Wassira azomewa vibaya mkutanoni na kuondolewa chini ya ulinzi mkali wa Polisi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wassira azomewa vibaya mkutanoni na kuondolewa chini ya ulinzi mkali wa Polisi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, May 24, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mahusiano Stephen Wassira amezomewa vibaya na mamia ya wananchi akiwa katika mkutano wa hadhara jimboni kwake Bunda.

  Wassira alikumbwa na balaa hilo alipoanza kukishambulia chama cha demokrasia na maendeleo-CDM.

  Wassira alianza kumshutumu mkurugenzi wa mambo ya nje na Mbunge wa nyamagana Ezekiah Wenje kwamba haelewi ni nini kilimpeleka Bunda kufanya mkutano kwenye jimbo lake. Wassira pia alidai Wenje sio raia wa Tanzania bali ni wa nchi jirani.

  Katika mkutano Wenje aliofanya jimboni Bunda mamia ya watu wakiwemo makada mashuhuri waliihama CCM na kujiunga na CDM.

  Wassira alienda mbali zaidi na kuvishutumu vikali vyombo vya habari vinadanganya vinapozungumzia habari za CDM.

  Alidai ni uongo mkubwa kusema huko Arusha maelfu ya wanaCCM wanakimbilia CDM. Alisema yeye ni mlezi wa CCM Arusha na ni wanachama watatu tu waliohama CCM na kujiunga CDM na haelewi vyombo vya habari vina agenda gani na CDM.

  Baada ya kusema hayo wananchi walianza kupaaza sauti kubwa za kuzomea na kumtaka Wassira aseme amefanya nini tangu awe mbunge na sio kukashifu CDM.

  Wassira alipandwa na hasira kubwa ndipo wananchi walizidisha makelele ya kuzomea huku uwanja mzima ukinyoosha vidole viwili na kuimba kwa sauti kubwa Peopleeeeees Power.

  Wassira kuona hivyo alishuka haraka Jukwaani na kupanda gari na kuondoka chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

  Source: Nipashe Jumatano/Tanzania Daima Jumatano.

  ===============
  Kutoka Gazeti la Tanzania Daima:

  JINAMIZI la zomeazomea limezidi kumwandama mbunge wa jimbo la Bunda, Steven Wasira, ambapo jana tena alizomewa na wananchi baada ya kushindwa kujibu maswali waliyomuuliza.

  Wassira alikumbwa na zahma hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani ya mjini Bunda.
  Katika mkutano huo, Wasira aliulizwa maswali matatu na kijana mmoja aitwaye Joashi Kunaga ambayo baadhi yalionekana kumkasirisha.

  Maswali hayo pamoja na kumtaka aeleze ni kwa nini eneo la Shule ya Msingi Balili limechukuliwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya, Chiku Galawa, ambaye sasa ni mkuu wa mkoa wa Tanga na wananchi walishalalamika lakini yeye hajawahi kulizungumzia.

  Swali la pili kijana huyo alitaka kufahamu ukosefu wa maji katika Hospital ya DDH Bunda ambako sasa hivi wagonjwa wanalazimika kutoa maji majumbani mwao huku wakati ziwa liko km 11 toka mjini Bunda.

  Katika swali lake la tatu alimuuliza kuwa katika mkutano huo alikuwa anahutubia kama mbunge, waziri au kada wa CCM kwani alitakiwa kufahamu kuwa Bunda ina wachama wa vyama vingi.

  Mwingine aliyeuliza swali ni mwenyekiti wa mtaa wa Nyerere, Maxmilian, aliyetaka kujua ni kwani nini halmashauri imetengeneza milango ya shule za sekondari za kata kwa shilingi laki nne kwa kila mlango.

  Baada ya kuulizwa maswali hayo Wassira alisimama katika hali iliyoonyesha kuwa ana hasira na kuaanza kujibu maswali hayo kwa ukali.

  Wassira alianza kujibu swali la kwanza la Kunaga akisema kuwa hawezi kulisemea hilo ni la watu wa ardhi kwa madai kuwa kama mtu alikuwa na pesa zake akaomba akapewa yeye hawezi kulizungumzia.

  Kuhusu suala la maji alisema kuwa maji yapo katika mchakato na kwamba wananchi watarajie kupata maji muda si mrefu jibu ambalo wananchi walilikataa na kudai kuwa ahadi zake kuhusu maji zimekuwa za uongo tangia mwaka 2007 hadi leo amekuwa akisema uongo.

  Akijibu kuhusu hoja ya yeye kuhutubia kama mbunge au waziri, Wassira alionekana kujawa na hasira na kuuliza kwa ukali, "Kwani Wenje alikuja kuhutubia hapa hivi karibuni kama nani?"

  Jibu hilo lilizidi kuwachefua wananchi ambao walianza kuzomea huku wakiimba: "People's Power."

  Wengine walisikika wakisema: "Afadhali Esther Bulaya kuliko wewe."

  Jambo ambalo lilifanya polisi waliokuwepo kuanza kujiandaa kwa lolote na ndipo Wasira alipochukia na kuamua kuondoka majira ya saa 11 huku akiacha wananchi wakiwa bado na maswali ya kumuuliza.

  Hata hivyo baada ya kuondoka wananchi hususan kundi kubwa la vijana lililokuwepo mkutanoni hapo liliendelea kuimba: "People's Power." Huku wakinyoosha vidole viwili vinavyotumiwa na Chama cha CHADEMA na wengine wakilitaja sana jina la mbunge wa viti maalumu vijana Bulaya ambaye sasa anaonekana kuwa kipenzi cha Wanabunda kutokana na msimamo wake bungeni wa kutetea mambo mbalimbali likiwemo suala la kero ya maji ambalo ni tatizo kubwa kwa wananchi wa mji wa Bunda na vitingoji vyake.

  Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya Wassira kuondoka, baadhi ya wananchi walimtuhumu mbunge huyo kushindwa kujibu maswali aliyoulizwa wakisema kuwa kitendo hicho kinaonyesha alivyochoka kutokana na umri wake.
  Wananchi hao walimshutumu Wassira wakisema kuwa aliishawaona wananchi wa Bunda ni watu wa kudanganywa lakini safari hii wamechoshwa na hadithi zake.

  "Huyu mzee ni msanii; juzi alipoona anataka kufanya mkutano hapa aliwaita waandishi wa habari wa TV na magazeti wale wanaomsapoti akaandaa na mtambo wa kuchimba mtaro ambao ulichimba km chache na akachukua wajumbe wa bodi ya maji wakachukuliwa maoni na yeye akaongea lakini baada ya yeye kuondoka huko Nyabehu ule mtambo haupo tena na kazi hiyo haiendelei sasa leo anakuja kutupatia hadidu za rejea," alisema mkazi mmoja Chacha Maswi mkazi wa kijiji cha Nyabehu.

  Hata hivyo mkutano huo ulihudhuriwa na watu wachache tofauti na siku nyingine lakini pia ukilinganisha na ule aliohutubia mbunge wa Nyamagana Eziekiel Wenje mwezi uliopita na wananchi wakakubali kunyeshewa mvua wakimsikiliza.

  Hali kadhalika idadi hiyo ya watu waliohudhuria mkutano huo wa Wassira pia haikufikia ile ya waliokuwepo juzi wakati Bulaya akikabidhi kombe la timu ya vijana wa Bunda mjini.

  Source:
  Tanzania Daima
   
 2. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Baadeye utamsikia Wasira anasema hakuzomewa, alikua anashangiliwa na habari kua ameondoka chini ya ulinzi wa polisi ni uongo....
   
 3. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 837
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  1. Amekuwa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani-IDARA YA UHAMIAJI?

  2. Kama ni watatu si awataje Majina...?
   
 4. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,111
  Likes Received: 10,468
  Trophy Points: 280
  Big up wananchi wa Bunda ila mngefanya la maana kama mngempopoa mawe.
   
 5. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Ukiona nyani anatamba msituni ujue kakwepa mishale mingi,lakini bunduki walizomtayarishia sijui kama hatatoka salama bunda 2015.lazima afe!sokwe.................
   
 6. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Wassira alishinda Bunda by a landslide and a half. Miaka miwili baadae iweje watu wale wale wamekuja kumzomea? Unless alifanya mkutano pembeni ya makao makuu ya CHADEMA jimboni. Itisha uchaguzi kesho Bunda uone itakuwaje kwenye ballot box!

  Taarifa hizi za true lies ndio zinafanya wapinzania wanaendelea kupigwa bao sehemu ambazo wanategemea kushinda mpaka dakika ya mwisho, hakuna technical polling wala scientific survey wala in-depth analysis of citizen sentiment. What has happened to change these people's minds all of a sudden?
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,101
  Trophy Points: 280
  Safi sana!!! Magamba wote wanastahili kuzomewa katika kila kona ya nchi yetu.
   
 8. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  je alivotoka hapo akaenda wapi?
  Gembe, Selou, Manyara, Ngorongoro, Mikumi, Serengeti au Katavi?
   
 9. e

  environmental JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,054
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Tyson anasahau kuwa jimbo lake halijali chama bali mtu hata yeye alikuwa NCCR mageuzi
   
 10. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Wassira amepewa nafasi nzuri wakati wote na ameshindwa kuzitumia zaidi ya Ubabe. Akiwa Waziri wa Kilimo ikaja Kilimo Kwanza angaitumia vizuri fursa hii ambayo inafadha nyingi zikiwemo za wafadhili angeweza kuleta mabadiliko ya haraka hasa vijijini, lakini wapi amebaki kuendekeza Ubabe tu. Kwanza amezeeka ni bora ajiandae kupumzika maana siasa za ubabe kwa sasa zimeishapitwa na wakati.
   
 11. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,404
  Likes Received: 3,734
  Trophy Points: 280
  Nadhani kushuka kwa imani yao juu ya utendaji wa serikali is what has happened these people's minds all of a sudden.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  karibu nyumbani ujue nini kimebadili mawazo ya watu
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kuwa magamba ni janga la kitaifa.Weka wewe hiyo ya kweli unayoijuwa.Kwa hiyo hakuzomewa? Alishangiliwa na gari kusukumwa?
   
 14. D

  DUNIANGUMU JR Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watendaji wote wa serikali kama wangekuwa wanatumia nafasi zao kuendeleza makwao kama jamaa anavyosema sehemu za nchi hii zingine zisingekuwa na na barabara!!!! si maneno ya kuhimiza hayo ya kupendelea pale unapotoka labda kama ni sera za baadhi ya vyama vya siasa.
   
 15. S

  STIDE JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  NO!! Alienda kisiwa kimoja kinaitwa LUBONDO NATIONAL PARK!! Kisiwa hiki kipo maeneo ya Chato kwa John Pombe, katikati ya kijiji kimoja kinaitwa Mganza na Kimwani.
   
 16. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ni dalili kwamba huyu mteule wa rais hakubaliki popote pale maana kama ndni ya jimbo lake hakubaliki ni wap sasa pa kukubalika tena. asubiri kipindi cha bunge kifike akalale tu mana naona kwa sasa hana kazi
   
 17. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tanzania Daima

  Wassira azomewa mkutanoni  na Mwandishi wetu, Bunda
  JINAMIZI la zomeazomea limezidi kumwandama mbunge wa jimbo la Bunda, Steven Wasira, ambapo jana tena alizomewa na wananchi baada ya kushindwa kujibu maswali waliyomuuliza.

  Wassira alikumbwa na zahma hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani ya mjini Bunda.

  Katika mkutano huo, Wasira aliulizwa maswali matatu na kijana mmoja aitwaye Joashi Kunaga ambayo baadhi yalionekana kumkasirisha.

  Maswali hayo pamoja na kumtaka aeleze ni kwa nini eneo la Shule ya Msingi Balili limechukuliwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya, Chiku Galawa, ambaye sasa ni mkuu wa mkoa wa Tanga na wananchi walishalalamika lakini yeye hajawahi kulizungumzia.

  Swali la pili kijana huyo alitaka kufahamu ukosefu wa maji katika Hospital ya DDH Bunda ambako sasa hivi wagonjwa wanalazimika kutoa maji majumbani mwao huku wakati ziwa liko km 11 toka mjini Bunda.

  Katika swali lake la tatu alimuuliza kuwa katika mkutano huo alikuwa anahutubia kama mbunge, waziri au kada wa CCM kwani alitakiwa kufahamu kuwa Bunda ina wachama wa vyama vingi.

  Mwingine aliyeuliza swali ni mwenyekiti wa mtaa wa Nyerere, Maxmilian, aliyetaka kujua ni kwani nini halmashauri imetengeneza milango ya shule za sekondari za kata kwa shilingi laki nne kwa kila mlango.

  Baada ya kuulizwa maswali hayo Wassira alisimama katika hali iliyoonyesha kuwa ana hasira na kuaanza kujibu maswali hayo kwa ukali.

  Wassira alianza kujibu swali la kwanza la Kunaga akisema kuwa hawezi kulisemea hilo ni la watu wa ardhi kwa madai kuwa kama mtu alikuwa na pesa zake akaomba akapewa yeye hawezi kulizungumzia.

  Kuhusu suala la maji alisema kuwa maji yapo katika mchakato na kwamba wananchi watarajie kupata maji muda si mrefu jibu ambalo wananchi walilikataa na kudai kuwa ahadi zake kuhusu maji zimekuwa za uongo tangia mwaka 2007 hadi leo amekuwa akisema uongo.

  Akijibu kuhusu hoja ya yeye kuhutubia kama mbunge au waziri, Wassira alionekana kujawa na hasira na kuuliza kwa ukali, “Kwani Wenje alikuja kuhutubia hapa hivi karibuni kama nani?”

  Jibu hilo lilizidi kuwachefua wananchi ambao walianza kuzomea huku wakiimba: “People’s Power.”

  Wengine walisikika wakisema: “Afadhali Esther Bulaya kuliko wewe.”

  Jambo ambalo lilifanya polisi waliokuwepo kuanza kujiandaa kwa lolote na ndipo Wasira alipochukia na kuamua kuondoka majira ya saa 11 huku akiacha wananchi wakiwa bado na maswali ya kumuuliza.

  Hata hivyo baada ya kuondoka wananchi hususan kundi kubwa la vijana lililokuwepo mkutanoni hapo liliendelea kuimba: “People’s Power.” Huku wakinyoosha vidole viwili vinavyotumiwa na Chama cha CHADEMA na wengine wakilitaja sana jina la mbunge wa viti maalumu vijana Bulaya ambaye sasa anaonekana kuwa kipenzi cha Wanabunda kutokana na msimamo wake bungeni wa kutetea mambo mbalimbali likiwemo suala la kero ya maji ambalo ni tatizo kubwa kwa wananchi wa mji wa Bunda na vitingoji vyake.

  Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya Wassira kuondoka, baadhi ya wananchi walimtuhumu mbunge huyo kushindwa kujibu maswali aliyoulizwa wakisema kuwa kitendo hicho kinaonyesha alivyochoka kutokana na umri wake.

  Wananchi hao walimshutumu Wassira wakisema kuwa aliishawaona wananchi wa Bunda ni watu wa kudanganywa lakini safari hii wamechoshwa na hadithi zake.

  “Huyu mzee ni msanii; juzi alipoona anataka kufanya mkutano hapa aliwaita waandishi wa habari wa TV na magazeti wale wanaomsapoti akaandaa na mtambo wa kuchimba mtaro ambao ulichimba km chache na akachukua wajumbe wa bodi ya maji wakachukuliwa maoni na yeye akaongea lakini baada ya yeye kuondoka huko Nyabehu ule mtambo haupo tena na kazi hiyo haiendelei sasa leo anakuja kutupatia hadidu za rejea,” alisema mkazi mmoja Chacha Maswi mkazi wa kijiji cha Nyabehu.

  Hata hivyo mkutano huo ulihudhuriwa na watu wachache tofauti na siku nyingine lakini pia ukilinganisha na ule aliohutubia mbunge wa Nyamagana Eziekiel Wenje mwezi uliopita na wananchi wakakubali kunyeshewa mvua wakimsikiliza.

  Hali kadhalika idadi hiyo ya watu waliohudhuria mkutano huo wa Wassira pia haikufikia ile ya waliokuwepo juzi wakati Bulaya akikabidhi kombe la timu ya vijana wa Bunda mjini.
   
 18. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  tehe tehe swafi sana, hilo zee la gombe halina tija, umri ushamtupa mkono. Nadhani msisho wake umewadia peeoples power si mchezo bana
   
 19. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  kazi wanayo 2015
   
 20. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Bora asome alama za nyakati
   
Loading...