... what happened in the interim? Between one year and a half ago todate? What happened?

I don't gullibly swallow the content from TANZANIA DAIMA, gazeti la chama, any more than I swallow the content of UHURU, gazeti la Chama! Yote hayawezi kukuelezea ukweli wa maendeleo ya chama! ....ni magazeti ya chama! hahahahahahaa!

(Invisible, usifute post zangu, umenifuta kwenye thread ya SHIBUDA!!! Hahahahaaaaa!)
 
Sielewi maana ya kushinda by a landslide?

NATIONAL ELECTION COMMITTEE

STEPHEN WASSIRACCM27,50266%
ELIAS KAJERI MAARUGUCHADEMA12,22429%
WIREGI SONGAMBELECUF4341%

Let's do basic arithmetics for a second: Kura za CHADEMA zidisha mara mbili ongeza 7% ndio zingekaribia karibia zile za Wassira. Sasa hapo kweli jamani sijui maana ya maneno ninayotumia nikisema alishinda by a landslide kweli kaka??

Reporter mwingine wa JF aliandika hivi:

Kwa hiyo, kabla hatujakaa hapa tunafanyia kazi ripoti ya TANZANIA DAIMA, kwamba Wassira kazomewa Wassira kaondoka na polisi, let's go a little deeper than that... what happened in the interim? Between one year and a half ago todate? What happened?

I don't gullibly swallow the content from TANZANIA DAIMA, gazeti la chama, any more than I swallow the content of UHURU, gazeti la Chama! Yote hayawezi kukuelezea ukweli wa maendeleo ya chama! ....ni magazeti ya chama! hahahahahahaa!

(Invisible, usifute post zangu, umenifuta kwenye thread ya SHIBUDA!!! Hahahahaaaaa!)

Kwa hiyo Balasconi hajaondoka madarakani? na uchaguzi uliopita hakushinda? unafikiri binadamu ni static. Soma trend binadamu. Unaweza ukashangiliwa leo na kesho ukatolewa vilevile.
 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mahusiano Stephen Wassira amezomewa vibaya na mamia ya wananchi akiwa katika mkutano wa hadhara jimboni kwake Bunda.

Wassira alikumbwa na balaa hilo alipoanza kukishambulia chama cha demokrasia na maendeleo-CDM.

Wassira alianza kumshutumu mkurugenzi wa mambo ya nje na Mbunge wa nyamagana Ezekiah Wenje kwamba haelewi ni nini kilimpeleka Bunda kufanya mkutano kwenye jimbo lake. Wassira pia alidai Wenje sio raia wa Tanzania bali ni wa nchi jirani.

Katika mkutano Wenje aliofanya jimboni Bunda mamia ya watu wakiwemo makada mashuhuri waliihama CCM na kujiunga na CDM.

Wassira alienda mbali zaidi na kuvishutumu vikali vyombo vya habari vinadanganya vinapozungumzia habari za CDM.

Alidai ni uongo mkubwa kusema huko Arusha maelfu ya wanaCCM wanakimbilia CDM. Alisema yeye ni mlezi wa CCM Arusha na ni wanachama watatu tu waliohama CCM na kujiunga CDM na haelewi vyombo vya habari vina agenda gani na CDM.

Baada ya kusema hayo wananchi walianza kupaaza sauti kubwa za kuzomea na kumtaka Wassira aseme amefanya nini tangu awe mbunge na sio kukashifu CDM.

Wassira alipandwa na hasira kubwa ndipo wananchi walizidisha makelele ya kuzomea huku uwanja mzima ukinyoosha vidole viwili na kuimba kwa sauti kubwa Peopleeeeees Power.

Wassira kuona hivyo alishuka haraka Jukwaani na kupanda gari na kuondoka chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

Source: Nipashe Jumatano/Tanzania Daima Jumatano.

===============
Kutoka Gazeti la Tanzania Daima:

JINAMIZI la zomeazomea limezidi kumwandama mbunge wa jimbo la Bunda, Steven Wasira, ambapo jana tena alizomewa na wananchi baada ya kushindwa kujibu maswali waliyomuuliza.

Wassira alikumbwa na zahma hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani ya mjini Bunda.
Katika mkutano huo, Wasira aliulizwa maswali matatu na kijana mmoja aitwaye Joashi Kunaga ambayo baadhi yalionekana kumkasirisha.

Maswali hayo pamoja na kumtaka aeleze ni kwa nini eneo la Shule ya Msingi Balili limechukuliwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya, Chiku Galawa, ambaye sasa ni mkuu wa mkoa wa Tanga na wananchi walishalalamika lakini yeye hajawahi kulizungumzia.

Swali la pili kijana huyo alitaka kufahamu ukosefu wa maji katika Hospital ya DDH Bunda ambako sasa hivi wagonjwa wanalazimika kutoa maji majumbani mwao huku wakati ziwa liko km 11 toka mjini Bunda.

Katika swali lake la tatu alimuuliza kuwa katika mkutano huo alikuwa anahutubia kama mbunge, waziri au kada wa CCM kwani alitakiwa kufahamu kuwa Bunda ina wachama wa vyama vingi.

Mwingine aliyeuliza swali ni mwenyekiti wa mtaa wa Nyerere, Maxmilian, aliyetaka kujua ni kwani nini halmashauri imetengeneza milango ya shule za sekondari za kata kwa shilingi laki nne kwa kila mlango.

Baada ya kuulizwa maswali hayo Wassira alisimama katika hali iliyoonyesha kuwa ana hasira na kuaanza kujibu maswali hayo kwa ukali.

Wassira alianza kujibu swali la kwanza la Kunaga akisema kuwa hawezi kulisemea hilo ni la watu wa ardhi kwa madai kuwa kama mtu alikuwa na pesa zake akaomba akapewa yeye hawezi kulizungumzia.

Kuhusu suala la maji alisema kuwa maji yapo katika mchakato na kwamba wananchi watarajie kupata maji muda si mrefu jibu ambalo wananchi walilikataa na kudai kuwa ahadi zake kuhusu maji zimekuwa za uongo tangia mwaka 2007 hadi leo amekuwa akisema uongo.

Akijibu kuhusu hoja ya yeye kuhutubia kama mbunge au waziri, Wassira alionekana kujawa na hasira na kuuliza kwa ukali, “Kwani Wenje alikuja kuhutubia hapa hivi karibuni kama nani?”

Jibu hilo lilizidi kuwachefua wananchi ambao walianza kuzomea huku wakiimba: “People’s Power.”

Wengine walisikika wakisema: “Afadhali Esther Bulaya kuliko wewe.”

Jambo ambalo lilifanya polisi waliokuwepo kuanza kujiandaa kwa lolote na ndipo Wasira alipochukia na kuamua kuondoka majira ya saa 11 huku akiacha wananchi wakiwa bado na maswali ya kumuuliza.

Hata hivyo baada ya kuondoka wananchi hususan kundi kubwa la vijana lililokuwepo mkutanoni hapo liliendelea kuimba: “People’s Power.” Huku wakinyoosha vidole viwili vinavyotumiwa na Chama cha CHADEMA na wengine wakilitaja sana jina la mbunge wa viti maalumu vijana Bulaya ambaye sasa anaonekana kuwa kipenzi cha Wanabunda kutokana na msimamo wake bungeni wa kutetea mambo mbalimbali likiwemo suala la kero ya maji ambalo ni tatizo kubwa kwa wananchi wa mji wa Bunda na vitingoji vyake.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya Wassira kuondoka, baadhi ya wananchi walimtuhumu mbunge huyo kushindwa kujibu maswali aliyoulizwa wakisema kuwa kitendo hicho kinaonyesha alivyochoka kutokana na umri wake.
Wananchi hao walimshutumu Wassira wakisema kuwa aliishawaona wananchi wa Bunda ni watu wa kudanganywa lakini safari hii wamechoshwa na hadithi zake.

“Huyu mzee ni msanii; juzi alipoona anataka kufanya mkutano hapa aliwaita waandishi wa habari wa TV na magazeti wale wanaomsapoti akaandaa na mtambo wa kuchimba mtaro ambao ulichimba km chache na akachukua wajumbe wa bodi ya maji wakachukuliwa maoni na yeye akaongea lakini baada ya yeye kuondoka huko Nyabehu ule mtambo haupo tena na kazi hiyo haiendelei sasa leo anakuja kutupatia hadidu za rejea,” alisema mkazi mmoja Chacha Maswi mkazi wa kijiji cha Nyabehu.

Hata hivyo mkutano huo ulihudhuriwa na watu wachache tofauti na siku nyingine lakini pia ukilinganisha na ule aliohutubia mbunge wa Nyamagana Eziekiel Wenje mwezi uliopita na wananchi wakakubali kunyeshewa mvua wakimsikiliza.

Hali kadhalika idadi hiyo ya watu waliohudhuria mkutano huo wa Wassira pia haikufikia ile ya waliokuwepo juzi wakati Bulaya akikabidhi kombe la timu ya vijana wa Bunda mjini.

Source:
Tanzania Daima

Pipo pawa
 
kama kungekuwa na haki ya wapiga kura jimboni kumwondoa mbunge wao, wasira angeshakuwa historia bunda!
 
Kamata mwizi meeeeeeeeeeee!nahisi wananchi walikua wanamwimbia huu wimbo
 
Kuhusu suala la maji, wananchi wana hoja kubwa na nzito ambayo inatakiwa kujadiliwa. Wilaya zote zilizoko kando ya ziwa zina shida ya maji kiasi cha dumu la lita 20 za maji kuuzwa kwa shilingi 500 hadi 700 ilihali ziwa liko kilomita 5 to 5 kutoka katika miji hiyo, ukerewe imezungukwa na maji sehemu zote lakini haina maji safi na salama, hali hii ni kuwadhalilisha wananchi wanaoishi maeneo hayo. nawasilisha.
 
huyu nabii inakuwaje anazomewa,au yeye anaweza kutabiri ya cdm tu na siyo ya kuzomewa
 
Hii jamii forum sasa inaonekana ina Fungamana na chadema,haitoi habari kwa usawa,juzi juzi hapa kuna wanachama wa chadema wamehamia Ccm hamjasema!!!

siungesema wewe..?ungesema tungechangia..yawezekana wewe ni memba pekee uliyesikia/soma habari hiyo..
 
Umefika wakati wa viongozi wote wanaoshikilia itikadi za chama tawala kama wasira kukaa pembeni tumewachoka,hongereni wananchi mwendo huohuo msirudi nyuma.
 
Badala ya magamba kuweweseka wanapaswa kuja mbele ya wananchi kwa unyenyekevu kuelezea ahadi zimefikia wapi? Hata wafanyeje janga ndo limewakuta....
 
Back
Top Bottom